Hili ni jambo la kuogofya sana linaelekea kutokea nchini, serikali imepeeleka mswada bungeni ili kumuongezea kinga rais na viongozi wengine wa bunge na mahakama kinga dhidi ya kushatakiwa moja kwa moja kwa kukiuka katiba ya nchi.
Huu ni mswada wa ajabu na wa kuogofya sana, mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi inakuwaje leo anatafuta uhuru wa kuivunja katiba hiyohiyo?
Inakuaje marais wengine wote waliotangulia hawakuona kikwazo chochote kwenye kufuata katiba lakini huyu wa sasa kwake yeye katiba imekua kero kwake?
Ni nini hatma ya nchi yetu ikiwa tutaruhusu ujinga wa namna hii kuendelea kutokea? Unajua hata Adolf Hitler aliingia madarakani kwa njia halali kabisa, lakini taratibu akaanza kujiongezea mamlaka na kuwanyamazisha wote aliowaona kuwa kikwazo. Mwisho wake sote tunajua kilichotokea. Binadamu wote ni corrupt kwa viwango tofauti tofauti, hauwezi kumpa binadamu mwezako mamlaka yasiyo na mipaka, mwisho wake ni mbaya tu.
Wito wangu kwa wote mlioapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati wenu ni sasa kufanya hivyo, the republic as we know it is under attack.