Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

pole sana...kwanza jifunze historia ya Tanganyika na Zanzibar, baadae jifunze historia ya Tanzania. Mambo haya hayataki ushabiki, usiwe mtu wa kufuata mkumbo kirahisi.

Mi naona kama we ndo ujifunze realistic! Kwa hili la bodi ya mikopo zenj mnajichanganya, heslb inatoa mikopo kwa vyuo vyote vikiwemo ZU,SUZA,Chukwani na sidhani kama una proven evidence kuwa zenj inabaguliwa ktk hili. Ndo dizzle akasema hii inprove low thinkin capacity mlonayo. Hebu simamieni hiyo free port bubu yenu kwanza,badala ya kuja na pumba za namna hii!
 
zanzibar ikijitenga,wakazi wa mbagala,gongolamboto,kibaha,moro,arusha musoma n.k. Wataathirika vipi?
Muungano unamsaidia nini mzee masikini aliyeko rukwa?
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

Ukisikia vichekesho vya mahoka ndo hivi!!! Toka lini sisimizi akawa mlinzi wa tembo??? Acha dharau mkubwa!!! Pamoja na kuwa Tanganyika inaweza ikawa sleeping giant lakini si kwa kiasi cha kulindiwa usalama na Zenji!!! By the way I fail to understand how Dubai is a threat to our lovely Tanganyika!!!!....
 
WaTanganyika msijifanye wababe mbele ya sheria. Mna haki kabisa pale Bungeni kudai Serikali yenu ya Tanganyika iliyokufa kibudu.

Kama kwli mna nia basi anzisheni hoja binafsi ya kudai Tanganyika.
 
WaTanganyika msijifanye wababe mbele ya sheria. Mna haki kabisa pale Bungeni kudai Serikali yenu ya Tanganyika iliyokufa kibudu.

Kama kwli mna nia basi anzisheni hoja binafsi ya kudai Tanganyika.

vunja muungano ... kila mtu arudi kwao akachunge n`gombe au unaonaje
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

acha ukilaza wewe... sikuhizi dunia iko modern and advanced ..... mambo eti ya usalama.....hiyo ni zamani.... siku hizi ukileta fyoko fyoko unachapwa na wababe tena wakiwa huko huko makwao .... siku hizi kambi za majeshi zimemehamia kwenye maji ..... hakuna tena yale mavita ya kizamani ya infantry .... kuna ballistic missile ambazo zinaitwa precision guided missiles zinakuwa guided na GPS ...angalia libya kinachotokea..... wacha uendelee kushangaa shamgaa na hako kakisiwa tu .... ikija tsunami kitazama chooote
 
Inavyoonesha wewe mgeni na ZNZ. Wala huijui ZNZ. Mshamba tu wewe. Bora unyamaze na vipicha vyako vibovu.
mimi zanzibar naifahamu vyema-hembu naomba upload picha yoyote iliopigwa zanzibar ambayo utakuwa umerizika nayo ili uthibitishe huo-u-paradise wao-mimi sijaona picha yoyote nzur zaid ya hio nilio upload
 
@Straatkasyambe,

Mkuu.

Umeandika mengi. Mengine yanafikirisha na mengine yanachekesha.
Kama unavyosema dunia inabadilika kama Zanzibar ilikuwa tishio hapo zamani sioni huo ukomunisti na uislamu wa kuogopesha ulioko Zanzibar leo.

Naamini cha kuhofu zaidi ni ushamiri wa religious fundamentalism huku Tanganyika.
Udini utaitafuna sana Tanganyika. Sijui kama unaelewa uchaguzi uliopita kuna kampeni za wazi wazi za kidini zilifanyika kulingana na dini za wagombea.

Hata taasisi za dini zilikuwa zinatoa matamko na maelekezo kwa waumini wao juu ya uchaguzi mkuu.

Kwa maelezo uliyoandika katika mchango wako ume-assume kuwa Tanganyika ni Catholic country, au at large Christian country.Mkuu sijui ulikuwa unajaribu kuipa nguvu hoja yako ya Tanganyika kuimeza Zanzibar ukasahau kuwa Tanzania ina waislamu na wakristo kwa idadi, more or less, inayolingana.... Unaweza kuuliza nimetoa wapi takwimu hii ? Ukirudi katika takwimu za mwisho ambazo zilionesha uhusiano ya watu na dini zao basi waislamu walikuwa ndio segment iliyokuwa kubwa na baadae Mwalimu alifuta kipengele cha uainisho wa dini ya mtu katika sensa za nchi.

