Lucha
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 14,516
- 50,658
Kwahiyo dogo kweli ni mwizi , nazi zimepangwa kwanini uokote?
Hata kama ni Mwizi je Mwakinyo alistahili kufanya hayo aliyoyafanya ikiwa alifanikiwa kumdhibiti? Kwanini asimpeleke polisi.Kwa mwonekano wa dogo kuna uwezekano mkubwa kuwa ni mwizi ila haitoi uhalali wa Mwakinyo kufanya alichofanya. Huyu bondia wa kimataifa hajui kuwa tuko enzi za digitally kwamba alichofanya Tanga kinajulikana hadi New York muda huohuo?
Wananchi wanasema siyo tukio la kwanza Mwakinyo kufanya hivyo huyo ni mtu wa nne hapo mtaani yupo aliewahi kumchoma na pasi je ni sawa?
Binafsi naona mwakinyo kafeli kuishi na jamii yake, mtaa mzima wazee, wanawake , vijana kukukataa ni kupoteza, inaonekana haishi kwa wema na majirani zake, hao ndo walitakiwa kuwa mashabiki zake wa kwanza ila katengeneza nao uadui kwa status yake ku attempt murder kisa nazi ni mambo yasiyoingia akilini, ni hulka tu ya ukorofi ndo ina influence hayo matukio