Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Unaelewa nini kwenye sentensi hii:
Muda wangu bado?
 
Hii nimeiskia kwenye ngoma ya dj khaleed jayz kasema 'jesus turned water to wine
for hov it's just need stov....



Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Hii idea ya fungu la kumi ni utata mtupu, yaani kabisa 10% nimpelekee mchungaji akaitumie anavyotaka yeye? bora ingekuwa 1% ningeelewa kidogo maana kanisa halina biashara (income)
 
Unaweza kunionyesha andiko LOLOTE linalotaja POMBE? Walevi na walafi wa pombe hujaribu kuyapindua maandiko kwa kueneza uongo. Haya, lete aya yenye neno pombe ama alcohol.
Hebu pitia kidogo hapa mtumishi.

Kumbukumbu la Torati 14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;

25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako.

Pombe maana yake ni kinywaji kinacholevya au kileo.
Ni kwamba hakijakatazwa bali kinywewe kwa kiasi na kwa wakati wake na sio kiulevi. kama vile chakula kuepusha ulafi.
 
Mkuu, hapa si suala la Ubishi, mimi nimekuomba unithibitishie kuwa Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua na Kilevi, mbona bado unakwepa kuutoa huo uthibitisho wa Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua na Kilevi?

Kama mpaka sasa haujatoa uthibitisho, unapata wapi confidence ya kusema Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua na Kilevi?
Mimi najua divai zote zina kilevi na sijawahi iona divai isiyo na kilevi.

Kwetu Roman Cathoric ndio tunayo itumia kumega mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wa mateso ya Bwana Yesu.

Kama wewe umeiona na unathitibisha kuwa ndiyo aliyotengeneza isiyo na kilevi yaani divai juice, basi uwanja ni wako lete huo ushahidi hapa tuusome.

Kwangu mimi ushahidi wa Kibiblia ni huu hapa unaoutaka.

Mwanzo 9:20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

Je wanalewaga divai juice ?
 
Mimi najua divai zote zina kilevi na sijawahi iona divai isiyo na kilevi.

Kwetu Roman Cathoric ndio tunayo itumia kumega mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wa mateso ya Bwana Yesu.

Kama wewe umeiona na unathitibisha kuwa ndiyo aliyotengeneza isiyo na kilevi yaani divai juice, basi uwanja ni wako lete huo ushahidi hapa tuusome.

Kwangu mimi ushahidi wa Kibiblia ni huu hapa unaoutaka.

Mwanzo 9:20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

Je wanalewaga divai juice ?
Na wapeni kilevi ili wasahau shida zao Kwa muda wapate kusikia neno
KRNT 9:17-1
 
Na wapeni kilevi ili wasahau shida zao Kwa muda wapate kusikia neno
KRNT 9:17-1
Sisi wachungaji tukiwa madhabahuni tunahubiri kuwa pombe sio kinywaji kizuri. Na kuwazuia waumini kunywa pombe halari.

Unajua ni kwa sababu gani ?

Ukiwawaambia waumini ruksa kunywa pombe kwa kiasi utasababisha baadhi ya waumini kuwa walevi.

Kwanini.

Kuna mtu akinywa glasi moja tu ya Safari lager, anaharibika kabisa kimwili na kiroho na kuwa mlevi.

Kilevi kinawafaa wenye hekima, busara na nguvu. Wanaojua majira ya kunywa kwa kiasi na ya kufanya kazi njema, na kumtukuza Mungu mwenye wingi wa Hekima na Nguvu.

Kama ni mtumishi usije kuthubutu kuwaambia waumini watumie kilevi. Kwakuwa kuna baadhi ya waumini hawana kabisa uwezo wa kutumia kilevi, wala kuweza kuhimili mikiki mikiki yake.
 
Unataka kusema YESU ALIKUWA CHAPOMBE?
Hakuwa cha pombe ila yesu mwenyewe kasema alikuwa anakunywa pombe sikia haya maneno ya yesu mwenyewe ...yesu anasema yohana alikuja anyi pombe wala ...wakasema ana pepo bali mimi nimekuja nakunywa wakasema mlevi na mrafi
 
Aya ya 9.
Muwe mnasoma maandiko yenu jamani.View attachment 2066759
Sasa wewe mbona umechanganya madesa ...unajua maana ya wasinye pombe wala divai wakupanapo kwenye hema ya kukutania ...unajua hiyo hema maana yake ni nini ? Tena wale wanao sema divai siyo pombe waje hapa wajibu kwanini mungu amekataza kunywa pombe wala divai wakutanapo kwenye hema la kukutania ? Kwani kula zabibu ni kosa kukutana kwenye hema huku umekula zabibu au juice ya zabibu ? Hapo tunaona mungu anawakataza kila aina ya kilevi kwa watu wanao taka kuingia kwenye hema ya kukutania ambayo ni hekalu.
 
Yes kaka. Jana nilikunywa ALTAR wine (divai ya madhahabuni) nikalewa.
Divai ni pombe ndiyo maana mungu alipowaambia wana wa Israel wajitakase alikataza pia wasinywe divai ila awakukatazwa kula zabibu sasa kama divai ni maji ya zabibu yasiyo na kileo kwanini mungu alikataza kunya wakati wa kujitakasa ...tena yesu mwenyewe ana sema "yohana alikuja ali wala anywi wakasema ana pepo mimi nimekuja nakula na nakunywa wakasema mlafi na mlevi"
 
Back
Top Bottom