Uchaguzi 2020 Musoma yarindima Lissu akilakiwa kwa Shangwe kubwa, fomu za dhamana zajazwa

Uchaguzi 2020 Musoma yarindima Lissu akilakiwa kwa Shangwe kubwa, fomu za dhamana zajazwa

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kwahiyo mjipange kwa hilo "TUMEIBIWA"
Na kwasababu hilo neno tumeisha lisikia mara nyingi.
Sasa uje kivita uone moto wake mpaka mtakaosalimika mtakuwa wakimbizi hapo Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo lako unaongea ukiwa ndani ya chupa...!

Waliyo ndani ya chupa hawawezi kuona dunia ilivyobadilika...

Nchi hii ni ya Watanzania na wakiamua, hawashindwi kitu...!!

Nguvu ya umma (people's power) haiogopi risasi wala virungu wala mabomu ya machozi wala maji washawasha bro, wala NEC wala polisi wala TISS wala jeshi...

Mwaka huu ni mwaka wa kuiasi MAMLAKA HARAMU.

Ombeni tuwe wajinga kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

I am afraid to tell you that, IT'S TOO LATE NOW...
 
Jiwe kajificha anapanga nitoke vipi

Kapilimba alitoa taarifa ya kijasusi kuonyesha Lissu na Zitto ndio wanasiasa wenye ushawishi zaidi
Kuelekea uchaguzi 2020 akaishia kutumbuliwa sasa ndio naelewa kwamba idara ya usalama wa taifa inajuwa nani rais ajaye.
Hao ni watu wachache sana hata Diamond pekee anazidi hao akija kupiga mziki
 
Magufuli ni binadamu kama tulivyo binadamu wote. Anazo hulka zake kama kila binadamu alivyo na hula zake. Mojawapo ya hulka zake kuu (yaani zinazotawala ubinadamu wake) ni UKATILI.

Anaweza kuwa anajijua au la, lakini Magufuli ana hulka ya moyo wa ukatili. Ametumia Katiba yetu hii mbovu kuweka hulka yake katika vitendo.

Katiba yetu mbovu inampa uwezo Rais kuwa kama 'mungu mtu'. Na kama ana moyo huu kama alio nao Magufuli, basi watu wengi watateseka ( abuse of power). Watanzania walio wengi wameteseka kimya kimya kwa namna tofauti. Lakini hakuwa na bado hawana pahala pa kupazia sauti kulalamika dhidi ya abuse of power.

Wale waliokuwa wajanja, wakajipendekeza na kweli wakala na wanaendelea kula na 'kipofu' (mfano Wabunge na madiwani waliohama vyama vyao vya upinzani ili 'kuunga mkono juhudi').

Hiki tunachokiona na tutaendelea kukiona sana ni wananchi kupata pahala pa kupazia sauti zao, Watanzania wamepata tabu sana katika miaka hii mitano ya ukatili uliovalishwa koti la uzalendo. Sasa wanatema nyongo, chambilecho Waswahili wa kwetu!

Na tunafahamu kabisa kwamba hakuna jinsi ambavyo Tume ya Uchaguzi inavyoweza kutomtangaza kuwa ndiye mshindi wa urais (kwanza, hakuna hata uhakika kama Lissu ataruhusiwa na Tume kugombea), lakini jambo kubwa ama somo kubwa hadi muda huu ni kwamba Magufuli afungue macho na masikio (asikilize sauti kutoka upande mwingine) ili muhula wake wa pili aendelee na jitihada zake za kujenga miundombinu lakini ujenzi huo uambatane na kuwafanyia binadamu wenzie UTU. AACHE UKATILI.
 
CCM kupambana kwa hoja na Lissu hawataweza, watakachofanya ni kuangalia namna ya kumwengua kwenye mchakato kwa kutumia vyombo vyao yaani Tume ya uchaguzi mahakama..hii ndiyo the last option aliyonayo kwa sasa.!!
 
FISI hawamini kinachotokea...

Ngoja tuendelee shuhudia maajabu.

Kimyaaa
 
Lakini Mzee Kinana pale Dodoma aliwaambia hakuna uchaguzi mwepesi!kabla Lissu CCM walijua mambo hayatakuwa kamailivo leo.Kinana aliona ambalo CCM karibu wote hawakuliona
 
Jiwe kajificha anapanga nitoke vipi

Kapilimba alitoa taarifa ya kijasusi kuonyesha Lissu na Zitto ndio wanasiasa wenye ushawishi zaidi
Kuelekea uchaguzi 2020 akaishia kutumbuliwa sasa ndio naelewa kwamba idara ya usalama wa taifa inajuwa nani rais ajaye.

Kadanganye wajinga, huyo alikuwa na mradi wa kujenga hofu na kutengeneza mazingira.
 
Kwa kiasi cha watu kujitokeza na kungalia au kushangilia sio kigezo cha kuwa unakubalika tuu au unapendwa saana.

Kuna wengine wanajiokeza kwa kuwa umeenda kwao au hawajawahi kukuona live ndio wanatumia fursa hiyo kukuona tuu na kujiridhisha tuu,hivyo idada a watu sio kigezo cha kujipa matumaini kuwa kwenye sanduku la kura lazima ushinde kwa ushindi mkubwa kama mnavyojitanabaisha. Hivyo msione umati wa watu mkadhani siku ya kura itakuwa hivyo hivyo.watanzania sio wajinga kama mnavyowadhania siku hizi watu waeelimika tofauti na chaguzi zilizopita awamu zote 4.
Niwatakie maandalizi mema ya kampeni.
Tukutane Oktoba.
 
Back
Top Bottom