Muungano wa Ulaya umeachia orodha iliyoimarishwa ya mashirika ya ndege yanayodhaniwa kuwa hatari, na kuyakataza kufanya kazi ndani ya anga la EU

Na sisi tuorodheshe mashirika yao ya kuyawekea vikwazo
 
🤣 🤣 🤣
 
🌤️🙋‍♂️🔊🎯👌👍👊👏🤝🙏💐🛡️
 
Huwezi kumvimbia ambaye tairi likiiaha au oil ikiisha unaenda kumpigia goti akuuzie.
 
Usalama ni neno pana tusichukulie kirahisirahisi.

Jamaa wanaangalia maeneo mengi sana, kuanzia technical side, management side, politics side nk
 
Atcl waendane na wakati.Huduma zao ni mbovu sana na ndege zao ni mitumba ndiyo maana wamepigwa marufuku EU.Watanzania tupande Kenya air au Rwanda air ambao wamekidhi ubora wa usalama 100%.
 
Huwezi kumvimbia ambaye tairi likiiaha au oil ikiisha unaenda kumpigia goti akuuzie.
Kwani ni EU peke yake wanaotengeneza tairi na oil za ndege? Huku kujinyongesha kwetu ndiko kunawavimbisha kichwa na kuwapa kiburi cha kutufanyia wapendavyo.
 
Kwani ni EU peke yake wanaotengeneza tairi na oil za ndege? Huku kujinyongesha kwetu ndiko kunawavimbisha kichwa na kuwapa kiburi cha kutufanyia wapendavyo.
Tunajinyongesha au ni wanyonge? Si muanzishe viwanda vyenu? SGR tu watu wanakata nyaya za umeme.
 
Demand ya air services Bado kubwa sana africa

ATC waachene na anga la ulaya Kwa sasa

Bado wachanga sana
Tatizo Air France imepata hasara ya Billion 68 kwa kujifanya kununa kufanya safari za nchi zilizokuwa makoloni yake.

Hio hasara ya miaka 2 tu sasa hizi ndege za kiafrika kwenda Ulaya huleta changamoto kubwa za kibiashara kwao. Lazima waje na sababu ili wabaki wao na huduma ya kutoka ulaya na kuja afrika. Na hizi za Africa zibaki hukuhuku mpaka mashirika yote kufa.
 
Tunajinyongesha au ni wanyonge? Si muanzishe viwanda vyenu? SGR tu watu wanakata nyaya za umeme.
Huko ni kujinyongesha. Kama South Korea tulikuwa nao level moja ya kielimu na kimaendeleo tulipopata uhuru, wao walienda kununua wapi huko kujiamini mpaka wakaendelea kiasi hicho hivi leo? Huku kujinyongesha ndiko kumetufanya tusiweze kutumia vizuri raslimali zetu kibao ili kujiletea maendeleo. Kujiaminisha kuwa sisi ni wanyonge ni ugonjwa hatari wa kufisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…