Mvutano wa kisheria, tuhuma ya msanii aliyechoma picha ya Rais

Choma tu, kinachokatazwa ni kunyofoa picha za kampeni na kuziharibu wakati kampeni zikiendelea
Nimecheka wakili anauliza maswali, kachoma picha iliyopigwa au kuchorwa na nani ambae sasa analalamika? Na mnajuaje picha iliyochomwa inafanana na Samia hadi mseme kachoma picha ya Samia, toa ushahidiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Halafu nimemwona Kamanda wa Polisi Mbeya ni mtupu aliposema, sie tumemkamata tunasubiri DPP atuambie tumemkamata kwa kuvunja sheria ipi! Yaani Polisi wa Tanzania bwana, ovyo sana. Sasa kwa nini Mkuu wa Mkoa aliposema kamkamate hamkuuliza haya maswali? Kuna siku Kamanda wa Polisi ataambiwa amkamate mwanamke kwa sababu kamkataa mkuu wa mkoa. Wawe na ujasiri wa kuuliza unatutuma tumkamate huyu mtu kwa kuvunja sheria gani na kushauri kama ni sawa kumkamata au la. Polisi wasiwe wanaamrishwa na wanasiasa kama hawana akili kichwani, ni roboti tu.

Hivi kama mimi ni msanii, nikachora picha ya Samia, lakini watu wakasema nimekosea macho sijayafanya marembo kama yalivyo ya Samia, na kidevu sijaweka cha mfuto kama chake, nikaamua kuichoma ili nichore picha nyingine, nitashitakiwa kwa kosa la kuchoma picha ya Samia?
 
Wewe mbona unakurupuka hapa ni mtoto wa maskini? Au kwa kuwa uko upande wao ndio unajiona uko sahihi
 
Picha ya kuchorwa yazua taharuki baada ya kuchomwa moto...
Nani aliichora, swali fikirishi je ilichorwa vizuri kama haikuchorwa vizuri kosa hapo ni yule aliyepiga picha inawezekana picha haikuchorwa vizuri
 
Mwenye kosa hapo ni aliyekupiga hiyo video ama picha wakati unaichoma hiyo picha swali fikirishi je picha uliyo ichora vibaya uitunze ama uiteketeze
 
Huenda picha ya raisi ni sawa na nembo ya taifa, ni sawa na kuchoma wekundu wa msimbazi hadharani, umelidharau taifa.
 
Very true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…