Rukwa, Katavi na Mbeya hizo percentage ni nyingi sanaKwa maoni yangu DSM, Tanga, ni Waislamu by 60.
Lindi Waislamu 70%.
Tabora 50
Mtwara 50
Pwani 70
Moro 50
Dom 40
Ruvuma 40
Kigoma 30
Kagera 30
Geita 05
Mara 20
MWANZA 20
Shinyanga 30
Simiyu 10
Singida 30
Manyara 20
Arusha 10
Kilimanjaro 20
Mbeya 10
Rukwa 10
Katavi 10
Dom 40
Iringa 20
Njombe 10
Hizo ni % ninazo wapa Waislamu katika Mikao. Ya Tz
Note siyo takwimu Rasmi. Ni maoni yangu binafsi
Waliambiwa hiyo sensa waifanye kwa muda wao sio kwa mgongo serikali maana hizo ni kodi zetu, sasa sijui walitaka mtelezo, kufanya sensa hakuna anayewazuiaWe jamaa bna,maaskofu 2012 walimpinga ponda kutaka waislam wasihesabiwe mpaka pawekewe column ya dini kwenye sensa,maaskofu walitoka shimoni kupinga,wakati huo kwenye kalenda ya ofisi wa Waziri mkuu wametoka takwimu ati waislam 30%
Saana
Ilikua kuongeza column tu ya swali la dini,haikuhitaji karatasi zimaWaliambiwa hiyo sensa waifanye kwa muda wao sio kwa mgongo serikali maana hizo ni kodi zetu, sasa sijui walitaka mtelezo, kufanya sensa hakuna anayewazuia
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa pesa ya naniIlikua kuongeza column tu ya swali la dini,haikuhitaji karatasi zima
Unajua maana ya column!?
Kwani huku bara Hatuna ustaarabu wetu?Nyinyi watanganyika hemu acheni tabia zenu za kibishi bishi mnavokuja kuweleza huku visiwani. Zanzibar tuna ustaarabu wetu kwaio mkija huku muwe mnakuja na adabu zenu
Wakati wa sultanate zanzibar ilikuwa na maendeleo makubwa ila baada ya mapinduzi na muungano imeanguka
Uncivilized, seriously? Na wewe unayeiga vya watu mpaka majina ya kina Marco Polo ndiyo umejiona umefiiika hapo kwenye maendeleo!Wazanzibar ni wabaguzi sana Niko nao huku yaan ni very uncivilized sijui wanajionaga kina nani aisee? Rais wa nchi kusimama mbele ya hadhara eti mm ni mzanzibar!! shame!! Mbona huongozi nchi ukiwa huko zenji kutwa upo bara.
Bora ya mwarabu kuliko mkoloni mweusi.
Uncivilized, seriously? Na wewe unayeiga vya watu mpaka majina ya kina Marco Polo ndiyo umejiona umefiiika hapo kwenye maendeleo!
[emoji23][emoji23][emoji23] umejua kunichekesha mkuu!Ukishaona watu school wanaiita skuli fikiria mara mbili kisha chapa lapa [emoji205]
Zanzibar ni kama limao lililopandikizwa kwenye mchungwa!Tatizo tunashindwa kuelewa Zanzibar ni nchi na INA sheria zake japokuwa ipo katika muungano na Tanganyika, hivyo sheria zake muda mwingine zinawezakuwa tofauti na za Tanganyika kikubwa kutambua na kuheshim kwa maana nchi bila sheria ni jalala.
muacheni mzee apmzike tupambane vijana haya yote yanatokea kwa sababu ya unafiki mwingi tunaoufanyaga viongozi wa baraKinachosumbua hapo ni udini
Sekta ya elimu inatakiwa kuwa huru mfano Tanzania bara ni hiari ya shule kufundisha masomo ya Dini au kuyaacha kabisa.
Za private ziko Muslim schools na Christian schools.
Mtu alienda Muslim schools anakutana na ya kiislamu kibao kuanzia kuvaa hizo hijabu nk akienda Christian schools atasali kikristo nk Na wazazi huridhika
Zanzibar hicho kinafanyika ni kutaka kulazimisha mwenye Shule ageuze shule kwa lazima iwe Muslim school
Zanzibar mbona Muslim schools ziko kibao wazazi wapeleke watoto wao huko huo ni ukorofi usio na sababu mtu kafungua Christian school yake kwa Nini umkomalie kuwa lazima iwe Muslim school.
Hii ichukuliwe kama kero ya muungano.Ichukuliwe wazi kabisa kuwa huyo mwenye shule ananyanyaswa kidini
Raisi Mwinyi aingilie kati Hilo swala haraka
hivi mnajua historia yenu wazanzibar mmetokea huku ndio mana kila unayemuuliza ana historia ya bara tukiwaachia waarabu watakuja kuwatandika viboko kulipizua mapinduzi ila nyie ni sawa na wilaya tu ya geita huku baraMi mwenyewe huwa nashangaa mnavyotung'ang'ania. Mliwafunga watu miaka mingi bila ushahidi 😀 kisa tu wanasema zanzibar kwanza. Wazanzibar walikwisha ukataa huu Muungano kitambo tu tena kwa kusema wazi wazi kwenye majukwaa, nyie mmefanya nini zaidi ya kuwa Keyboard warriors 😀
fuatilia data zako vizuriHaha. Wapi Kanda ya Ziwa na Magharibi ndiyo Kuna birth rate kubwa na huko ni 80% Wakristo.
