Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Yaani jua la Desemba lilijua kuniwakia aiseeh, nilikuwa na hekaheka za kariakoo, buguruni, ilala karibu kila wiki.

Unatiririka jasho zile leso kubwa unajifuta inajaa majasho inakuwa mbichi unafanya kuikamua.

Nilikuwa nikitoka nabeba leso 3, miwani ya jua na mwamvuli. Nikirudi nyumbani nafikia bafuni navaa kivesti gauni nakaa mezani kula matunda aiseeh navuja majasho utasema kuli wa bandari.
Sema sikuwa na kitoyoyozi na feni inaniumiza mafua, basi tabu tupu.

Kwenye jua unapigika na joto na majasho ila shughuli zinafanyika na zinaendelea kama kawaida.

Mvua sasa, hali ya hewa nzuri ila shughuli zinasimama, saa ingine hata kama una gari hutoki, barabara hazipitiki, foleni, yaani mateso bila chuki.

Bongo daresalamu.
"inakuwa mbichi unafanya kuikamua", wee mama mbona unanitia vishawishini.
 
Wakazi wa dar mnafirahisha, mvua kidogo mnafungua thread, huku kugoma radi zinapigwa mpaka miti inakauka lakini fresh na watu hawawezi wala nini? Lakini poleni maana kwa dar mvua kunyesha sio kawaida.
Ndio tofauti ya dar na kigoma, mvua ya nusu saa dar ni tofauti na mvua ya saa tatu kigoma!
 
Back
Top Bottom