Viongozi wakristo na waislamu wameshaongoza serikali ya muungano sasa hii assumption yako ina walakini kidogo.

Ama kusema Zanzibar kuna muslim fundamentalism, katika kila jamii wako watu wa msimamo mkali mkuu, lakini wao sio majority. Unataka kusema kuwa hapa Tanganyika hakuna waumini wa msimamo mkali, waislamu na wakristo ?

Njia ya ku-defeat extremism ni kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao, maisha mazuri na uhuru wa kusema usiwekewe vipingamizi. Jambo ambalo serikali kwa miaka 50 imeshindwa kufanya.

Majority ya wananchi Tanganyika na Zanzibar ni wapiga mbio kutafuta cha kushibisha tumbo na kutafuta karo ya shule kwa watoto wao. Ijumaa wanakwenda misikitini na jumapili wanakwenda makanisani.

Kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wanasiasa ndio wanapandikiza hizi hisia za udini kwa jamii. Kama hawataacha kueneza sumu hii basi si Zanzibar itakayokuwa sababu ya kuripuka kwa Tanganyika.

La msingi, muda umefika kwa serikali ya Muungano na CCM kuacha usanii, ubabe na ubabaishaji bali ilete reforms za maana kuiepusha nchi kufikia kama Ivory Coast au yaliyotokea Kenya...Ni vyema kusimamia kupatikana kwa hii katiba mpya na hivyo kunegotiate upya Muungano pia, Tume huru za uchaguzi na investments kwenye miundo mbinu ya jamii na huduma za jamii.

Nionavyo mimi hata huu muungano umetumiwa na wajanja wa CCM kutowajibika katika kuwaletea maendeleo wananchi katika Tanganyika na Zaznibar. Na wananchi badala ya kujua adui wao wa kweli wameingia katika malumbano, kejeli na chuki baina ya Tanzania bara(Tanganyika) na Zanzibar.

Hapa chini kuna mchangiaji ametanabahi adui ni nani.


kweli kama watafikia hatua ya kupewa pesa kutoka HESLB nipo radhi kwa muasi-mbaona zanzibar wanatusumbua hivi?napata hasira sana nikisikia madudu ya zanzibar-kwa nini hawa viongozi wetu hawataki kuvunja huu muungano?wananiboa sana
 
[quote="Nonda,

Nashukuru kwa mchango wako ila naona hukunielewa kidogo bwana Nonda, sijasema Tanganyika inaongozwa na kanisa katoliki na wala sina maana kuwa waislam ni wachache ndani ya Tanganyika, wanaweza wakawa wengi zaidi ya wakristo au ndani ya Tanganyika ila kwa idadi ndogo.

Tofauti ya Zanzibar na Tanganyika ni kwamba Zanzibar hakuna nguvu yoyote wa Wakristo, waislam ndio wenye nguvu lakini bara hata kama wakristo ni wachache kwa idadi ndogo kama mnavyosema lakini si siri kuwa wakristo wa bara wana nguvu kwa sababu ya mfumo wa elimu wa magharibi unaotawala sasa na ndio ambao wakristo wengi unaowapa nguvu.

Kuhusu kuwa Tanganyika pia imewahi tawaliwa na Waislam ukitoa mfano wa Mwinyi, na Kikwete kwa sasa, kwa fundamentalist kwao hao sio waislam ndugu yangu. Nchi za magharibi ndio zinawapandikiza watu wenye msimamo wa kati kama hawa sehemu mbalimbali dunia, nafikiri unajua ni mara ngapi former president wa Egyty alikoswa kuawawa.

Hawa marais wanapandikizwa tu na ndio kitu kinachofanyika middle-East na katika hizo vita zinaendeshwa na Marekani na washirika wake. Nia ni kuweka watu wenye mlengo wa kati kama hao akina Mwinyi ili watawale Kirahisi. Ndio maana nikasema huu muungano una nguvu ya nje zaidi kuliko ya ndani na ndio maana nimeandika kwa kuwa mfumo wa Kimagharibi ndio unatawala kwa sasa ambao kuutenganisha na ukristo ni vigumu kwa hiyo ni rahisi kuitumia Tanganyika kutawala Zanzibar kwakuwa nguvu ya Ukristo ni kubwa Tanganyika kuliko huko Zanzibar.

