Unaweza kunionyesha andiko LOLOTE linalotaja POMBE? Walevi na walafi wa pombe hujaribu kuyapindua maandiko kwa kueneza uongo. Haya, lete aya yenye neno pombe ama alcohol.
Hebu pitia kidogo hapa mtumishi.
Kumbukumbu la Torati 14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako.
Pombe maana yake ni kinywaji kinacholevya au kileo.
Ni kwamba hakijakatazwa bali kinywewe kwa kiasi na kwa wakati wake na sio kiulevi. kama vile chakula kuepusha ulafi.