Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

3 Comments

mwada-wachanwa-564x272.jpg
Ahmed Rajab
Aprili 13, 2011TENGE na tahanani iliyozuka majuzi Zanzibar wakati wa mijadala ya katiba ya Tanzania lazima iliwafanya wengi wasiozielewa hisia za Wazanzibari kuhusu Muungano waghumiwe.

Samuel Sitta, waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, aliingia kizaazaa alipozomewa alipokuwa akiizungumzia rasimu ya muswada wa sheria ya kuanzisha Tume ya Mapitio ya Katiba ya Tanzania na kuiona hiyo rasimu ikichanwa.
Vishindo hivyo visistaajabishe. Jazba na hamasa zilizopandishwa na Wazanzibari waliokwenda kumsikiliza Sitta hazikuwa za bure.

Wala hazikuwa za Wazanzibari wa mwelekeo fulani tu wa kisiasa. Zilikuwa hisia za Wazanzibari wote wana CCM na wana CUF pamoja na wale wasio wafuasi wa chama cho chote cha kisiasa. Hii ni hali inayowashangaza wengi Bara wasiofahamu jinsi Muungano unavyowachoma Wazanzibari.

Wazanzibari hawakuviona hivyo vishindo vya katiba kuwa ni vigeni au kuwa viroja. Na ukiwauliza watakwambia kwamba wana historia ndefu ya michakato ya utungaji wa katiba.

Watakutajia Lancaster House, lile jengo maarufu jijini London, ambako kulifanywa mkutano wa mwanzo wa kuizingatia katiba ya Zanzibar mwaka 1962.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (Hizbu), Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) na Afro-Shirazi Party (ASP).

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria walikuwa ni baadhi ya viongozi wa kihistoria wa Zanzibar. Nao ni Sheikh Ali Muhsin, Sheikh Muhammed Shamte, Sheikh Abeid Amani Karume na Sheikh Othman Shariff.
Walihudhuria pia Abdallah Kassim Hanga, Hassan Nassor Moyo, Abdulrahman Babu na Salim Said Rashid, ingawa hawa wanne hawakushiriki kwenye mashauriano.

Ukiwachokorachokora tena Wazanzibari watakwambia kwamba katiba yao ya kwanza ilikuwa ile Katiba ya Uhuru ya mwaka 1963.

Baada ya Mapinduzi Januari 12 mwaka 1964, Baraza la Mapinduzi lilipitisha ile iitwayo Kanuni ya Serikali ya Kikatiba na Utawala wa Kisheria mnamo Februari 25 mwaka 1964.

Kanuni hiyo iliagiza Baraza la Kikatiba la Watu wa Zanzibar liliitishwe kabla ya Januari 11 mwaka 1965 ili kufanya maamuzi kuhusu katiba mpya ya Zanzibar.

Kwa bahati mbaya agizo hilo halikutimizwa kwa sababu muda si mrefu pakaundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hakika, Muungano huo uliundwa bila ya Hati za Muungano kuidhinishwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kama ilivyotakiwa iwe kwa mujibu wa hizo Hati za Muungano na kama inavyohitajika kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria za Kimataifa na Utaratibu wa Mikataba.

Taksiri hiyo inaonekana wazi kwa vile ilani inayosema kwamba Baraza la Mapinduzi lilikutana na kuziidhinisha hizo Hati za Muungano ilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali ya Tanganyika, the Tanganyika Gazette, na kutiwa saini na P.R. Ninnes Fifoot kwa vile alikuwa na wadhifa wa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanganyika.
Ajabu ya mambo ni kwamba ilani hiyo haikuchapishwa katika gazeti rasmi la Serikali ya Zanzibar, the Zanzibar Gazette, na wala haikutiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, ambaye wakati huo alikuwa Salim Said Rashid.

Kweli kulikuwa na Katiba ya Muda ya Muungano iliyotayarishwa kwa kuibadili kidogo Katiba ya Tanganyika na kuzifanya sheria husika za katiba hiyo ziwe zinatumika pia Zanzibar.

