Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Zanzibar has a great future chini ya muungano kama wakiamua. Sidhani kama wanaweza kujimudu peke yao. Natumia sidhani maana sida economic au social data za ku-support hii and i have no time to research.

Wamekuwa ndani ya muungano miaka yote hiyo wameendelea kushea umaskini na Tanganyika.
Mbona Mauritius na Sychelles wako kivyao hawajaungana na mozambiki na wanazidi kupaa kimaendeleo? Labda tukiwaachia hata ufisadi kwao itakuwa historia.
 
Fact: zanzibar mwaka jana wamekusanya kodi $20m kwa mwaka na wamesamehe $19m. (ilikua ni mzozo sana mwaka jana kwenye baraza la wawakilishi). bara wanakusanya kodi $300m kwa mwezi na sio $20m kwa mawaka. Kwa hiyo ukae ukijua bajeti ya zanzibar inafadhiliwa na bara.
acha kudanganya watu wewe mshamba! kama bara waifadhili Zanzibar ,sasa Zanzibar haitaki kufadhiliwa na bara. kila mtu aangalie mpango wake. huu muungano ni kutiana umasikini tu. hali ya maisha ni mbovu Zanzibar kwasababu ya muungano!
 
Kinacho boa ni Z'bar kila kitu sasa wanataka kufanya kivyao na hawaishi kulalamika. Wana serikali yao wenyewe, bendera yao wenyewe, national anthem yao wenyewe etc which is more than Bara can say. Hivi wana ringia nini haswa? Hata airport ya kimataifa I doubt wanayo. I think as time goes by wazanzibar are getting facts & dreams confused na ever since haya mafuta yagunduliwe ndiyo imekuwa tabu kabisa. Wamekuwa kama watoto wanaotaka kupewa kila kitu wanacho taka. Kwenye vitu vya kwao basi ni vya zanzibar tu vya bara ni vya wote. Hivi umeme wa zanibar unatoka wapi? Si bara? basi nasisi tuseme umeme wakwetu? Ukweli ni kwamba muungano can be a beautiful thing but if one side doesn't want it hata kama stratigically muungano ni muhimu vipi ni bora tuachane. Hata kwenye ndoa mmoja akingangania divorce au sijui afanye mambo yake mwenyewe basi ndoa ita vunjika. The yes or no uestion I have for zanzibar is MNATAKA MUUNGANO YES OR NO? Kama mnautaka basi lets be adults tutafakari cha kufanya kama hamtaki kueni direct siyo kulete mambo ya chini chini.
hatutaki muungano. huu muungano ndio unaitia zanzibar umasikini. kila mtu aangalie mpango wake. munatuleta wizi wa mali asili. hebu jiulize wewe unafaidika na nini kutoka katika maadini ya bara. sisi hatutaki. zanzibar can be better without so called "muungano" please try to fix your own problems first before you talk about zanzibar.
 
Wakati watanzania leo wanadhimisha miaka 45 ya Muungano wa Tanyanyika na Zanzibar, Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud amesema wakati umefika Serikali ya Tanganyika ikarejeshwa.

Hayo ameyaeleza katika mada yake iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria Ali Omar ambalo limewashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri wasomi, na viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo wa CCM na CUF.

Aboud alisema kwamba serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya muungano kwa upande wa Tanzania bara ili kuwa na mfumo kama unaotumika Zanzibar.

Amesema tangu kufikiwa kwa Muungano serikali ya Zanzibar imekuwa na katiba na serikali yake ambayo inasimamia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.

“kwa kutumia katiba ya Tanganyika iundwe serikali ya Tanganyika inayoshughulikia mambo yake ambayo sio ya Muuungano” alisema Enzi katika mada yake hiyo.

Alisema kwamba uchumi wa Zanzibar umekuwa ukififia kutokana na vikwazo mbali mbali vilivyomo katika mfumo wa muungano na kushauri Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika jumuiya za kimataifa ili iweze kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi wake.

Vile vile alisema mbali na kurejeshwa na serikali ya Tanganyika pia katiba ya Tanganyika inapaswa kuwepo ili iweze kusimamia mambo ya ndani ya Tanganyika na mambo ya Muungano yashughulikiwe na serikali ya Muungano.

