Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ni mtanzania wa hali ya kawaida sana . Ninakerwa na Viongozi wanao ogopa Kumfunga paka Kengele. Kikwete kasema Muungano yeye hauvunji labda atoke madarakani ndiyo watu waje kuuvunja. Inaonyesha CCM wanaogopa kubeba hiyo Dhambi ambayo kwenye Biblia wala Quran haipo. SASA MIMI NAJITOLEA KUBEBA HIYO LAWAMA KWA HISTORI YA VIZAZI VYOTE VITAKAVYOKUJA MBELE YETU. Nipeni Urais wa Mkataba wa Mwaka Mmmoja nifanye yafuatayo.
1. Siku ya pili baada ya kuapishwa Nitatangaza Nchi ya Tanganyika; hivyo nitatoa Mwezi MMOJA Wazanzibar wote popote pale walipo huku Tanganyika warudi kwao. Watakao taka kurudi Bara Wafuate taratibu za Uhamiaji.
2. Wanajeshi wote Kutoka Tanzania Bara watarudishwa Tanganyika. Hii ikiwa na kubeba Silaha zote zilizokuwa huko Visiwani.
3.Nitaimarisha ulinzi Mkali kwenye Mwambao wote wa Bahari ya Hindi Kuanzia Tanga hadi Mtwara.
4. Watanganyika Nitawapa Mwezi MMOJA waamue Jina la nchi yao. Je libaki kuwa TANZANIA au lirudi TANGANYIKA.
5.Vyama vya siasa Vitaamua vyenyewe kubadirisha majina au Kutumia hayohayo ya Mwanzo.
6. Mwisho Nitaitisha Uchaguzi mkuu Muwachague viongozi wenu mtakao wataka Wanchi yetu TANGANYIKA ambao hawatakuwa wamebeba hii lawama.
Asanteni sana. SITANII NIKO SERIOUS.
Nyerere aliacha - Muungano serikali moja nchi mbili, tumefiakaje kwenye muungano serikali mbili na nchi mbili? halafu sasa hata rasimu za katiba ziko mbili, moja ya maoni ya wananchi, nyingine maoni ya vyama. Kufika sijui?Wakati wa Chama kushika hatamu ulipita zamaaani! Sasa hivi Watanzania wameelimika na wanajua nini ni nini mambo ya kupeana miongozo hayapo tena. Suala la Katiba ni la watu binafsi na siyo la kivyama. Kila mtu atatoa mawazo yake binafsi. Kama lingekuwa la vyama basi wangekusanya vyama vya siasa na kwenda kupata maoni.
Siyo kila anayepingana na CCM ni BAVICHA.BAVICHA NA NDOTO ZA ALINACHA.......
niliwaambia humu Kuwa serikali Tatu hazitakuwepo hata msujudu uchi.
Hii nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya KI-MBWA
Ni wakati wa kuwa na Tanganyika yetu ndo tuungane nao. Huu unafiki wa serikali mbili ni dhambi kubwa ya taifa!
Mkuu tunaomba utaje hizo faida nyingi angalau kwa uchache tu.faida za muungano zipo nyingi sana kuliko hasara.siku zote umoja ni nguvu. Lakini hatuwezi kuona faida kubwa za muungano hadi kwa bahati mbaya tutengane, wajerumani ukiwauliza leo watakwambia faida nyingi sana za muungano .sikatai kuna baadhi ya viongozi wetu hawasimamii ipasavyo mambo ya muungano na baadhi ya vipengele vya muungano vyahitaji kurekebishwa.haya ni mawazo yangu binafsi.
Kama ni Mzanzibar nakupongeza kwakuwa unaakili sana ila kama unatoka bara nakuonea huruma kwa ujinga wako.Siyo kila anayepingana na CCM ni BAVICHA.
Kama ni Mzanzibar nakupongeza kwakuwa unaakili sana ila kama unatoka bara nakuonea huruma kwa ujinga wako.
Mkuu ngongo .. heshima mbele.... hili bandiko limeshiba ukweli na uhalisia ....asante sana .... umenichosha ama kunifurahisha hapo kwenye red .... utanitendea haki pamoja na wengine wanaofuatilia mada hii ukitoa angalau ufafanuzi kidogo tu kuhusu sentensi hii
Ccm Ina hasara
Wanasiasa wengi wamekuwa wakisifia sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kwamba wale wote wanaokosoa muungano ni watu wasiotakia mema nchi.lakini nimekuwa nashangazwa na haohao linapokuja suala la muungano wa E.africa.watakuja na hoja zilezile zinazotumiwa na wazenji dhidi ya Tanganyika mara ooh hatutaki wachukue ardhi mara vile.SASA NAJIULIZA KAMA MUUNGANO NI KITU KIZURI MBONA SISI TUNAOKWAMISHA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI.NA KAMA NI KITU KIBAYA KWANINI TUNAING'ANG'ANIA ZANZIBAR.nawasilisha.
faida za muungano zipo nyingi sana kuliko hasara.siku zote umoja ni nguvu. Lakini hatuwezi kuona faida kubwa za muungano hadi kwa bahati mbaya tutengane, wajerumani ukiwauliza leo watakwambia faida nyingi sana za muungano .sikatai kuna baadhi ya viongozi wetu hawasimamii ipasavyo mambo ya muungano na baadhi ya vipengele vya muungano vyahitaji kurekebishwa.haya ni mawazo yangu binafsi.
BAVICHA NA NDOTO ZA ALINACHA.......
niliwaambia humu Kuwa serikali Tatu hazitakuwepo hata msujudu uchi.
Hii nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya KI-MBWA
Hizo zote umetoa hoja dhaifu sana,pili umeonyesha faida ziko kwa wazanzibari,je watanganyika wanafaidika nini na muungano?
Kwa akili yako chochote alichokisema au kukifanya Nyerere hakitakiwi kuhojiwa?au ni kosa kukihoji.
Unaleta hoja ya kuoleana?hata watanzania wanaoishi mipakani wameoana sana na wenzao wa upande wa pili,je tuungane nao pia?
Hoja namba 6 ni hoja dhaifu kuliko zote,kwa hiyo tunaungana kwa kuhofia waarabu?