Hiyo lakini ilikuwa ni hatua ya muda na palikuwa na utaratibu uliowekwa wazi kwenye Hati za Muungano wa kuifikia katiba ya kudumu ambayo ilikuwa itungwe katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuundwa Muungano.

Kufikia Machi 24 mwaka 1965 Bunge la Muungano lilipitisha Hati ya Sheria ya Katiba yenye haki na uwezo wa kutunga au kubadilisha katiba. Hati hiyo ilivibadili vifungu vya Hati za Muungano na kukirefusha kipindi cha Katiba ya Muda ya Muungano mpaka utapofika wakati muwafaka.

Yote hayo yalitendeka licha ya kuwa Bunge la Muungano lenyewe halina mamlaka yo yote ya kisheria ya kuzibadili Hati na Sheria za Muungano bila ya mageuzi hayo pia kuridhiwa na baraza la utungaji sheria huko Zanzibar.
Mtindo huu ulifurutu ada na ulirejelewa mara kadha wa kadha kwa minajili ya kufanya mageuzi ya kisheria au kuongeza mambo katika ile orodha ya mambo yanayopaswa kuwa ya Muungano.

Mwalimu Julius Nyerere alibabaishababaisha kwa kusema kwamba: Mamlaka ni ridhaa ya watu. Si kipande tu cha karatasi.

Kama mamlaka ni ridhaa ya watu basi mamlaka ya Muungano si ya halali kwani watu wa Zanzibar hawakushauriwa iwapo walitaka, walihitaji au walipendelea kuendelea kuwa katika Muungano. Wala baraza lenye kutunga sheria za Zanzibar halikushauriwa kama inavyopaswa.

Mwaka 1977 Nyerere aliiteua kamati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iupige mhuri na kuubariki muungano wa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na ASP. Halafu kamati hiyo ikakabidhiwa jukumu la kuandaa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yalitendeka miaka 13 baada ya kuundwa Muungano licha ya kuwa kwa mujibu wa Hati za Muungano Baraza la Kutunga Katiba lilikuwa likutane kufikia Aprili mwaka 1965 kutunga muswada wa Katiba ya Muungano.

Si hayo tu bali baraza hilo lilikuwa liwe na idadi sawa ya wajumbe wa Tanganyika na wa Zanzibar.

Mwaka 1979 Sheikh Aboud Jumbe, akiwa Rais wa Zanzibar, aliitoa ukumbini Katiba mpya ya Zanzibar miaka kumi na tano baada ya Mapinduzi ijapokuwa, kama tulivyokwishasema, Baraza la Mapinduzi liliamua Februari 1964 kwamba Zanzibar itakuwa na katiba mpya kufikia Januari 11 mwaka 1965.
Katiba hiyo ya mwaka 1979 ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1984.

Tukiiangaza basi historia ya Zanzibar kwa upande wa katiba na utungaji katiba tunaona kwamba Wazanzibari si wageni wa mchakato wa utungaji katiba.

Wazanzibari wanatambua vyema athari za badiliko lo lote katika Katiba ya Muungano kwa vile marekebisho yaliyokwishafanywa kuhusu masuala ya Muungano yaliongezwa kiubabe na Bunge la Tanzania, bunge ambalo halina mamlaka au uwezo wa kisheria wa kufanya hivyo.

Akhasi ya mambo ni kwamba mageuzi hayo yaliifanya Zanzibar ipungukiwe na nguvu zake. Wengine wanahoji kwamba hali hiyo ndiyo iliyopelekea uchumi wa Zanzibar uzorote kwa muda wote huu wa karibu nusu karne.

Tukumbuke kwamba pamekuwako tume mbili zikiongozwa na Majaji Francis Nyalali na Robert Kisanga zilizoundwa na Serikali ya Muungano kuutalii mfumo wa Muungano na Katiba ya Muungano.

