Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

048d834584accda0145fb5339a0536da.jpg

Kuna mambo mengi kwenye muungano wa tanganyika na zanzibar ambayo yanaumeza kichwa; baadhi ni....
1. Kuna Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar, kwanini Tanzanyika hawana Rais?
2. Kuna katiba ya Tanzania na Zanzibar wana katiba yao. Kwanini Tanganyika hawana?
3. Kuna bunge la Tanzania na Zanzibar wana bunge lao kwanini?

....ongeza mengine yanayokutatiza.
 
Kwa nini gari ukinunua Zanzibar ukifika nayo Bara unatakiwa ulipie tena wakati ni nchi moja?

Kwa nini Zanzibar na Bara wanatumia leseni tofauti za kuendeshea gari?

Kwa nini usajili wa vyombo vya moto (plate number) unatofautiana kama ni nchi tofauti?
 
Union matters zinashughulikiwa na serikali ya Muungano. Non Union yanashughulikiwa na Serkali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar. Je,non union matters yanashughulikiwa na chombo kipi kwa huku Bara?
 
Nikurekebisha tu, kufutilia mbali sio vyema
mkuu sasa kama hizo nyufa hazizibiki na zaidi sana zinaongezeka
wakati wa nyerere muungaoni uliopo sio wa leo hii. walidhania wanauboresha kumbe wanaongeza ufa
Leo hii

1. zanzibar ina full presedent na anapigiwa mizinga 21

2. zanzibar ina katiba yake kama nchi na wimbo wao wa taifa

3. zanzibar hata kwenye mpira CAF wamewatambua

4. zanzibar kuna mamabo yao muungasno hauyagusi hata chembe - YAANI Muungaono wa chao chao - chetu cha wote. How?

Hata hesabu za chekechea wanajua UNGANO na MUUNGANO. wao wana serikali yao full, Tangayika ya wote. inakuwaje?
sol. 1 seikali moja ama TATU. Hapo utapata muungano sawia. sio muundo wa sasa. jamani tumerogwa?
Tena afadhali sasa hivi hatusumbuliwi visa!! zamani bila visa hugusi lakini wao wanakuja free kama kwenda kariakoo!!!! wapi hiyo. au mpaka tuwe wote kama palamanangada kabudi!!! ( jina gumu hata kulitamka)
 
Ndoa ya kikristo haivunjikagi mkuu
Hii wala sio Ndoa ya kikristo, maana kuna Karume na nyerere waasisi wenyewe tayari kuna hitilafu hapo, karume ruksa nyerere no. Mie naona kuulinda ni kuufanyia marekebesho ya makusudi tu. tupige referendum serikali moja au tatu na hii ya pili utashinda. maana moja wanamapinduzi hawakubali.

Nyerere mwenyewe alishindwa kuondoa baraza la mapinduzi!!! so muunganoi serikali tatu. awepo raisi wa tangayika, na raisi wa zanzibar then rais wa shirikisho sasa hapo waamue huyo raisi wa shirikisho ana dola au hana? au basi tu adopt two states ONLY marekani wana magavana kila jimbo then rais, na kila jimbo lina sheria zake ila kuna fedral; laws . hapo kazi ni kuamua huyu federal presedent ana powers gani?

The easy way serikali tatu kama Warioba alivyopendekeza na tume yake. lakini huu wa sasa kiini macho!!
 
Tunahitaji kutafakari sana kwa hili, Mzee wetu aliwahi kusema kuwa muungano umesaidia usalama kwa bara.
Kwa sasa jama hawa mamwinyi wana kila kitu chao kuanzia bendera, wimbo, rais, na mambo mengine mengi. In Short if we were to vote today then i would vote for a big NO. na sitabadili huu msimamo. Tuachane nao tu manake maandamano kibao hasa ule ugonvi wa deposits za mafuta yalogunduliwa. Katika bajeti ya taifa nadhani wanapata mgao mara mbili kutoka muunganoni na mapinduzini!
mm naona viroba tu ndio vina kusumbua. Zanzibar wamepoteza kila kitu na Tanganyika hawajapoteza chochote zaidi ya jina tu kutokaTanganyika kuwa Tanzania kama liko walilopoteza naomba ututajiye Please.
 
Unachoongea hata mimi nilikiafiki tatizo ni wanasiasa mf leo hii ni rais wa tz; Leo tz ikifa, atakuwa rais wa nchi ipi?
Rais wa zenj ataendelea kuwa rais wa zenj kwa sababu zenj ipo hapo ndipo wenzetu walipojitambua

Unaona ilivyo kaa vibaya hiyo
UFUMBUZI NI KATIBA MPYA.
atakuwa raisi wa Tanzania kwani simumebadilisha jina lenu kutoka Tanganyika kuwa tanzania
 
Lete serikali tatu . kila mmoja ajiwakilishe menyewe mataifa ya nje . Kuwe na jeshi la muungano kama wakati wa Karume, amiri jeshi mmoja pale panapotokea vita kama vile ilivyo NATO. Wazenj ni halali kabisa kumiliki ardhi bara , Zanzibar hakuna ardhi yakutosha ya kilimo. Hiyo ardhi wanayomiliki si wanalima tu kwa faida ya huko huko bongo. Kuna waafrika na watanganyika wengi sana wenye ardhi hapa zenj walioipora wakati wa 1964 mbona hatulalamiki.
 
Usilalamike juu ya uchomaji wa bar za pombe. Kama umefungua bar ndani ya mtaa na inaleta matatizo kwa wakaazi wa sehemu hiyo, watu watakwenda kwenye vyombo vya sheria kuifunga kiusalama kabisa. Ila kama serikali haikuheshimu maoni ya watu na ikaendelea kuleta uchafuzi wa maadili ya watu utapewa onyo na hukusikia tutaichoma na utahama.
 
Habar zenu wanaJF mimi binafsi sijajua maana ya huu muunganiko wetu kati ya bara na visiwan tumeunganika katika lipi.
 
Watakuja na kutuambia kuwa taifa la Tanganyika limekufa/ limepotea baada tu ya muungano
sasa je, kwanini tunasherekea uhuru wa tanganyika kila december 9?
 
Mtanisamehe ila haya ndio niliyoyaona kwenye muungano wetu. Kwa mimi naona Tanganyika na Zanzibar hakuna muungano,

1: Zanzibar wana bendera yao wakati Tanganyika hana.

2: Zanzibar wana wimbo wao wa Taifa wakati Tanganyika hatuna tunatumia wimbo wa muungano ambao unajumlisha Tanganyika na zanzibar = Tanzania.
3: Zanzibar wana Rais wao wakati Tanganyika hawana.
4: Zanzibar wana Serikali yao wakati Tanganyika hawana.

HUWEZI ukasikia wanaita rais wa Tanganyika lazima utasikia Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Wakati huohuo zanzibar wanaita Rais wa zanzibar sasa wa Tanganyika anaenda wapi. Ushauri kama ni Muungano basi kungekuwa na Rais mmoja tuu. Yaani zanzibar wasiwe na rais Au Bara kuwe na rais wa Tanganyika na kule visiwani kuwe na rais wa zanzibar harafu ndo awepo huyo Magufuri kama rais wa Muungano ambaye ataweza kuwacontrol hawa marais wawili.

Mfano leo hii ukiangalia hata plate number za magari kati ya bara na Zanzibar ni tofauti hivyo. Zanzibar hawatumii TANZANIA wao kama kawa wanatumia Zanzibar. Hivyo na sisi tungekuwa na Tanganyika.

basi mnisamehe kama nakosea huu mtazamo wangu tu.
 
Back
Top Bottom