Aboud ambaye ni Mwadhishi wa habari mkongwe aliewahi kufanya kazi katiak vyombo vya habari kadhaa ya Tanzania Bara na kukamata nafasi za juu za serikali ya Zanzibar na ndani ya Chama CCM alisema kwamba wakati umefika mkataba wa awali wa muungano ukapelekwa katika baraza la wawakilishi ili wajumbe wapata nafasi ya kuridhia mkataba huo.

“Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambao ni baraza la wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huu ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar” alisema Kiongozi huyo.

Alisema mkataba huo wa Muungano baada ya kufikiwa mwaka 1964 uliridhiwa na upande mmoja wa muungano lakini baraza la kutunga sheria wakati huo Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikupewa nafasi ya kuridhia

Kiongozi huyo mwandamizi amesema kwamba orodha ya mambo ya muungano hivi sasa imeongezeka kutoka 11 hadi 38 na kuzua mjadala mrefu kutoka pande mbili za muungano kwa vile umefuta baadhi ya mambo ya msingi yaliokuwemo awali katika orodha ya mambo ya muungano.

“Hakuna awezae kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake muungano huu umejengeka kutokana na khofu, kutiliana shaka na kutoaminiana baina ya pande mbili zinazounda ambapo wakati mwengine hupelekea hata kutishia uhai wa muungano wenyewe” alisema Aboud katika mada yake.

Kiongozi huyo mwandamizi wa SMZ alikumbusha historia ya Rais wa awamu ya pili Aboud Jumbe Mwinyi alipolazimishwa kujiuzulu pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi wake Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake sita waliokuwa na msimamo wa kutaka kuitishwa kura ya maoni kuhusu Muungano.

Hata hivyo alisema kwamba nafasi bado ipo ya kutosha ya kutatua kero za muungano lakini lazima mijadala yake ifanyike kwa uwazi na kuweka mbele maslahi ya taifa hasa katika maeneo ya kiuchumi na misingi ya kuendeleza muungano wenyewe.

Kongamano hilo limefuatia maandamano yalizuwiwa kuunga mkono suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya muungano kama ilivyopendekezwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi Zanzibar.

Mapema juzi Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam alisema suala la mafuta na gesi asilia ni suala la kikatiba na linapaswa kujadiliwa na mabaraza ya kutunga sheria na sio jumuiya au taasisi nyengine hivyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo.

Wakishangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baadhi ya washiriki walisema tatizo kubwa linaloukabili muungano ni kuwa wananchi hawajashirikishwa kabla ya kufikiwa muungano huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa UPDP Haji Othman Haji alisema kwamba muungano ulifikiwa kwa mamuzi ya Nyerere na Karume lakini wananchi hawakupewa muda wa kutosha wa kufikiria na kuamua katika suala hilo.

“Tatizo kubwa linalokabili muungano wetu wananchi hatukupata nafasi ya kutosha kuamua kwa vile ilikuwa ni makubaliano ya viongozi wawili kwa niaba ya wananchi wao” alisema kiongozi huyo.

Professa Abdul Sharif ambaye ni mtafiti wa mambo ya historia alisema wananchi katika taifa wamegawanyika kutokana na mitizamo tofauti kuhsuu muungano ambapo wapo wanaofikiria muungano uvunje na uundwe upya ili kuwepo na muungano wenye mashahi ya kiuchumi badala ya kisiasa pekee.

Kwa upande wa Ali Mohammed Said alisema wananchi wajadili uhalali wa muungano wenyewe badala ya kujadili kero za muungano kwa kile alichodai kuwa ufumbuzi wa mambo ya muungano ni kurudi kuangalia mfumo wa muungano.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Ustadh Farid Hadi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuondoa woga na kujadili kwa uwazi matatizo yanayoukabili muungano kwa maslahi ya wananchi wake na vizazi vijavyo.

“Watu waondoshe khofu wawe huru kujadili ikiwa wewe mzee wa miaka 70 au 65 sijui unaogopa nini kwa vile umekuwepo miaka mingi lakini umeshindwa kuelezea ukweli juu ya muungano” alieleza Ustadh huyo.

Kongamano hilo limefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji ambapo mada tatu zimewasilishwa ikiwemo Athari za Muungano kwa Uchumi wa Zanzibar, Athari za Muungano kwa Utamaduni wa Zanzibar na Zanzibar katika Muungano ambapo awali Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna alitarajiwa kulifungua lakini hakuhudhuria kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kikazi.
 