Mapendekezo makuu ya tume zote hizo mbili yalikataliwa na Marais wa Muungano. Hii rasimu ya sasa ya Muswada wa Sheria wa Mapitio ya katiba ya Muungano inatoa fursa ya tatu ya kuendelea na mchakato huo, kwa nia ya kutaka kuyajuwa maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo yatayopelekea kufanywa mageuzi.

Muda uliowekwa wa mchakato huo ni miaka mitano. Hayo yana maana kwamba kwa muda wa miaka mitano zaidi hali ya mambo itaselelea kuwa vivi hivi ilivyo na Zanzibar itaendelea kugubikwa na ufukara pamoja na uadimikaji wa neema za kiuchumi na kijamii.

Hivyo ni muhimu pachukuliwe hatua za dharura za kuiwezesha Zanzibar kisheria kuwa na mfumo wake wenyewe wa sera za kiuchumi na kijamii zitazoweza kuikwamua nchi hiyo.

Kwa vile huu muswada wa sasa umekataliwa na wananchi wa Zanzibar, wakiwemo miongoni mwao mawaziri kutoka vyama tofauti vya kisiasa, kuna umuhimu wa zoezi hili kuanzishwa upya.

Tena liwe katika mfumo wa mashauriano kati ya serikali mbili, yaani Serikali ya Umoja wa Taifa ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Serikali hizo mbili ziwe wabia wenye haki sawa, yaani ziwe zinashauriana zikiwa washirika sawa katika Muungano, si upande mmoja kujifanya kaka na kuuona upande mwengine kuwa mdogo au usiostahiki haki sawa.

Hii leo ikiwa patafanywa kura ya maoni na Wazanzibari wataulizwa iwapo wanautaka Muungano uliopo na wajibu ama ndio au la sina shaka yo yote kwamba wengi wao wataukataa.

Hawatoukataa kwa sababu wanaamini ya kuwa kuna mapungufu katika mfumo wake. Wataukataa kimsingi kwani wanaamini ni Muungano ulioifanya hadhi ya Zanzibar ishuke kutoka kuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa ukubwa wa Jumla ya Pato la Kitaifa (GDP) na kutumbukia chubi katika shimo la ufukara na kuwa moja kati ya nchi zilizo na umasikini wa kutisha barani humo.

Kwa ufupi, wanaukataa Muungano kwa sababu wanaamini kwa dhati ya nafsi zao kwamba umewakandamiza.
Kila wakipiga bongo wengi wa Wazanzibari wanaona kwamba mustakbali wa nchi yao utakuwa mzuri endapo tu patakuwako mfumo mpya wa mahusiano baina ya Zanzibar na ile nchi iliyokuwa ikiitwa Tanganyika.

Si hayo tu bali wanataka Zanzibar iwe na mahusiano hayo ikiwa ni mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Ili uweze kuhakikisha kwamba Zanzibar badala ya kuwa nchi yenye uhuru nusu inakuwa na uhuru kamili, mfumo huo mpya hautokuwa na budi ila kuirejeshea Zanzibar mamlaka yake yaliyoporwa kwa ghiliba na Tanganyika.

*Raia Mwema
 
Mwiba,
ikiwa muungano utavunjika watakao pata tabu ni watanzania.elewa kuwa palipo watanganyika na wazanzibar pana watanzania pia.sasa ikitokea dhahama hiyo jamaa hawatakuwa na pakwenda.hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Nje ya wazanzibari na watanganyika, ni watanzania gani hao unaowazungumzia?
 
Unapo zuia mzanzibari kujadili muungano ktk mchakato wa kuandaa katiba ya Tz, nikumnyima haki kwake kiunganishi ni muungano, muungano usijadiliwe kama katiba inayoandikwa ni ya tanganyika tu au zanzibar peke yake!
 
Zanzibar imevinjari yadai talaka...

lC.gif
Ahmed Rajab
Aprili 13, 2011
rC.jpg

TENGE na tahanani iliyozuka majuzi Zanzibar wakati wa mijadala ya katiba ya Tanzania lazima iliwafanya wengi wasiozielewa hisia za Wazanzibari kuhusu Muungano waghumiwe.

