Muungano wa Ulaya umeachia orodha iliyoimarishwa ya mashirika ya ndege yanayodhaniwa kuwa hatari, na kuyakataza kufanya kazi ndani ya anga la EU

Muungano wa Ulaya umeachia orodha iliyoimarishwa ya mashirika ya ndege yanayodhaniwa kuwa hatari, na kuyakataza kufanya kazi ndani ya anga la EU

Na sisi tuorodheshe mashirika yao ya kuyawekea vikwazo
 
jamani ndio tumeshatapesliwa hivyo..yaani ndege wametuuzia wao alafu leo mdai eti hazina usalama wala vigezo vya kuruka ulaya.! mbona kama wanajua haya walituuzia hizo ndege za nini.!sasa nimeanza kuamini waliosema hizi ndege sio mpya bali ni used mtumba zilizopakwa rangi upya ila ukweli ni za zamani tumepigwa kizembe kweli tumenunua mtumba kwa gharama ya mpya..!
🤣 🤣 🤣
 
Watu tuliojua matatizo ya biashara ya ndege tulisema tangu mwanzo kuwa kutumia hela nyingi kununua midege bila ya kuwa na business plan inayoeleweka ni uamuzi mbaya.

Watu wakatupinga hapa na kununua midege kwa sifa, kufakamia na kujimwambafy.

Matatizo tuliyotabiri ndiyo haya sasa.
🌤️🙋‍♂️🔊🎯👌👍👊👏🤝🙏💐🛡️
 
Dawa ni kuwapiga "tit for tat", badala yake abiria wetu wasafiri kwa mashirika ya nchi nje ya EU halafu tuwaone watafanya nini.
Hawa jamaa na yule ndugu yao anayetishia nchi zinazotaka kuacha kutumia dolla yake wanajaribu kulazimisha ukiritimba wa kumiliki uchumi wa dunia. Wanasahau kuwa hiyo keki ni yetu sote.
Ndege tunanunua toka kwao, service zinafanyiwa huko huko kwao, leo zinakuwaje ni hatari kwa usalama wa anga zao?
Huwezi kumvimbia ambaye tairi likiiaha au oil ikiisha unaenda kumpigia goti akuuzie.
 
Usalama ni neno pana tusichukulie kirahisirahisi.

Jamaa wanaangalia maeneo mengi sana, kuanzia technical side, management side, politics side nk
 
Atcl waendane na wakati.Huduma zao ni mbovu sana na ndege zao ni mitumba ndiyo maana wamepigwa marufuku EU.Watanzania tupande Kenya air au Rwanda air ambao wamekidhi ubora wa usalama 100%.
 
Huwezi kumvimbia ambaye tairi likiiaha au oil ikiisha unaenda kumpigia goti akuuzie.
Kwani ni EU peke yake wanaotengeneza tairi na oil za ndege? Huku kujinyongesha kwetu ndiko kunawavimbisha kichwa na kuwapa kiburi cha kutufanyia wapendavyo.
 
Kwani ni EU peke yake wanaotengeneza tairi na oil za ndege? Huku kujinyongesha kwetu ndiko kunawavimbisha kichwa na kuwapa kiburi cha kutufanyia wapendavyo.
Tunajinyongesha au ni wanyonge? Si muanzishe viwanda vyenu? SGR tu watu wanakata nyaya za umeme.
 
Demand ya air services Bado kubwa sana africa

ATC waachene na anga la ulaya Kwa sasa

Bado wachanga sana
Tatizo Air France imepata hasara ya Billion 68 kwa kujifanya kununa kufanya safari za nchi zilizokuwa makoloni yake.

Hio hasara ya miaka 2 tu sasa hizi ndege za kiafrika kwenda Ulaya huleta changamoto kubwa za kibiashara kwao. Lazima waje na sababu ili wabaki wao na huduma ya kutoka ulaya na kuja afrika. Na hizi za Africa zibaki hukuhuku mpaka mashirika yote kufa.
 
Tunajinyongesha au ni wanyonge? Si muanzishe viwanda vyenu? SGR tu watu wanakata nyaya za umeme.
Huko ni kujinyongesha. Kama South Korea tulikuwa nao level moja ya kielimu na kimaendeleo tulipopata uhuru, wao walienda kununua wapi huko kujiamini mpaka wakaendelea kiasi hicho hivi leo? Huku kujinyongesha ndiko kumetufanya tusiweze kutumia vizuri raslimali zetu kibao ili kujiletea maendeleo. Kujiaminisha kuwa sisi ni wanyonge ni ugonjwa hatari wa kufisha.
 
Back
Top Bottom