Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Muda mwingine bora msomi aliyeishia darasa la saba kuliko hao Maprofesa wanaoendeshwa na matumbo yao!
(Kusoma sana sio kuwa na akili)
Ni kauli za walioshindwa kuendelea kusoma. Msomi ni msomi tu, mfumo wa kumfanya mwanasiasa awe juu ya mwanataaluma ndio unaowafanya walazimishwe kutoka nje ya weledi wao
 
Kwahiyo sasa hivi kimefanyika kuhusu na corona?
 
Ule wa mapapai ulikuwa ni nini bwashee?
Ulifanyika maabara ya Chato.
Ukiwaambia watu waliopoteza wapendwa wao kwamba Tanzania haijawahi kuwa na Corona kwa sababu ya vipimo vya mapapai alivyotangaza yule kiongozi mwongo kuwahi kutokea nchini watakupiga mawe. Bora hata Nyerere alikuwa anaangalia TV peke yake usiku, asubuhi anatutangazia yatakayotokea nje ya nchi na jioni tunatangaziwa BBC tunamwona mnajimu.
 
Kwa mara ya kwanza kabisa leo namuunga mkono huyu #teamla7
 
Msukuma ana ugomvi mkubwa sana na wasomi sijui kwanini.

Na anageuza habari! Hao maprofesa wakati wa JPM ni lini walifanya utafiti wakagundua Tanzania hakuna korona? Hakukuwa utafiti wowote isipokuwa kulikuwa na matamko kuwa Tanzania hakuna korona
Hata sasa hao Maprofesa hawajafanya utafiti zaidi ya kuja na mapendekezo tu.
 
Yeye kipindi cha mwendazake akili aliipeleka wapi?

Juzi kati hapa si kasema watu walinyang'anywa viwanda kimakosa?
Enzo hizi lazima akili zimrudi,na hao aliowakandia wakati fulani nizamu yao kumburuza,awe mpole kutesa kwa zamu.
 
Muda mwingine bora msomi aliyeishia darasa la saba kuliko hao Maprofesa wanaoendeshwa na matumbo yao!
(Kusoma sana sio kuwa na akili)
Endelea kujifariji,pia kumbuka hayo yananafasi kwa mazingira ya Tz na zaidi Afrika
 
Ule wa mapapai ulikuwa ni nini bwashee?
Ule haukufanywa na ma Professa ulifanywa na Magu mwenyewe, alikusanya zile sample akazipa majina ya uongo na kupeleka maabara ya taifa, majibu yakaja positive, ndio yeye mwenyewe akapinga...wala hakuna Profesa aliyefanya vile....pengine Kabu..
 
Ule haukuwa utafiti kuwa Tanzania hakuna korona, isipokuwa ulikuwa utafiti kuwa korona hata kwenye mapapai inaonekana. (Labda mchato alitaka kuiaminisha dunia kuwa corona is a Hoax)
Ule utafiti ulikuwa unahusu utata wa vipimo vya corona.
 
Msiwalishe maneno ma Profesa, aliyesema hivi ni Hayati Magu...maprofesa walikaa kimya hawakusema...
 
Msiwalishe maneno ma Profesa, aliyesema hivi ni Hayati Magu...maprofesa walikaa kimya hawakusema...
Magu alisema kutokana na waliyoyasema matokeo ya utafiti uliofanywa na wachunguzi/maprofesa/doctors na wanausalama aliowatuma
 
Wameambiwa na Rais Samia kuwa ni ruksa kuikosoa serikali.sasa Msukuma alitakiwa tu ajiulize wakati wa magufuli kwanini haikusa ruksa kuikosoa serikali?
 
Yeye si alikuwa anapiga nyugu alikuwa anajikinga na nini kwani ? Aendelee na uganga wake wa kienyeji awaache wataalamu wavae barakoa na chanjo
 
Wameambiwa na Rais Samia kuwa ni ruksa kuikosoa serikali.sasa Msukuma alitakiwa tu ajiulize wakati wa magufuli kwanini haikusa ruksa kuikosoa serikali?
Kwani walikatazwa, mbona Bashe alikuwa anakosoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…