Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Jua lilikuwa serious na kazi yake aisee

Acha tuu, ilikuwa haina haja ya kwenda Sauna Bath. Mafuta yote yalikuwa yanayeyuka mwilini.

Nilikuwa nikirudi nyumbani naoga maji ya baridiii halafu naacha maji yakauke yenyewe.

Na baada ya nusu saa naanza kutoka jasho upya.
 
Pole sana mkuu.
Hii tabia nchi tumejiletea wenyewe kwa kupambana dhidi ya mazingira
 
Pole sana mkuu. Vipi hali ya mvua sasa? Bado inaendelea kunyesha?
 
Pole sana mkuu. Vipi hali ya mvua sasa? Bado inaendelea kunyesha?
Muda huu inashuka ile mama yake ya jana. Huku ninapoishi hata magogoni ikizama sisi tunakuwa wa mwisho.

Nimefumbata mikono nawaombea wanadaresalama wenzangu ambao ahsubuhi hii wanatatarika katikati ya mvua na katarina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…