Mvutano ndani ya CCM ni alama ya kuvifungua akili vyombo vya dola. Vikiwa makini huu ndo wakati wa kusimika mifumo imara

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Siasa za Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi ni siasa za makundi kugombania Madaraka na Ulaji.

Makundi yote yanafanana kwenye jambo kuu moja. Uchu wa madaraka ili kuila keki ya Taifa vizuri. Makundi yote haya yanaamini yakishika utawala wa nchi basi watapata hela wapendavyo, wataishi vizuri wapendavyo. Wataishi kama wako peponi kwa kodi za Wananchi.

Tofauti pekee ya haya makundi ni hii. Kundi moja lina amini CCM ndo nchi na Serikali na Mifumo inapaswa kuwajibika kwa CCM.( kundi la Polepole na wenzao wanajulikana kama Sukuma Gang)

kundi la pili lina amini mifumo ya nchi ni vizuri iwepo ila inapaswa ifanye kazi ya kuilinda CCM. Hawa wanaamini mifumo haipaswi kuwa huru hasa katika kutenda haki dhidi yao pale wanapoila nchi na kuifisadi wapendavyo.( Kizimkazi Gang/ Msoga Gang)

Ukitizama kwa makini hakuna kundi kati ya haya linayoiweka Tanzania mbele. Hakuna kundi linalopigania maslahi mapana ya Taifa hasa kwenye masuala ya Utawala Bora, Ukweli na Haki.

Taifa lolote duniani linasimama imara na kudumu kwenye uimara kwa muda mrefu pale panapokuwa na Utawala Bora, Ukweli na Haki.

Taifa lolote duniani linakuwa imara pale panapokuwa na mifumo imara inayosimama imara dhidi ya Wanasiasa na hila zao. Bila kusahau ngebe zao.

Ni bahati nzuri kwa sasa nchini Tanzania ni Cha kimoja tu cha siasa kinachosimama bila haya na kusema ukweli wa wazi kuwa nchi yetu inahitaji Katiba Mpya iliyo Bora inayosimika mifumo imara. Maana bila hiyo mifumo kila siku tutakuwa tunazunguka mbuyu bila kutatua kiini cha tatizo linaloimaliza Tanzania. Chama hicho ni CHADEMA.

Kwa yanayoendelea huko CCM ambapo kuna vita ya makundi kugombea madaraka ni vizuri vyombo vya dola vikajifunza na kulazmisha nchi yetu inapata Katiba Bora inayohakikisha nchi inasimamiwa na mifumo imara na sio Wanasiasa wenye uchu wa madaraka na hila zao.

No Reform No Election ✊️✌️
 
Siasa za Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi ni siasa za makundi kugombania Madaraka na Ulaji.

Makundi yote yanafanana kwenye jambo kuu moja. Uchu wa madaraka ili kuila keki ya Taifa vizuri. Makundi yote haya yanaamini yakishika utawala wa nchi basi watapata hela wapendavyo, wataishi vizuri wapendavyo. Wataishi kama wako peonies kwa kodi za Wananchi.

Tofauti pekee ya haya makundi ni hii. Kundi moja lina amini CCM ndo nchi na Serikali na Mifumo inapaswa kuwajibika kwa CCM.( kundi la Polepole na wenzao wanajulikana kama Sukuma Gang)

kundi la pili lina amini mifumo ya nchi ni vizuri iwepo ila inapaswa ifanye kazi ya kuilinda CCM. Hawa wanaamini mifumo haipaswi kuwa huru hasa katika kutenda haki dhidi yao pale wanapoila nchi na kuifisadi wapendavyo.

Ukitizama kwa makini hakuna kundi kati ya haya inayoiweka Tanzania mbele. Hakuna kundi linalopigania maslahi mapana ya Taifa hasa kwenye masuala ya Utawala Bora, Ukweli na Haki.

Taifa lolote duniani linasimama imara na kudumu kwenye uimara kwa muda mrefu pale panapokuwa na Utawala Bora, Ukweli na Haki.

Taifa lolote duniani linakuwa imara pale panapokuwa na mifumo imara inayosimama imara dhidi ya Wanasiasa na hila zao. Bila kusahau ngebe zao.

Ni bahati nzuri kwa sasa nchini Tanzania ni Cha kimoja tu cha siasa kinachosimama bila haya na kusema ukweli wa wazi kuwa nchi yetu inahitaji Katiba Mpya iliyo Bora inayosimika mifumo imara. Maana bila hiyo mifumo kila siku tutakuwa tunazunguka mbuyu bila kutatua kiini cha tatizo linaloimaliza Tanzania. Chama hicho ni CHADEMA.

Kwa yanayoendelea huko CCM ambapo kuna vita ya makundi kugombea madaraka ni vizuri vyombo vya dola vikajifunza na kulazmisha nchi yetu inapata Katiba Bora inayohakikisha nchi inasimamiwa na mifumo imara na sio Wanasiasa wenye uchu wa madaraka na hila zao.

No Reform No Election [emoji110]️[emoji3577]
Sio wakati muafaka kwa sasa.
 
Hakuna chombo chochote cha dola kilicho huru - vyote vipo chini ya CCM.

Sasa swali je huyo CCM ni nani?
 
This is a myth ambayo haina ukweli wowote. Wakiamua wanaweza.
 
Back
Top Bottom