Muungano wa Vyama 14 vya Siasa kuongea na vyombo vya Habari

Muungano wa Vyama 14 vya Siasa kuongea na vyombo vya Habari

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Leo wataongea na vyombo vya Habari.
=================
Hotuba nzima ilikuwa ni kumjibu Mnyika na CHADEMA badala ya kuzungumzia ripoti ya Kikosi Kazi.

5588C524-4DE8-493F-8E2B-594A84B8E117.jpeg


"Tumesikiliza taarifa ya @ChademaTz ikielezea kupinga taarifa ya kikosi kazi, tunachoweza kusema kwa sasa, CHADEMA wamejawa na ubinafsi, choyo na wivu mkubwa kuona Tanzania ikiwa kwenye maridhiano huku wao wakiwa nje ya mchakato wa kupatikana kwa maridhiano hayo" @DoyoHassan, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini

"Mhe. Rais @SuluhuSamia amesema wazi kuwa maoni sio amri kwa serikali, wapo wanaokosoa kauli hiyo, nani aliyekwambia maoni ni amri, maoni yanakuwa amri baada ya kutungiwa kanuni na sheria" @DoyoHassan, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini

"Kimsingi tumeshangazwa na viongozi wa kisiasa na moja ya chama cha siasa kupinga ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa na Mhe. Rais @SuluhuSamia, sidhani kama kupinga kule ni kauli ya chama, kwa tunavyofahamu tamko la chama linatokana na vikao vya chama" @BulenduDotto

"Kitendo cha chama cha siasa kupinga jambo ambalo hata hujalisoma, hujui nini kipo ndani yake, hili pekee ni tatizo kubwa. Kwani, hadi sasa taarifa iliyotolewa kwetu wananchi na wajumbe wa kikosi kazi ni muhtasari tu, unawezaje kusema ni mbaya na wananchi msiipokee" @DoyoHassan.
 
Back
Top Bottom