Samuel Sitta, waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, aliingia kizaazaa alipozomewa alipokuwa akiizungumzia rasimu ya muswada wa sheria ya kuanzisha Tume ya Mapitio ya Katiba ya Tanzania na kuiona hiyo rasimu ikichanwa.
Vishindo hivyo visistaajabishe. Jazba na hamasa zilizopandishwa na Wazanzibari waliokwenda kumsikiliza Sitta hazikuwa za bure.

Wala hazikuwa za Wazanzibari wa mwelekeo fulani tu wa kisiasa. Zilikuwa hisia za Wazanzibari wote — wana CCM na wana CUF pamoja na wale wasio wafuasi wa chama cho chote cha kisiasa. Hii ni hali inayowashangaza wengi Bara wasiofahamu jinsi Muungano unavyowachoma Wazanzibari.
Wazanzibari hawakuviona hivyo vishindo vya katiba kuwa ni vigeni au kuwa viroja. Na ukiwauliza watakwambia kwamba wana historia ndefu ya michakato ya utungaji wa katiba.

Watakutajia Lancaster House, lile jengo maarufu jijini London, ambako kulifanywa mkutano wa mwanzo wa kuizingatia katiba ya Zanzibar mwaka 1962.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (Hizbu), Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP) na Afro-Shirazi Party (ASP).
Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria walikuwa ni baadhi ya viongozi wa kihistoria wa Zanzibar. Nao ni Sheikh Ali Muhsin, Sheikh Muhammed Shamte, Sheikh Abeid Amani Karume na Sheikh Othman Shariff.

Walihudhuria pia Abdallah Kassim Hanga, Hassan Nassor Moyo, Abdulrahman Babu na Salim Said Rashid, ingawa hawa wanne hawakushiriki kwenye mashauriano.
Ukiwachokorachokora tena Wazanzibari watakwambia kwamba katiba yao ya kwanza ilikuwa ile Katiba ya Uhuru ya mwaka 1963.

Baada ya Mapinduzi Januari 12 mwaka 1964, Baraza la Mapinduzi lilipitisha ile iitwayo Kanuni ya Serikali ya Kikatiba na Utawala wa Kisheria mnamo Februari 25 mwaka 1964.
Kanuni hiyo iliagiza ‘Baraza la Kikatiba la Watu wa Zanzibar’ liliitishwe kabla ya Januari 11 mwaka 1965 ili kufanya maamuzi kuhusu katiba mpya ya Zanzibar.

Kwa bahati mbaya agizo hilo halikutimizwa kwa sababu muda si mrefu pakaundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa hakika, Muungano huo uliundwa bila ya Hati za Muungano kuidhinishwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kama ilivyotakiwa iwe kwa mujibu wa hizo Hati za Muungano na kama inavyohitajika kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria za Kimataifa na Utaratibu wa Mikataba.

Taksiri hiyo inaonekana wazi kwa vile ilani inayosema kwamba Baraza la Mapinduzi lilikutana na kuziidhinisha hizo Hati za Muungano ilichapishwa katika gazeti rasmi la serikali ya Tanganyika, the Tanganyika Gazette, na kutiwa saini na P.R. Ninnes Fifoot kwa vile alikuwa na wadhifa wa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanganyika.

Ajabu ya mambo ni kwamba ilani hiyo haikuchapishwa katika gazeti rasmi la Serikali ya Zanzibar, the Zanzibar Gazette, na wala haikutiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, ambaye wakati huo alikuwa Salim Said Rashid.

Kweli kulikuwa na Katiba ya Muda ya Muungano iliyotayarishwa kwa kuibadili kidogo Katiba ya Tanganyika na kuzifanya sheria husika za katiba hiyo ziwe zinatumika pia Zanzibar.
Hiyo lakini ilikuwa ni hatua ya muda na palikuwa na utaratibu uliowekwa wazi kwenye Hati za Muungano wa kuifikia katiba ya kudumu ambayo ilikuwa itungwe katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuundwa Muungano.