..hakuna haja ya kuanzisha serikali ya Tanganyika.

..masuala ya Tanganyika yanashughulikiwa na serikali ya Muungano.

..kama Zanzibar hawako tayari kuvunja SMZ na masuala yote yashughulikiwe na serikali ya Muungano basi wachukue hatua za kujitoa ktk Muungano.

NB:

..msimamo wangu mimi huu Muungano uvunjwe tu.
 
Naomba kuuliza wana wa Jamii,

Kama tunaweza kuita Zanzibar Zanzibar, wakati Tanganyika na Zanzibar ndio zinazofanya Tanzania, je itakuwa sahihi kutamka Tanzania Bara Na Tanzania Visiwani?

Kama tunaweza kutamka Tanzania na Zanzibar; Kwa mantiki hiyo hakuna Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Wakati sasa hivi nchi nyingi zimeungana kwa mfano, EU sisi huku bado tu tunamawazo ya kujitenga.

Vunjeni tu huo Muungano mkae mjadiliane! Who is the loser? Saa nyingine kuvunja uhusiano ndio inakuwa njia mbadala ya kuujenga uhusino huo,
Vunjeni!
 
Mmemsikia Kiongozi muandamizi kutoka ofisi ya Waziri kiongozi (Prime Minister) kama haitoshi hapo kuna mkusanyiko wa viongozi wa CCM na CUF hii ni kuwaonyesha wazi WaTanganyika kuwa WaZanzibari wanaelekea kuungana kikamilifu la muhimu si kushindana nao ,itakuwa mnakosea ni lazima na nyinyi mjiulize iko wapi Serikali ya Tanganyika ?

Juzi nilisema matatizo ya Muungano hayawezi kutatuliwa ikiwa Tanganyika haipo ,itakuwa ni kuionea Tanganyika na WaTanganyika ,maamuzi yatakayopatikana yanaweza yakapata tabu ingine baadae ,anaweza baada ya miaka akazuka mtu na kusema ,hili na lile liliamuliwa Tanganyika iliwakilishwaje wakati ilikuwa haipo ? Zanzibar ilitumia mwanya wa kutokuwepo Tanganyika na kuamua mambo ambayo Serikali ya kushauriwa ya Tanganyika haipo ,hatulikubali.

Hivyo la muhimu ni kuirudisha serikali ya Tanganyika ,ifahamike tu kuwa hapa hapavunjwi Muungano maana kama hata ni kuuvunja basi ni lazima Bibi Tanganyika awepo ili Bwana Zanzibar atoe talaka. 😀
 
wabara ndio wanaoungangania huu muungano Zanzibar hawautaki
 
Last edited:
Moja ya matatizo makubwa sana nchini ni kwamba we are not informed. Tuliambiwa kwamba wahusika, mawaziri wa muungano, wanasheria wakuu n.k, wameagizwa wakae watatue kero za muungano. (Kwa wamazo ya kina Pinda, that blowhard Shamhuna na Idi Pandu na Mwanyika, wanaweza wakakaa waka solve huu Muungano.)

Walifikia tamati gani, hakuna kiongozi aliyetuhabarisha, hakuna mwandishi aliyeuliza, hatujui, we don't know nothing. Imekuwaje hili swala la Muungano limeibuka tena, si walisema wamekaa kulisuluhisha?
 
Maslahi tu binafsi ya kisiasa hapa!

Watu wanatafuta vyeo vya kisiasa hapa!

Mzalendo,

Mimi ni mtu, ni memba hapa

Kuna memba wengi humu, ni watu! wewe mmoja wapo

Je ni kweli, watu wanatafuta vyeo vya kisiasa hapa?

Naomba kusahihisha.
 
..kama CUF wako serious hawataki Muungano basi ni vizuri hizi hoja zao wakazizungumzia ndani ya Bunge la Muungano.

..sasa hivi kuna kikao cha Bunge kinaendelea sasa tunasubiri kusikia CUF wakileta hoja ya kuvunja Muungano, au kuunda serikali ya Tanganyika.
 
..kama CUF wako serious hawataki Muungano basi ni vizuri hizi hoja zao wakazizungumzia ndani ya Bunge la Muungano.

