Muungano wa Vyama 14 vya Siasa kuongea na vyombo vya Habari

... kumbe mamluki katika mwamvuli wa vyama vya siasa? Naona wanamtumikia bwana wao aliyewatuma hadi bwana kaamua kuahirisha mkutano na waandishi maana tayari alishawakilishwa na wakeze!
 
"Rais Mhe. @SuluhuSamia alipokutana na Mwenyekiti wa @ChademaTz, @TunduALissu katika kikao chao Lissu aliomba kurejeshewa passport yake na mafao, kwanini hakumwambia Rais masuala ya tume huru na katiba mpya? ili tuone wana nia njema na Taifa hili" @DoyoHassan ACD.
 
Ngoja tuone kama kuna a.mbaye atazungumzia mgombea binafsi kutokuwepo katika mapendekezo ya Tume na pia Tume ya uchqguzi kuajiri wafa yakqzi wake yenyewe kuanzia wilayani hadi Taifa.
 

Kwa hivyo Tundu Lissu akimwambia Rais ndio atatekeleza?. Mbona kikosi kazi kimetoa mapendekezo na bado Rais hajayakubali kasema ataenda kuyaangalia kwa jicho la tatu?.
 
Ccm acheni Sanaa hasa hizi zilizopitwa na wakati! Hivi hamfanyi tafiti za kujua aina ya wananchi mnaojing'ang'aniza kuwaongoza Wana upeo Gani wa uelewa?
Kiujumla mpo nyuma ya wakati mkidhani hii ni mwaka 1977 wa Nyerere na wananchi ni walewale!
Yaani mnahonga posho, ukumbi na agenda za kuongea Kwa watu wasio na mvuto Kisha mnataka wananchi wawaelewe! Hizo ni cheap propaganda ambazo soko lake linapatikana china TU Kwa Sasa!
Kubalini TU kuwa mmechuja na mnahitaji kutiwa rangi Kama batiki!
 
Tatizizo kubwa ni kudhani kuwa CHADEMA inaq hatimiliki ya nembo "upinzani". Wasiposema wao au wakipingwa basi wapingaji ni tawi la CCM. Nchi nyingi, inaposhindikana kukliondoa chama tawala madarakani, huwa vyama vyote vya upinzani vinaungani na kufanya kazi pamoja. Lakini kwa uchu wa madaraka kama ilivyo CCM, CHADEMA inataka ifanye hiyo kazi peke yake itwae uongozi.

Ni muhimu CHADEMA ijue kuwa bila kufanya kazi na vyama vingine vya siasa na kuendelea kuvibeza hivyo vyma ndiyo furaha ya CCM. Pasipo upinzani kufanya kazi pamoja na kudhani kuwa CHADEMA peke yake itatoboa, ni ndoto za mchana.

CHADEMA inazidiwa kete na CCM, maana CCM siku zote inaombea mfarakano kwenye upinzani. Katika vyama vyote CUF kilikuwa chama pekee kilichokuwa na nguvu kubwa hasa kule Zanzibar. Ilichokifanya CCM kila mtu anajuwa, sasa CUF ni karibu marehemu. CCM pia imekuwa ikiichakaza CHADEMA mdogomdogo. Migogoro mingi ndani ya CHADEMA, kama vile kuondoka/kufukuza kwa Zuberi na wengineo amao walikijenga CHADEMA haukosi mkono wa CCM. Lakini CHADEMA hili hawalioni. Wao kila kukicha ni kutaka kujiona ndiyo upinzani pekee na hivyo vyama vingine havina kitu.

Nafikiri tatizo kubwa ni uroho wa madaraka na kujitakia misifa. CHADEMA wanateka ikiwezekana washinde kura na washike nchi peke yao, maana wakiungana ukipatikana ushindi, inabidi wagawane vyeo. Ni hatari kuwategemea wanasiasa wachache na kuwaabudu kama Mungu, kudhani peke yao ndiyo wataleta mafanikio. Acheni kubeza vyama vingine. Kaeni navyo mpange mikakati ya kuiondoa CCM kwenye madaraka, lakini hii ya kufikiria CHADEMA pekee itafanikiwa ni ndoto. Sana saana mtaishia kupata ruzuku na kulipana mishahara, lakini kushika nchi hamtaweza bila kushirikiana na vyama vingine vya upinzani.
 
CHAMA CHA UPINZANI TANZANIA NI KIMOJA TU AMBACHO NI "CHADEMA" NYIE WENGINE NI MAMLUKI
 
Takataka hii
 

Kweli CHADEMA ni tishio aliongea Mbowe kuhusu tozo Mwigulu akajitokeza kujibu , Sasa kaongea mnyika kidogo vyama 14 ikiwemo na CCM vimejitokeza kujibu.

Na Sasa CHADEMA imetangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima nadhani IGP lazima atoke kujibu mapigo na kutoa vitisho.
 
CDM kwa aina yao ya siasa ndio kinaifanya CCM isiweze kulala, na kwa kiasi kikubwa kinaifanya CCM izidi kutumia vyombo vya dola, maana nje ya vyombo vya ni lazima ipotee kama KANU ya Kenya. Ni Mbowe tu alizengua kwa kwenda ikulu kupoteza muda.

Mbowe alizingua Sana. Alikuwa hana Cha kupoteza umekaa rumande karibia miezi Saba bila kosa unaendaje kuongea na mama Samiah aliyekutangaza kuwa ni gaidi, tena BBC. Angeendeleza harakati Leo mambo yangekuwa tofauti. Wamemwachia mama kila kitu ataangalia kwa jicho la tatu.
 
22 October 2022

CHADEMA WAREJEA RIPOTI YA JAJI WARIOBA SIKU CHACHE BAADA YA KIKOSI KAZI KUKABIDHI MAPENDEKEZO YAKE

Source: chadema media
 

Ndio maana huwa nasisitiza Mbowe asistaafu siasa bali apumzike kwenye nafasi ya uenyekiti. Kwa mtu wa umri na manyanyaso wanayoweza kupata viongozi wa chama kikubwa hivyo, ni vyema akapisha mwenye mwili wa kumudu shuluba, kuliko kujiangusha ndani ya 18 ukitegemea kupata penalti.
 
Haya sasa, hawa nao wanataka wawe wanapewa RUZUKU!

Kodi za wavuja jasho wa nchi hii, kwa akili mbovu kama hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…