Kufikia Machi 24 mwaka 1965 Bunge la Muungano lilipitisha Hati ya Sheria ya Katiba yenye haki na uwezo wa kutunga au kubadilisha katiba. Hati hiyo ilivibadili vifungu vya Hati za Muungano na kukirefusha kipindi cha Katiba ya Muda ya Muungano mpaka utapofika ‘wakati muwafaka’.

Yote hayo yalitendeka licha ya kuwa Bunge la Muungano lenyewe halina mamlaka yo yote ya kisheria ya kuzibadili Hati na Sheria za Muungano bila ya mageuzi hayo pia kuridhiwa na baraza la utungaji sheria huko Zanzibar.

Mtindo huu ulifurutu ada na ulirejelewa mara kadha wa kadha kwa minajili ya kufanya mageuzi ya kisheria au kuongeza mambo katika ile orodha ya mambo yanayopaswa kuwa ya Muungano. Mwalimu Julius Nyerere alibabaishababaisha kwa kusema kwamba: ‘Mamlaka ni ridhaa ya watu. Si kipande tu cha karatasi.’

Kama mamlaka ni ridhaa ya watu basi mamlaka ya Muungano si ya halali kwani watu wa Zanzibar hawakushauriwa iwapo walitaka, walihitaji au walipendelea kuendelea kuwa katika Muungano. Wala baraza lenye kutunga sheria za Zanzibar halikushauriwa kama inavyopaswa.

Mwaka 1977 Nyerere aliiteua kamati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iupige mhuri na kuubariki muungano wa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na ASP. Halafu kamati hiyo ikakabidhiwa jukumu la kuandaa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yalitendeka miaka 13 baada ya kuundwa Muungano licha ya kuwa kwa mujibu wa Hati za Muungano Baraza la Kutunga Katiba lilikuwa likutane kufikia Aprili mwaka 1965 kutunga muswada wa Katiba ya Muungano.

Si hayo tu bali baraza hilo lilikuwa liwe na idadi sawa ya wajumbe wa Tanganyika na wa Zanzibar.
Mwaka 1979 Sheikh Aboud Jumbe, akiwa Rais wa Zanzibar, aliitoa ukumbini Katiba mpya ya Zanzibar miaka kumi na tano baada ya Mapinduzi ijapokuwa, kama tulivyokwishasema, Baraza la Mapinduzi liliamua Februari 1964 kwamba Zanzibar itakuwa na katiba mpya kufikia Januari 11 mwaka 1965.
Katiba hiyo ya mwaka 1979 ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1984.

Tukiiangaza basi historia ya Zanzibar kwa upande wa katiba na utungaji katiba tunaona kwamba Wazanzibari si wageni wa mchakato wa utungaji katiba.
Wazanzibari wanatambua vyema athari za badiliko lo lote katika Katiba ya Muungano kwa vile marekebisho yaliyokwishafanywa kuhusu masuala ya Muungano yaliongezwa kiubabe na Bunge la Tanzania, bunge ambalo halina mamlaka au uwezo wa kisheria wa kufanya hivyo.

Akhasi ya mambo ni kwamba mageuzi hayo yaliifanya Zanzibar ipungukiwe na nguvu zake. Wengine wanahoji kwamba hali hiyo ndiyo iliyopelekea uchumi wa Zanzibar uzorote kwa muda wote huu wa karibu nusu karne.

Tukumbuke kwamba pamekuwako tume mbili — zikiongozwa na Majaji Francis Nyalali na Robert Kisanga — zilizoundwa na Serikali ya Muungano kuutalii mfumo wa Muungano na Katiba ya Muungano.