Kwa mfumo uliopo Christian fundamentalist wala si threat kwa nchi za Magharibi and they are promoted lakini muslim fundamenatist ni threat kwa magharibi na automatically they are termed as terrorist. Ni rahisi kwa Zanzibar kuwepo kwa muslim fundamentalist kama hakuna nchi ya kuwamonitor kwa karibu kama Tanganyika na kwa hali ya uislam wa Tanganyika fundamentalist wa kiislam ni ngumu sana kuimalika. Na kwa msingi huo ndio maana Zanzibar inaogopwa kuwa huru kwa wakati huu.

Muslim fundamentalist sio kwamba wanaogopwa na Tanganyika bali ni theat kwa nchi za Magharibi kama walivyolipuwa balozi za Marekani za DSM na NRB. Kwa hiyo Zanzibar ikifikia kuwa na fundamentalist ni hatari kwa mambo mengi na zaidi kwa Nchi za magharibi na Ukristo (Jaribu kuangalia zile video za Blackwalter-Christian Fundamentalist and their role in Iraq and Afghanistan in You tube nimeshindwa kuziweka hapa kwa kuwa na ndefu)
 
hapo ndipo linapokuja kongamano la waislamu arusha. lengo likiwa kuukomesha mfumo kristo. it will take time but it will be done
 
@Straatkasyambe,

Mkuu.
Unajitahidi kunishawishi lakini napata tabu kukubaliana na wewe na hoja hii ya kuwa Muungano upo kwa ajili ya ku-monitor U-muslim fundamentalism wa Waislamu wa Zanzibar.
Itakuwa vyema ukaandaa mada ambayo itawaamsha wananchi wa Tanganyika kuwa huu muungano hauna faida nasi. Ni muungano kwa maslahi ya West. Lakini katika kufanya hivyo uwe na tahadhari kubwa ya kutoelezea kuwa wakristo wa Tanganyika wanatumika kuwadhibiti waislamu wa Zanzibar..kwani implification yake itakuwa pia kuwa nguvu ya ukristo inatumika Tanganyika pia kuwakandamiza waislamu wa Tanganyika.

Wengi wa wachangiaji hulipinga hili inapoibuka mijadala ya waislamu na munung'uniko yao na matakwa yao. Hoja zinazotolewa huko ni kama hii inayoisema hapa kuwa Tanganyika,Tanzania inaongozwa kwa mfumo kristo kwa upande mmoja na wengine husema ni kwa sababu ya elimu madrasa na uvivu wa watu wa upande mwengine.

Kama wewe utalithibitisha hili kuwa ni kweli Tanzania inaongozwa na mfumo kristo basi unatengeneza mgogoro ambao mimi nafikiri ndio utakaoitafuna Tanganyika.Kwa vile ni wakati wa ukweli na uwazi hata hivyo itakuwa vyema ukiwaamsha wananchi ili kujua hilo na wasipoteze muda wao katika kutupiana maneno juu ya Muungano.

Ni wazi kwa sasa inaonekana wananchi watanganyika hawautaki muungano na pia wananchi wa Zanzibar hawautaki Muungano wa aina hii uliopo leo.Hauna tija kwao.Lakini wataelewa kuwa Muungano ni mradi wa West na kwa Wakristo kama kundi linalowezeshwa kuwa na nafasi maalum litaelewa nafasi yao katika kuulinda Muungano na nafasi hii maalum na kwa hiyo tutaacha kuupinga Muungano.

Lakini kwa ku-refresh hoja yako basi pitia hii link . halafu utuandikie mada hiyo ya Muungano ni mtaji wa West,,lakini kama Watanganyika na wazanzibar hatuuhitaji.

Revolutions: What went wrong in the west? - Opinion - Al Jazeera English

Mkuu.
By the way 911 na mabomu ya balozi za East africa. ni wao wenyewe wamarekani katika kutekeleza mikakati yao ya muda mrefu.
Pitia hizi series uone kama utashawishika. ziko 1-19.

 
Last edited by a moderator:
Mi naona kama we ndo ujifunze realistic! Kwa hili la bodi ya mikopo zenj mnajichanganya, heslb inatoa mikopo kwa vyuo vyote vikiwemo ZU,SUZA,Chukwani na sidhani kama una proven evidence kuwa zenj inabaguliwa ktk hili. Ndo dizzle akasema hii inprove low thinkin capacity mlonayo. Hebu simamieni hiyo free port bubu yenu kwanza,badala ya kuja na pumba za namna hii!
Hivyo ile sera ya kujitegemea ndio imekufa na mwenyewe Nyerere? Iwapo Wazanzibari wanaamua kujitegemea wewe hupendi? Mbona hamjuwi mnachotaka nyinyi? Mara ooh tunawabeba, mara mzigo na wanapoamuwa kukutueni mzigo mnapiga kelele. Kwani unataka iweje hasa kuhusu Zanzibar, iwe mzigo au ijitegemee?
 
