Magufuli ni binadamu kama tulivyo binadamu wote. Anazo hulka zake kama kila binadamu alivyo na hula zake. Mojawapo ya hulka zake kuu (yaani zinazotawala ubinadamu wake) ni UKATILI.
Anaweza kuwa anajijua au la, lakini Magufuli ana hulka ya moyo wa ukatili. Ametumia Katiba yetu hii mbovu kuweka hulka yake katika vitendo.
Katiba yetu mbovu inampa uwezo Rais kuwa kama 'mungu mtu'. Na kama ana moyo huu kama alio nao Magufuli, basi watu wengi watateseka ( abuse of power). Watanzania walio wengi wameteseka kimya kimya kwa namna tofauti. Lakini hakuwa na bado hawana pahala pa kupazia sauti kulalamika dhidi ya abuse of power.
Wale waliokuwa wajanja, wakajipendekeza na kweli wakala na wanaendelea kula na 'kipofu' (mfano Wabunge na madiwani waliohama vyama vyao vya upinzani ili 'kuunga mkono juhudi').
Hiki tunachokiona na tutaendelea kukiona sana ni wananchi kupata pahala pa kupazia sauti zao, Watanzania wamepata tabu sana katika miaka hii mitano ya ukatili uliovalishwa koti la uzalendo. Sasa wanatema nyongo, chambilecho Waswahili wa kwetu!
Na tunafahamu kabisa kwamba hakuna jinsi ambavyo Tume ya Uchaguzi inavyoweza kutomtangaza kuwa ndiye mshindi wa urais (kwanza, hakuna hata uhakika kama Lissu ataruhusiwa na Tume kugombea), lakini jambo kubwa ama somo kubwa hadi muda huu ni kwamba Magufuli afungue macho na masikio (asikilize sauti kutoka upande mwingine) ili muhula wake wa pili aendelee na jitihada zake za kujenga miundombinu lakini ujenzi huo uambatane na kuwafanyia binadamu wenzie UTU. AACHE UKATILI.