Mapendekezo makuu ya tume zote hizo mbili yalikataliwa na Marais wa Muungano. Hii rasimu ya sasa ya Muswada wa Sheria wa Mapitio ya katiba ya Muungano inatoa fursa ya tatu ya kuendelea na mchakato huo, kwa nia ya kutaka kuyajuwa maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo yatayopelekea kufanywa mageuzi.

Muda uliowekwa wa mchakato huo ni miaka mitano. Hayo yana maana kwamba kwa muda wa miaka mitano zaidi hali ya mambo itaselelea kuwa vivi hivi ilivyo na Zanzibar itaendelea kugubikwa na ufukara pamoja na uadimikaji wa neema za kiuchumi na kijamii.

Hivyo ni muhimu pachukuliwe hatua za dharura za kuiwezesha Zanzibar kisheria kuwa na mfumo wake wenyewe wa sera za kiuchumi na kijamii zitazoweza kuikwamua nchi hiyo.
Kwa vile huu muswada wa sasa umekataliwa na wananchi wa Zanzibar, wakiwemo miongoni mwao mawaziri kutoka vyama tofauti vya kisiasa, kuna umuhimu wa zoezi hili kuanzishwa upya.

Tena liwe katika mfumo wa mashauriano kati ya serikali mbili, yaani Serikali ya Umoja wa Taifa ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Serikali hizo mbili ziwe wabia wenye haki sawa, yaani ziwe zinashauriana zikiwa washirika sawa katika Muungano, si upande mmoja kujifanya kaka na kuuona upande mwengine kuwa mdogo au usiostahiki haki sawa.
Hii leo ikiwa patafanywa kura ya maoni na Wazanzibari wataulizwa iwapo wanautaka Muungano uliopo na wajibu ama ‘ndio’ au ‘la’ sina shaka yo yote kwamba wengi wao wataukataa.

Hawatoukataa kwa sababu wanaamini ya kuwa kuna mapungufu katika mfumo wake. Wataukataa kimsingi kwani wanaamini ni Muungano ulioifanya hadhi ya Zanzibar ishuke kutoka kuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa ukubwa wa Jumla ya Pato la Kitaifa (GDP) na kutumbukia chubi katika shimo la ufukara na kuwa moja kati ya nchi zilizo na umasikini wa kutisha barani humo.

Kwa ufupi, wanaukataa Muungano kwa sababu wanaamini kwa dhati ya nafsi zao kwamba umewakandamiza.
Kila wakipiga bongo wengi wa Wazanzibari wanaona kwamba mustakbali wa nchi yao utakuwa mzuri endapo tu patakuwako mfumo mpya wa mahusiano baina ya Zanzibar na ile nchi iliyokuwa ikiitwa Tanganyika.

Si hayo tu bali wanataka Zanzibar iwe na mahusiano hayo ikiwa ni mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ili uweze kuhakikisha kwamba Zanzibar badala ya kuwa nchi yenye uhuru nusu inakuwa na uhuru kamili, mfumo huo mpya hautokuwa na budi ila kuirejeshea Zanzibar mamlaka yake yaliyoporwa kwa ghiliba na Tanganyika.

*Raia Mwema
 
Makaimati, asante kwa hii mada, Ahamed Rajab amezama sana ndani ya muungano.
Muungano wetu huu, ni kama ndoa ya mkeka, ndoa ni ndoa, huingia kwa hiyari au ghilba. Ndoa ya hiyari ni pale mume na mke wanapopendana kwa dhati na kuamiua kuoana kwa ridhaa zao. Ndoa za ghilba, ni zile ambazo mwana ndoa mmoja, anakubali au analazimika kuingia kwenye ndoa kwa manufaa fulani, hizi huitwa marriage of convenience. Hata ndoa hizi za convenience, zikishafungwa ni ndoa kamili, hivyo mwanandoa mmoja hawezi kuomba talaka bila sababu ya msingi, tena ni ndoa ya Kikristo, hakuna talaka, mpaka kifo kitutenganishe!.