..sasa hivi kuna kikao cha Bunge kinaendelea sasa tunasubiri kusikia CUF wakileta hoja ya kuvunja Muungano, au kuunda serikali ya Tanganyika.
Joka wacha kukurupuka aliesema ni Kiongozi Mwandamizi katika Ofisi ya WaZiri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (CCM) akiwasemea wananchi ,hili si la CUF au CCM ni la WaZanzibari wote na ndio kama unavyoona hata Waziri kiongozi alikuwa awepo lakini akaambiwa akae pembeni zamu yao bado.

Kashkash za CUF hamziwezi msitafute kuita majeshi na mapolisi bure.
 
Mwiba said:
Joka wacha kukurupuka aliesema ni Kiongozi Mwandamizi katika Ofisi ya WaZiri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (CCM) akiwasemea wananchi ,hili si la CUF au CCM ni la WaZanzibari wote na ndio kama unavyoona hata Waziri kiongozi alikuwa awepo lakini akaambiwa akae pembeni zamu yao bado.

Kashkash za CUF hamziwezi msitafute kuita majeshi na mapolisi bure.

Mwiba,

..kikao cha Bunge kinaendelea Dodoma wiki ijayo.

..tusubiri kama Mzanzibari yoyote na atatamka kwamba Watanganyika wanawanyonya wa-Zanzibari.

..tuone kama kuna Mzanzibari atarudia kile alichosema Juma Duni kwamba wa-Tanganyika wanaharibu utamaduni wa wa-Zanzibari.
 
Basi waondoke. Nani kawazuia?

Anaewazuia ni Inspekta General Saidi Mwema na Commissioner wa Polisi Khamis Mohamed Simba.

Wamewaambia wazee 12 wenye saini 27,000 na wabunge 6 wa CUF kwamba wanafanya uhaini kwa ku sapoti petition Umoja wa Mataifa wakitaka kujitoa. Wakawatia kizuizini.
 
Wanaotakiwa kudai serikali ya Tanganyika ni Watanganyika wenyewe na si Wazanzibar.

Wazanzibar wana haki ya kudai mambo mengine yote, hili la kudai serikali ya Tanganyika si lao wala hawatakiwi kuwa na uchungu nalo.

Mimi kama Mtanzania kutoka ilokuwa Tanganyika sijawahi kumwomba hata mzanzibari mmoja kunisemea ili kudai serikali ya Tanganyika.

Hoja hii ya baadhi ya Wazanzibari ni hoja ya kukemewa vikali, kwa sababu lengo lake ni kurudisha nyuma hoja nzima ya kujadiri kero za muungano ambazo wote tunajua zipo na kamwe hazitakaa ziondoke mpaka sisi Watanzania wenyewe tuweke makalio yetu chini na kuzijadiri kwa kina na kuzitolea ufumbuzi wa kisheria.

Wote tumechoka kukoromewa na watu wanaojifanya kutetea muungano kwa misuli yao bila kuweka akili zao katika utetezi.
Lakini hatuwezi vumilia vitendo vya kuvuruga mambo na kuingilia haki za watu wengine na kuleta madai ambayo kisheria wasemaji hawana uwezo wa kuajadiri.

Kama hoja ya kudai Zanzibar hruru isiyokuwa mshiriki wa Muungano wa Tanzania haiwezi simama kwa miguu yake yenyewe mpaka hoja ya kudai Tanganyika iwekwe mezani, basi hoja ya kudai Zanzibar haina nguvu na pengine itakufa kwa kujikaba yenyewe kuliko kuuawa na watu.

Labda tu kama kuna maana nyingine ambayo mtoa hoja anaweza kuianisha, Sivyo "Shut Up and Drive".
 
wabara ndio wanaoungangania huu muungano Zanzibar hawautaki

Basi waondoke. Nani kawazuia?

Tee..hee.. hii yanikumbusha kwenye ndoa - hivi nani anatakiwa afungashe na kuondoka ? Anayeona hapendwi (anaonewa, hathaminiwi) au yule ambaye bado anapenda. Nafikiri hapa hakuna cha kuondoka mtu bali kuna wivu tu wa kutaka apendwe zaidi - wivu wa kike ? Nani tena huyu anataka kulitia doa penzi kati ya Tanganyika na kisiwa cha karafuu ?
 
Back
Top Bottom