Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

bora jua sijui sema linachoma na lenyewe

Yaani jua la Desemba lilijua kuniwakia aiseeh, nilikuwa na hekaheka za kariakoo, buguruni, ilala karibu kila wiki.

Unatiririka jasho zile leso kubwa unajifuta inajaa majasho inakuwa mbichi unafanya kuikamua.

Nilikuwa nikitoka nabeba leso 3, miwani ya jua na mwamvuli. Nikirudi nyumbani nafikia bafuni navaa kivesti gauni nakaa mezani kula matunda aiseeh navuja majasho utasema kuli wa bandari.
Sema sikuwa na kitoyoyozi na feni inaniumiza mafua, basi tabu tupu.

Kwenye jua unapigika na joto na majasho ila shughuli zinafanyika na zinaendelea kama kawaida.

Mvua sasa, hali ya hewa nzuri ila shughuli zinasimama, saa ingine hata kama una gari hutoki, barabara hazipitiki, foleni, yaani mateso bila chuki.

Bongo daresalamu.
 
Asee, ukuta umesha piga chini apa nilipo

Aiseeeh, Pole sana.

Kama kuna mkondo wa maji, ukijipanga kujenga ukuta mwingine, kwenye msingi weka madirisha ya nondo kuruhusu maji kupita halafu juu ukuta unapanda kama kawaida.

Hapo hata mafuriko yakija ukuta haudondoki.

Mfano wa huu ujenzi ni ukuta wa Interchick kule mbezi Beach. Walihangaika sana na ule ukuta ulikuwa unaanguka kila mwaka wanajenga.
 
Uko wapi tupeane kampani weekend hii
 
jua la december ni balaaaa kuna jua linawa makumbusho mpaka unajiuliza kwani huku wamemkosea nini Mungu πŸ™ŒπŸ»πŸ™ŒπŸ»


kariakoo mi naenda na vitambaa viwili na lazima nirudi na vipya viwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…