Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Tanganyika siyo JMT kwa sababu kwenye ramani, Tanzania imejumlisha na Zanzibar. Na kama Tanganyika ingekuwepo ingeonekana kwenye ramani. Usipuuze ramani, maana nchi zinatambulika rasmi kupitia kwenye ramani. Chama cha wanasheria wa Tanganyika kilianzishwa wakati Tanganyika ipo kwenye ramani. Lakini leo Tanganyika haipo.
 
Tanyanyika iko wapi? Kama Tanganyika bado ipo basi hata Buhaya, Busukuma, Chaga kingdom, na zinginezo bado zipo. Lakini nyie wenyewe mlimsikiliza Nyerere na mlikataa makabila yenu. Leo mnaioenea wivu Zanzibar mnataka kuirudisha Tanganyika kwa nguvu ambayo huyo huyo Nyerere aliiuwa.
 
Nakuonea huruma kwa sababu unachangia jambo usilo na uelewa nalo.

Huo mgawanyo wa Zanzibar kupata 4.5% imetamkwa wazi kuwa ni kwa misaada ya nje na mikopo toka nje.
Mikopo huwezi kugawa kwa asilimia hasa mikopo ya maendeleo. Kwa mfano mradi wa maji Arusha $500M una gawa 4.5% kwa Zanzibar!! Au fly over ya ubungo ni mkopo wa world bank pesa ngapi imegaiwa Zanzibar?. Ujenzi wa Airport ya Zanzibar watagawa vipi kkutupa 95.5 bara! Tatizo watu wengi hamfikirii vizuri mnapenda ushabiki zaidi kuliko kujua. Mapato ni tofauti maana ni makusanyo, misaada nayo ya nchi inawezekana lakini siyo yote mfano msaada kwa Tanzania wa kupunguza uaribifu wa bahari Tanzania utajumuisha mikoa yote yenye bahari na zanzibar. Msaada wa usafi wa maziwa huwezi kupeleka Zanzibar bali kigoma, kanda ya ziwa…… . Misaada ni miradi na kitu tofauti sana
 
Kwa fact hizi, kinachofanyika kwenye hii migao inayopelekwa zanzibar ni hujuma kwa Tanganyika...........wanaenda kuingiza Tanganyika kwenye madeni makubwa na umaskini wa kutisha.
 
Unaongelea yiyopo kichwani mwako au unaongelea articles of union zinasema nini kuhusu misaada na mikopo ya nje?
 
Kwa hiyo kila kilichoanzishwa wakati Yanganyika ipo, kimeendelea kuwa cha Tanganyika?

Kuna ramani inalitaja ziwa Nyasa ni Lake Malawi, na ramani nyingine zinalitaja Lake Nyasa. Kwa uelewa wako, kwa sababu hayo yote yapo kwenye ramani, ni sahihi?
 
Unaongelea yiyopo kichwani mwako au unaongelea articles of union zinasema nini kuhusu misaada na mikopo ya nje?

Flyover ya Ubungo ni mkopo Zanzibar imepata kiasi gani? Pesa ya maji Arusha ni mkopo Zanzibar imepata kiasi gani? . Hakuna mgao kwenye miradi mgao ni kwenye misaada au mapato. Sababu kubwa mahitaji haya fanani! Tufikirie badala ya kuweka ushabiki
 
Kwa hiyo kila kilichoanzishwa wakati Yanganyika ipo, kimeendelea kuwa cha Tanganyika?

Kuna ramani inalitaja ziwa Nyasa ni Lake Malawi, na ramani nyingine zinalitaja Lake Nyasa. Kwa uelewa wako, kwa sababu hayo yote yapo kwenye ramani, ni sahihi?
Hilo ziwa lina mgogoro (border dispute) ndiyo maana unaona kuna ramani zinasema ziwa Nyasa zingine zinasema lake Malawi. Mgogoro ukitatuliwa (reached settlement) ramani nazo zitabadilika. Ni sawa na ghuba ya uajemi, waarabu wanaiita Arabian Gulf, Iran wanaiita Persian Gulf. Wakitatua migogoro yao hiyo ghuba itaitwa jina moja na ramani zitabadilishwa. Kuna mifano mingi tuu mengine ya sehemu au majimbo ambayo yana migogoro. Tanganyika haina mgogoro, ilishakufa rasmi. Ndiyo maana haipo kwenye ramani yoyote ile kwa sababu haitambuliki rasmi.
 
Huu Muungano utaendelea kubakia kuwa ni wa kipuuzi tu miaka yote. Sijaona faida yoyote ile kwa Tanganyika kuungana na Zanzibar.

Huwezi kuungana na watu wabinafsi, na wategemezi siku zote! Watu wa changu changu, chako changu!
Kwahiyo watanganyika muko tayari muungano uvunjike?
 
Kwa fact hizi, kinachofanyika kwenye hii migao inayopelekwa zanzibar ni hujuma kwa Tanganyika...........wanaenda kuingiza Tanganyika kwenye madeni makubwa na umaskini wa kutisha.
Ha ha ha- payback period kwa kuwakandamiza wazanzibar miaka zaidi ya nusu karne. Hii curtain raiser subiri main show mjomba.
 
Ha ha ha- payback period kwa kuwakandamiza wazanzibar miaka zaidi ya nusu karne. Hii curtain raiser subiri main show mjomba.
Mkuu huoni kwamba Tanganyika ikikunjua makucha yake unaelewa ni nani ataumia........anyway, iachwe kama ilivyo nafikiri hatutasikia tena huko mbeleni malalamiko ya kero za muungano hata mama atakapoondoka.
 
Hata kesho uvunjike tu! Mbona hatuna cha kupoteza! Na nyinyi mbakiwe na Visiwa vyenu vya karafuu.
Shida ni kwamba nyie ndio wenye kuung'ang'ania huo muungano, mpaka mwalimu nyerere kuamua kumuua mzee karume ili alinde maslahi yake anayoyapata kwenye muungano.

Hapa ni kusema kwamba, tanganyika wamenufaika zaidi na huo unaoitwa muungano, kwa sababu wazanzibari walitaka kujitoa zamani kwenye uonevu huu.

Your browser is not able to display this video.
 
Mumeona haitoshi kuinyonya mamlaka Zanzibar mpaka mukaufanya muungano kuwa vita ya kidini.
 
Mwaka huu ndio mtajua hamjui! Mgao ni kati ya Tanzania na Zanzibar. Hakuna kitu inaitwa Tanganyika kwa sasa, Tanganyika iendelee kujificha kwwnye koti LA Muungano, naona tayari lishaanza kumbana anatoa sauti sasa. Hata bado had I kufikia 2030 Lazima Tanganyika itaomba poo kwa Zanzibar.
 
Weka hapa huo mkataba wa Muungano.Pili unaelewa maana ya kero za Muungano? Na je mkataba ni biblia au msahafu?

Mwisho Zanzibar sio Mkoa ni Nchi na pia ni sehemu ya JMT kwa hiyo ina haki zote na tena haki zaidi ya Mkoa.
Kama ni nchi basi mkakope nyie sio kutumia tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…