Kuna ndoa zinazotokana na ghilba, mathalan bibi kushika ujauzito katika starehe zenu, hamkupanga kiuoana, mlipanga kustarehe tuu, lakini kufuatia ujauzito, mkaamua kuoana ili kuepusha kumleta mwana haramu humu duniani, nayo ni ndoa tuu hata iwe ya mkeka!.

Hii ndio ndoa ya muungano wetu, na kwa taarifa tuu, aliyeitaka ndoa hiyo na kuilazimisha ni mke, Zanzibar, aliyejikabidhi kwa mume Tanganyika ili kuzuia waume wengine kumpora uhuru wake baada ya mapinduzi haramu yale, yaliyoishia kubarikiwa na ndoa ya ghilba ya muungano. Ndoa hii ndio iliyoizaa Tanzania.

Baada ya Tanzania kuzaliwa, ndoa hii sasa ni ndoa halali, hakuna kuivunja, hakuna talaka, na hata kufikiria tuu kuuvunja muungano huu ni uhaini!. Hapa hati za muungano hazijalishi, hivyo ni vipande tuu vya karatasi, tena havina sifa za mkataba kutokana na kukosekana kwa ridhaa ya upande mmoja, ila muungano huu utadumishwa kwa dhima ya waasisi wa muungano huo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheokh Abedi Amani Karume.

Kama msingi mkuu wa muungano ni dhima, na sio yale makaratasi ya hati za muungano, them muungano huu utadumu kwa dhima hiyo hiyo hata kama mke atataka kuleta chokochoko ikiwemo kudai talaka, chokochoko hizo zitazimwa na talaka hakuna!
 
Majority ya Wanzibari wanaitambua Katiba ya nchi yao chini ya Ufalme ina maana wengi wao ambao ni wenye asili ya kiafrica walipenda kuishi maisha ya chini ya falme hiyo it does not matter if they are second class citizens or first class.

Sasa baada ya Umma Party kuashiria Mapinduzi (Tanganyika na J K Nyerere Udhibitisho upo hawakushiriki) ni nani walioshangilia wakati huo hayo Mapinduzi? wananchi wengi wenya asili ya kiafrika walikuwa wanafurahia hayo Mapinduzi sasa unasema pia waliipenda Katiba ya Kifalme ya Uhuru? hata hao viongozi uliyowataja?
 
hivi we ni mzalendo kweli? muungano ni wa nchi wala sio CCM, hasara itakuwa pande zote za muungano, uligwa bhebhe CHADEMA? thanks
 
Majority ya Wanzibari wanaitambua Katiba ya nchi yao chini ya Ufalme ina maana wengi wao ambao ni wenye asili ya kiafrica walipenda kuishi maisha ya chini ya falme hiyo it does not matter if they are second class citizens or first class.

Sasa baada ya Umma Party kuashiria Mapinduzi (Tanganyika na J K Nyerere Udhibitisho upo hawakushiriki) ni nani walioshangilia wakati huo hayo Mapinduzi? wananchi wengi wenya asili ya kiafrika walikuwa wanafurahia hayo Mapinduzi sasa unasema pia waliipenda Katiba ya Kifalme ya Uhuru??? hata hao viongozi uliyowataja?

inaelekea unaelewa haya mapinduzi kwa historia za shule but sisi tunojua huwa tunawauliza watu kama nyie yule john okelo alotoka uganda ameletwa na nani ikiwa hivyo unavyosema ni sawa then wale askari vikaptula nao ni askari wa zanzibar?
 
Sio Shule nina CIA na book called 100 Days of Zanzibar Revolution; Niliweka hapa kwenye JF sikuona wewe ukicomment on those articles

Sasa Proove me wrong!! Ina Maana Katiba unayoitaka ni ile ya 1963?