Nathani nivizuri wajaribu nao waone kama wanaweza kubeba majukumu ayo, but nivizuri wajitegemee ata kifedha watafute njia mbada za kuingizia pato nchiyao ili wajitegemee.
 
@Straatkasyambe,

Nakupongeza kwa jitihada zako za kugeuza tatizo la Muungano wa Tanzania na nguvu za nje. Ni kweli kuwa hapo ulipoanzishwa Muungano kulikuwa na nguvu za nje ili kuidhibiti Zanzibar lakini nguvu hizo hazikuwa kwenye suwala la dini? Wamarekani na Waingereza walikuwa na hatamu na utawala wa Kifalme wa Zanzibar kabla ya uhuru na baada ya uhuru uhusiano huo ukaelekezwa kwa Chama cha machotara wa Kiarabu kabla ya kupinduliwa. Mapiduzi ya Zanzibar hayakuwa na misingi ya dini na waliochukuwa madaraka walikuwa na sifa ya Ukoministi. Msimamo huu ndio uliofanya West kutaka Zanzibar idhibitiwe.

Historia ya Zanzibar baada ya Mapinduzi haikuwahi kuwa na sura ya Islamic fundamentalism hata mara moja. Zanzibar ni sehemu ambayo Waislamu na Wakristo hungeweza kuwatafautisha labda siku za Ibada. Muda wote wa Muungano wakati alipokuwepo Karume nchi mbili hizi ziliishi kama nchi mbili tofauti na West hawakuingilia hali hii. Wanamapinduzi Zanzibar walifanya walivyotaka na hakuna aliewaingilia. Mambo yalikuja kugeuka baada ya Nyerere kuunganisha vyama vya siasa na kuundwab CCM. Bado hakuna ushahidi wowote kuwa west waliingilia kati suwala la Muungano huu wa kutufanya tuseme kuwa Muungano huu unawekwa kwa kuzuia Islamic fundamentalism.

Kama kweli West wana mkono na Muungano huu sasa hivi basi wangekwishakuwa werevu wa kuibana Tanganyika kuwafanyia ya haki Wazanzibari ili wasiwe na fikira za kuuona Muungano huu unaweadhalilisha. Wazanzibari laiti wangeishi kama walivyokuwa wakiishi kwa kujitegemea basi kusingekuwa na malalamiko. Wakati wa Karume na kipindi cha miaka michache ya Jumbe Wazanzibari hawakuwa na malalamiko na Muungano kwani kwao Muungano wanaukuta pale wanapotaka kwenda nje ya Tanzania kwa kupewa pasi ya Tanzania.

Tusitafute sababu za kidini kuuelezea Muungano huu hao West hawashindwi kuweka viogozi wanaowapenda hata Zanzibar kwani si wanafanya hivyo nchi zinazotambulika kuwa za Kiislamu mbali ya Zanzibar yenye viongozi kama Salmini, Karume, Sheni na Sief. Haijawahi kutokea hata siku moja kuwepo kwa tishio la Islamic fundamentalism Zanzibar kwani wananchi wa Zanzibar hawajakua katika misingi ya udini mkali.

Tatizo letu Watanzania ni kuwa tunapenda sifa za kisiasa na huku tukiukataa ukweli. Tunataka sifa kuwa Taifa lililodumu na umoja wakati sisi wenyewe hatuuenzi umoja huo. Mbona matatizo ya Muungano ni madogo sana iwapo tunataka kuuendeleza? Tukubali kuwa kila sehemu iwe huru kijiamulia mambo yake kwa maendeleo na kwa bahati nchi ili iendelee lazima iwe na mahusiano na nchi nyengine. Tunapotowa nafasi ya nchi moja (tanganyika) kuwa huru kufanya inavyotaka na Zanzibar isiwe na kauli yoyote ya kuhoji wakati Zanzibar inapofanya jambo basi lazima ijieleze na kuomba ruhusa kwa Tanganyika hapo unakosekana Muungano na badala yake inakuwa protectorate.

