Muungano bado una shida nyingi tusidanganyane

Usitudanganye hawa mwaka juzi walijitoa kwenye muungano na PM wao akaachia ngazi, muungano gani huu ambao wazanzibar pekee wamejaa huku kwetu(kwenye system) sisi kule tunachukuliwa kama watalii au vibarua wao, taja faida 3 ambazo sisi Tanganyika tunazipata? ukizitaja kuanzia tarehe 1-1-2024 hutoniona JF maisha yangu yote. Nchi za wenzetu muungano unapigiwa kura na wananchi na siyo maamuzi ya kamati kuu ya CCM pekee.
 
Nyerere alikuwa mnafiki sana.Aliua Tanganyika kwa maslahi yao
Nyerere alikuwa na akili zilizopitiliza, aliwaza miaka 100 ijayo hakutakuwa na mzamzibar asilia fundamentalists atatawala Zanzibar. Tuendelee TU kusogeleana, kuoana na kuishi pamoja. Siku hizi hata wamasai wanapatikana Zanzibar kwa wingi.. jitahidini sana kila mtanganyika aoe mzamzibar, ikishindikana zaeni nao watoto na kuwasomesha vya kutosha elmu dunia.
 
Wao wako 1m TU, hata wakijazana Huku hawana athari. Kumbuka kuwa kuwa wao hawana jeshi Wala fedha yao. Rais wao lazima achaguliwe huku Dodoma. Hawaruhusiwi kuwa na Rais wao ambae hakubaliki Tanganyika.
 
Kosa kubwa hili la kihistoria alifanya Nyerere. Lakin muda c mrefu tutafanya kama India kule cashmir
 
Hii ndio point ya msingi sana, kiutendaji na kiutawala itarahisisha sana. Inakera Rais wa nchi mpaka aende Wilayani Masasi ndio aambiwe changamoto za hospital,maji, umeme nk, wakati pale masasi kuna viongozi chungu nzima na rasilimali zote muhimu, wanachopaswa na full authority ya kujitawala.

Uwajibikaji:
Kwa sasa mkurugenzi wa wilaya au mkoa akizingua labda ametumia rasilimali vibaya, ufisadi nk... sio mkuu wa wilaya/mkoa, naibu waziri Tamisemi, waziri Tamisemi, naibu waziri mkuu, waziri mkuu, makamu wa Rais anayeweza kumtoa, wote wanasubiri mtukufu Rais aamue.. nchi hii ina wakurugenzi wangapi? Wakuu wa wilaya wanagapi? Rais atawezaje kuwamanage wote hawa?

Kwanini tusitengeneze serikali za majimbo? Ambazo zitajitawala zenyewe? Zitumie rasimali zilizopo kila mmoj kujiletea maendeleo..
 
Tukisema ipigwe kura ya kuuvunja muungano. Kule Zanzibar lazima yatatokea machafuko maana ni wanafiki
 
Fikiria mwenye kama inawezekana. Zanzibar 1+ milioni Ina rais 1. Kwa cross multiplication zako Tanganyika watu 60 + mil ilitakiwa kuwa na Marais 60!!!
 
Fikiria mwenye kama inawezekana. Zanzibar 1+ milioni Ina rais 1. Kwa cross multiplication zako Tanganyika watu 60 + mil ilitakiwa kuwa na Marais 60!!!
🀣🀣🀣
 
Kama ulimsoma mjukuu ukahisi ameona una.zingua ndivyo ilivyo wengi wanaona miyeyusho tu!
Inaelekea nchi nzima imeambukizwa ugonjwa wa CHADEMA kuburuzwa kama kondoo na viongozi / watawala!!
 
πŸ’¬πŸ’­πŸ™
 
πŸ’­πŸ’¬πŸ™
 
πŸ™
 
🀣🀣🀣
 
🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…