Form seven ni Shida, yaani yeye anadhani kipindi cha utawala ULE yale maamuzi ya kupinga na Kuficha kuwa Corona haikuwepo yanaweza ku-hold water kwa kiongozi wa sasa mwenye Maono (uongozi sikivu). Hivi ni kweli huyo form Seven hajui hasara ya kupoteza wapendwa wetu kwa Maamuzi ya ajabu ajabu. Mimi Ilikuja kunizidishia machungu na niliuchukia utawala ule zaidi tena Zaidi pale tu Dada yangu Daktari alipofariki kwa corona and was the only Dr in our family. Baba alikuwa anatuambia alimsomesha kwa gharama kubwa. Tumwombe tu huyo form seven hasiturudishe matesoni,kwani maamuzi ya uongozi wa sasa kuhusu Corona (task force ya kumshauri SSH kuhusu Corona) ni sahihi na yaheshimiwe. Anachojifanya hajui ni kuwa, Watawala uliopita Ulikuwa unaogopwa, ulikuwa utawala wa YES BOSS or ONE MAN SHOW kila alichokisema mtawala ndicho wasaidizi wake walikitenda na kutuaminisha kuwa tuko sahihi ili mradi tu Maisha na familia zao vilineemeka na utawala ule.