@Straatkasyambe,
Mkuu.
Unajitahidi kunishawishi lakini napata tabu kukubaliana na wewe na hoja hii ya kuwa Muungano upo kwa ajili ya ku-monitor U-muslim fundamentalism wa Waislamu wa Zanzibar.
Itakuwa vyema ukaandaa mada ambayo itawaamsha wananchi wa Tanganyika kuwa huu muungano hauna faida nasi. Ni muungano kwa maslahi ya West. Lakini katika kufanya hivyo uwe na tahadhari kubwa ya kutoelezea kuwa wakristo wa Tanganyika wanatumika kuwadhibiti waislamu wa Zanzibar..kwani implification yake itakuwa pia kuwa nguvu ya ukristo inatumika Tanganyika pia kuwakandamiza waislamu wa Tanganyika.
Wengi wa wachangiaji hulipinga hili inapoibuka mijadala ya waislamu na munung'uniko yao na matakwa yao. Hoja zinazotolewa huko ni kama hii inayoisema hapa kuwa Tanganyika,Tanzania inaongozwa kwa mfumo kristo kwa upande mmoja na wengine husema ni kwa sababu ya elimu madrasa na uvivu wa watu wa upande mwengine.
Kama wewe utalithibitisha hili kuwa ni kweli Tanzania inaongozwa na mfumo kristo basi unatengeneza mgogoro ambao mimi nafikiri ndio utakaoitafuna Tanganyika.Kwa vile ni wakati wa ukweli na uwazi hata hivyo itakuwa vyema ukiwaamsha wananchi ili kujua hilo na wasipoteze muda wao katika kutupiana maneno juu ya Muungano.
Ni wazi kwa sasa inaonekana wananchi watanganyika hawautaki muungano na pia wananchi wa Zanzibar hawautaki Muungano wa aina hii uliopo leo.Hauna tija kwao.Lakini wataelewa kuwa Muungano ni mradi wa West na kwa Wakristo kama kundi linalowezeshwa kuwa na nafasi maalum litaelewa nafasi yao katika kuulinda Muungano na nafasi hii maalum na kwa hiyo tutaacha kuupinga Muungano.
Lakini kwa ku-refresh hoja yako basi pitia hii link . halafu utuandikie mada hiyo ya Muungano ni mtaji wa West,,lakini kama Watanganyika na wazanzibar hatuuhitaji.
Revolutions: What went wrong in the west? - Opinion - Al Jazeera English
Mkuu.
By the way 911 na mabomu ya balozi za East africa. ni wao wenyewe wamarekani katika kutekeleza mikakati yao ya muda mrefu.
Pitia hizi series uone kama utashawishika. ziko 1-19.