Wewe ndio uone aibu kwa kukosa elimu na maarifaUkishaona watu school wanaiita skuli fikiria mara mbili kisha chapa lapa [emoji205]
I just love youSehemu yoyote, waislam wakiwa wengi ni shida, hata hapa bongo waislam siku wakiwa wengi kuzidi wakristo itakuwa shida
Ukiwa Zanzibar heshimu Katiba, Sheria na kanuni zote za Kisiwa hiko period.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imeifutia usajili Skuli ya Eden inayomilikiwa na Shirika la Afrika Agape Association kuanzia Januri 3 mwakani.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wizara kubaini mmiliki wa Skuli hiyo kuendesha Skuli kinyume na sheria, miongozo na kanuni za Wizara.
Akizungumza na wamiliki wa Skuli hiyo huko Shakani Kaimu Mrajis wa Elimu na Katibu wa Baraza la Elimu Zuwena Mataka Hafidh, amesema kumekuwepo malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wazazi hali iliyopelekea Wizara kuchukua maamuzi hayo.
Ameyataja baadhi ya malalamiko hayo ni pamoja na Wanafunzi wa kislam kutosomeshwa somo la dini ya kislaam na kiarabu, kulazimishwa kujifunza dini ya kikiristo, kutotakiwa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na Wanafunzi kutoruhusiwa kuvaa hijabu.
Malalamiko mengine amesema kupandishwa ada bila ya utaratibu, kutokuwa na mashirikiano mazuri baina ya wazazi, walimu na mmiliki wa skuli na mmiliki huyo kuendesha skuli kwa hisia zake binafsi.
Aidha amebainisha kuwa malengo ya Wizara sio kuifutia leseni Skuli hiyo bali ni kuhakikisha inafuata sheria na miongozo ya Serikali katika kuendesha Skuli yao.
Kaimu Zuwena, amebainisha kuwa mmiliki wa Skuli hiyo amekuwa mgumu kufuata sheria na miongozo ya Wizara na kuendesha Skuli yake anavyotaka yeye jambo ambalo halivumiliki.
“Haiwezekani Skuli kuendeshwa bila ya kufuata miongozo ya Wizara kwani tuna skuli 590 hatutakuwa tayari kuona mmiliki yoyote wa skuli binafsi anakwenda kinyume na utaratibu na hatutasita kuchukua hatua,” amesisitiza.
Hata hivyo, amesema Skuli hiyo imekuwa ikifatiliwa mara kwa mara na kupewa maagizo ya kurekebisha kasoro hizo lakini haizingatii maagizo anayopewa na badala yake kuendelea kuendesha skuli kinyume na sheria.
Amesisitiza kuwa skuli yoyote ya binafsi inatakiwa kufuata sheria, miongozo na mambo mbalimbali yanayotolewa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Nae Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mjini Magharibi, Amosi John Henock, amesema toka skuli hiyo kusajiliwa mwaka 2010 imekuwa ikijitokeza migogoro baina ya mmiliki na jamii pamoja na kushindwa kujirekebisha baadhi ya kasoro ambazo alitakiwa kuzifanyia kazi.
Aidha amesema Skuli hiyo imeshawahi kufungiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud na kutakiwa kurekebisha kasoro zilizoonekana lakini aliendelea kukaidi.
Amesisitiza kuwa Skuli hiyo haitaendelea kufundisha mpaka pale itakapokubali kwenda sambamba na maagizo ya Serikali katika kuwapatia watoto elimu.
Amesema hata katiba ya Zanzibar imeeleza wazi kwamba mtu yoyote hapaswi kufanya jambo lolote kwa lengo la ubaguzi wa moja kwa moja ama kwa taathira yake.
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Shakani bi Mwanaisha Khamis Rashid amebainisha kuwa mara nyingi amekuwa akikaa na uongozi wa Skuli hiyo katika uendeshaji elimu kwa kufuata miongozo na mitaala ya Wizara lakini hakuifuata.
Nae mmiliki wa skuli hiyo bwana Youung Am Kim ameahidi kuheshimu maamuzi ya Wizara ya Elimu ya kutofungua Skuli na hiyo na kuwajuillisha wazazi juu ya suala hilo.
Aidha amesema atahakikisha anafuata sheria ya elimu ya Zanzibar na kuondoa changamoto ambazo zinalalamikiwa kupitia Skuli yake.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake Mwalimu Ummy Aga amesema wameweka jitihada binafsi kwa wanafunzi wao kuona wanafanya vizuri katika mitihani yao na kujipima katika ufundishaji lakini kufutwa kwa Skuli hiyo imeondosha ndoto yao kwa Wanafunzi wao.