Kassim Hanga knows all about John Okello; Unajua alikuwa anafanya kazi Z'Bar na Pemba miaka ya 1959? - Prove me wrong !!!
 
nyumba yote ni mbovu.dawa ni kuivunja kama kuna ulazima tukajenga nyengine kwa plan ya kileo
 
Nakubaliana na wewe 100% kuwa hakukuwa na haki na uhalali wa Muungano kwa mujibu wa Sheria kwani sheria zilipindishwa na Hata muswada wenyewe wa Kuunda muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliletwa Bungeni kwa hati ya dharula na kuwanyima haki wananchi wa nchi zote mbili kuujadili kwa kina.

Nafikiri mumekuwa na katiba hiyo batili kwa kipindi chote sasa ni wakati muafaka kuandika katiba mpya itakayashirikisha watu wa rika zote na kada zote na kuhakikisha sheria zinafuatwa katika kujenga muungano wenu
 
nyumba yote ni mbovu.dawa ni kuivunja kama kuna ulazima tukajenga nyengine kwa plan ya kileo

Mie sijui huu muungano una faida gani kwa sisi watanganyika. Nadhani ni bora ukafa tu ili hawa ndugu zetu wa visiwani wasilalamike lalamike.
 
Dawa ya ndoa ambayo mwanamke ananyimwa talaka na mumewe hata kama sababu za mke ni za msingi ni kwa mwanamke kupiga uzinzi tu!! Nawashauri zanzibar wapige uzinzi kwa kwenda mbele!!! Ha ha haaaaaaa!!!
 
Written by administrator // 15/04/2011 // Habari-Picha // 2 Comments

mzalendo_3-564x272.jpg

Salma Said,
Huu ni mhadhara wa jumiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu zanzibar (JUMIKI) uliofanyika uwanja wa lumumba skuli baada ya kukataliwa na jeshi la polisi kuandamana viongozi wa JUMIKI walitii agizo la polisi lakini walisema katika mkutano huo maandamano yao yapo pale pale na yatafanyika wakati mwengine licha ya kuwa wamekubali sababu zilizotolewana jeshi la polisi kwa wakati huu
#gallery-1 { MARGIN: auto}#gallery-1 .gallery-item { TEXT-ALIGN: center; MARGIN-TOP: 10px; WIDTH: 33%; FLOAT: left}#gallery-1 IMG { BORDER-BOTTOM: #cfcfcf 2px solid; BORDER-LEFT: #cfcfcf 2px solid; BORDER-TOP: #cfcfcf 2px solid; BORDER-RIGHT: #cfcfcf 2px solid}#gallery-1 .gallery-caption { MARGIN-LEFT: 0px}

Haya ndiyo mambo ya kujadili kwenye katiba mpya

Ushiriki wa watu haukamiliki ikiwa kuna mipaka yao ya ushiriki katika jambo husika

Kwa CCM na serikali yake kuweka kizuizi cha mjadala wa Muungano ni kufunika bomu ili upate kitu cha kukalia...likifumuka linafumuka na wewe

Lazima Wazanzibar waamue kama wanataka Muungano au hawataki, kama wanataka waseme wanataka Muungano wa namna gani.....Vile vile kwa upande wa Tanganyika.....

Ni vema kwa wananchi kuanza kuonesha hisia zetu juu ya Muungano maana mwanzoni tuliubeba kwa kudumisha fikra za mwenyekiti na chama lakini hata leo hatuuelewi Muungano wenyewe ukoje...tusirithishe vizazi vyetu hisia na sikra za mwenyekiti na chama ambazo sisi wenyewe tumeshindwa kuzielewa miaka nenda rudi.....................Big Up wazanzibar
 
nngu007,
Zanzibar ilipata uhuru 1963 na vyama vyote vilishiriki mchakato wa Uchaguzi. Iwapo kama Wazanzibari waliamuwa kuwa chini ya mfalme basi ilikuwa ni hiari yao kama vile watu wa Tanganyika walivyokubali kuwa chini ya utawala wa kifalme wa muiafrika. Sioni tofauti ya ufalme na ule mfumo wa Nyerere wakati ule.
 
Soma kitabu kwaheri ukoloni kwaheri uhuru. Usibakie na cia tu.
 
Back
Top Bottom