Watanganyika huwa mnawashangaa viongozi wenu kwa kuungangania muungano kwa imani ile ile kuwa mnatumia nguvu zenu kuibeba Zanzibar lakini si kweli na ukweli ni kuwa kuushikilia Zanzibar hakuwathiri kimatumizi kwa vile hamtowi kitu kwa Zanzibar. Wazanzibari wachache wnaofanyakazi kwenye wizara za Muungano wapo kwa faida ya kuhakikisha sera za kuitawala Zanzibar zinafanikiwa na mnahakikisha kuwa Zanzibar inalipa matumizi ya kuweka caretakers hao. Iwapo zanzibar uchumi wake uko kwenye bandari na viwanja vya ndege na mnahakikisha kuwa mapato hayo yanaingia moja kwamoja kwenu hii nini maana yake.

Nashangaa na logic ya kuweka Wabunge kutoka Zanzibar kwenye bunge la Tanganyika lakini hii ni janja tu ya kufanya Wazanzibari eti wahisi kuwa Serikali ya Muungano si serikali ya Tanganyika. Ama kwa hili kila mtu inafaa ajiulize kwanini kusiwe na Bunge la Tanzania litakalozungumzia mambo ya Muungano tu? Kwani lengo la kukaa pamoja ni kujadili mambo ya Tanganyika na kwa uhalali gani Wabunge wa Zanzibar wafanye hivyo? Kwanini Wabunge wa Bara hawana uwezo huu?

Haya yote tuyaseme kuwa ni harakati za West kuzuia Islamic fundamentalism? Na kama ni hvyo kwanini basi Zanzibar inapewa kiduchu kwenye hiyo misaada ya West na hilo baada ya makelele mengi?
 
mimi zanzibar naifahamu vyema-hembu naomba upload picha yoyote iliopigwa zanzibar ambayo utakuwa umerizika nayo ili uthibitishe huo-u-paradise wao-mimi sijaona picha yoyote nzur zaid ya hio nilio upload

Kwani uzuri ni kitu gani? Pengine ustaarabu wa watu tu unaweza ukawa uzuri wa pahala.
 
Ukisikia vichekesho vya mahoka ndo hivi!!! Toka lini sisimizi akawa mlinzi wa tembo??? Acha dharau mkubwa!!! Pamoja na kuwa Tanganyika inaweza ikawa sleeping giant lakini si kwa kiasi cha kulindiwa usalama na Zenji!!! By the way I fail to understand how Dubai is a threat to our lovely Tanganyika!!!!....

Pengine sio Dubai kama nchi bali sifa zake. Ana maana yake hasa akikumbuka wakati wa Dr Salmini na harakati za Tanganyika kuzima juhudi zake.
 
Nathani nivizuri wajaribu nao waone kama wanaweza kubeba majukumu ayo, but nivizuri wajitegemee ata kifedha watafute njia mbada za kuingizia pato nchiyao ili wajitegemee.
Mkuu.
Siku ambayo tutawarejeshea uwezo wa kuingia mikataba na mataifa mengine.kwa maana nyengine siku tukiuvunja Muungano au kuweka mechanism ya wao moja kwa moja kuwa na uwezo na nguvu ya kushirikiana na nchi na mataifa mengingine kama Zanzibar sioni kwa nini watashindwa kufanya mambo yao vile wanapenda kufanya.
Kuvunja Muungano, ita-restore sovereignty yao fully na hiki ndio kitu wanachokikosa kwa sasa.

Unapomziba mtu pua na mdomo pia kumkaba koo halafu umwambie haya pumua, vuta pumzi kwa raha, unakuwa unamkejeli.
Lakini pale panapokuwa hakuna kizuizi kama havuti pumzi ni wazi kuwa atakabiliana na mauti mwenyewe na hatakuwa na wa kumlaumu.
 
Mi naona kama we ndo ujifunze realistic! Kwa hili la bodi ya mikopo zenj mnajichanganya, heslb inatoa mikopo kwa vyuo vyote vikiwemo ZU,SUZA,Chukwani na sidhani kama una proven evidence kuwa zenj inabaguliwa ktk hili. Ndo dizzle akasema hii inprove low thinkin capacity mlonayo. Hebu simamieni hiyo free port bubu yenu kwanza,badala ya kuja na pumba za namna hii!
Angalau Zanzibar wanaanza kujipanga na kudai haki zao iwe CCM iwe CUF... watu milioni 40+ watanganyika bado wamelala . Kazi kujisifu eti sisi tuna hiki , maadini , blah blah . Tanganyika itaendelea kuwa maskini kwa watu kama nyinyi. Hivi huoni aibu Tanzania kuwa miongoni mwa nchi masikini sana duniani? Umefika Mtwara?
 
Back
Top Bottom