Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano upo ICU haihitajiki Elimu ya juu kutambua Hilo hata wa darasa la pili anajua Kuwa Tanganyika anachunwa Kama buzi huku Zanzibar wakijiimarisha kwa kila nyaja kisha watimukie kwa waarabu.
 

Ha ha ha mkuu nimefurahi sana
 
Nyerere aliacha - Muungano serikali moja nchi mbili, tumefiakaje kwenye muungano serikali mbili na nchi mbili? halafu sasa hata rasimu za katiba ziko mbili, moja ya maoni ya wananchi, nyingine maoni ya vyama. Kufika sijui?
 
BAVICHA NA NDOTO ZA ALINACHA.......
niliwaambia humu Kuwa serikali Tatu hazitakuwepo hata msujudu uchi.
Hii nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya KI-MBWA
Siyo kila anayepingana na CCM ni BAVICHA.
 
Ni wakati wa kuwa na Tanganyika yetu ndo tuungane nao. Huu unafiki wa serikali mbili ni dhambi kubwa ya taifa!

Mkuu, hii thread ni ya miaka kibao nyuma!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Mkuu tunaomba utaje hizo faida nyingi angalau kwa uchache tu.
 

wakimbizi hawatajuwa wengi ksma sukosei sensa iliyopita zanibaru hajafika hat milioni 3 na kea muonekano a sa sa nafikiri nusu yao wako ilala magomeni na temeke
 
Naomba kuelewa hasara ni nani muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar ukivunijka ?

Je kuna maslahi yoyote ya kuwa katika muungano huu.
 
Wanasiasa wengi wamekuwa wakisifia sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kwamba wale wote wanaokosoa muungano ni watu wasiotakia mema nchi.lakini nimekuwa nashangazwa na haohao linapokuja suala la muungano wa E.africa.watakuja na hoja zilezile zinazotumiwa na wazenji dhidi ya Tanganyika mara ooh hatutaki wachukue ardhi mara vile.SASA NAJIULIZA KAMA MUUNGANO NI KITU KIZURI MBONA SISI TUNAOKWAMISHA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI.NA KAMA NI KITU KIBAYA KWANINI TUNAING'ANG'ANIA ZANZIBAR.nawasilisha.
 

Amini nakuambia Zanzibar ikijitenga mwaka hauishi watakuja kuomba hifadhi Tanganyika maana mapinduzi yapo nje nje kama kule Sudani. Kama unabisha weka jiwe mimi nakuahidi laki moja.
 

Mkuu acha kumung'unya maneno taja hizo faida za muungano ili wananchi wazielewe kusema ziko nyingi haitoshi:focus:
 
BAVICHA NA NDOTO ZA ALINACHA.......
niliwaambia humu Kuwa serikali Tatu hazitakuwepo hata msujudu uchi.
Hii nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya KI-MBWA

Inaonyesha jinsi ulivyo na upeo mdogo wa kufikiri jenga hoja za kutetea msimamo wako sio kutukana eleewa wenye
msimamo tofauti na wako wana haki ya kutoa mawazo yao sio kuwa wewe na kundi lako ndio mna mawazo mazuri
kushinda wengine matusi ni dalili ya kutokomaa kifkra na kukosa hoja za msingi:thinking:
 
Watu wengi, hasa hawa wa kizazi cha dijitali, wamekuwa wakijiuliza kuhusu faida za muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Muungano una faida nyingi za kiuchumi na kimaendeleo.

Zifuatazo ni baadhi tu ya faida za muungano:

1. Wazanzibar (wapemba) wengi wamepata fursa za kiuchumi nchini Tanganyika. Idadi kubwa ya wapemba wanamiliki ardhi, nyumba, na biashara kubwa nchini Tanganyika, jambo ambalo lisingewezekana nje ya muungano.

2. Kuoleana: Wananchi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakioleana tangu kale na wameendelea kufanya hivyo hata baada ya muungano.

3. Muungano ni wa kihistoria. Kuulinda ni sawa na kudumisha historia. Nyerere na Karume hawakuwa machizi walipoamua kuunganisha nchi hizi.

4. Visiwa vya Zanzibar ni vidogo na havitanuki. Kuungana kumewezesha baadhi ya wazanzibar kuhamia bara na kupunguza msongamano visiwani.

5. Kihistoria, wakazh wa Zanzibar walitokea Tanganyika. Muungano umewaunganisha na ndugu zao wa asili.

6. Bila muungano, waarabu watahamia Zanzibar na kuishambulia Tanganyika.
 
Hizo zote umetoa hoja dhaifu sana,pili umeonyesha faida ziko kwa wazanzibari,je watanganyika wanafaidika nini na muungano?

Kwa akili yako chochote alichokisema au kukifanya Nyerere hakitakiwi kuhojiwa?au ni kosa kukihoji.

Unaleta hoja ya kuoleana?hata watanzania wanaoishi mipakani wameoana sana na wenzao wa upande wa pili,je tuungane nao pia?

Hoja namba 6 ni hoja dhaifu kuliko zote,kwa hiyo tunaungana kwa kuhofia waarabu?
 
Unatoa hoja kama jk? Ina maana tukioa mwingereza ndo tuungane nao, hoja dhaifu kama mwenyekiti wa ccm taifa
 

Faida kuu kuliko zote ni usalama wa nchi yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…