Mwabukusi, Lissu, Nshalla na Mbowe mmetuharibia mjadala wa Bandari

Mwabukusi, Lissu, Nshalla na Mbowe mmetuharibia mjadala wa Bandari

Issues hapa ni terms za milataba vinavyoondoa sovereignty ya nchi ndio watu hawataki ( sasa hapo huelewi wap? ). Kama hujasoma hizo terms hapo uko sawa tofauti na hapo you are demonstrating your own ignorance,,,,
 
Du, ndio CHADEMA hii, inayotarajia kushika Dola 2025. Kweli wananchi watawapa kura nyie, halafu mkishindwa eti msingizie mmepigwa/mmeibiwa. Kelele za DPW mnadhani zinatosha kwenda ikulu! Mama anarudi ikulu kirahisi sana 2025.
CHADEMA ni janga la taifa.
 
Heshima kwenu Wakuu,

Majamaa tajwa hapo juu yawezekana kuwa wamelipwa rushwa kubwa sana na mamlaka za juu ili waharibu mjadala wa kitaifa juu ya uwekezaji wa DP WORLD katika bandari ya Dar es Salaam.

Hili limetokana na ukweli kwamba mara tu mjadala ulipoanza watu hawa walikimbilia kushambulia watu na kukandia asili zao badala ya kujadili hoja iliyopo mezani.

Wengine kama Nshalla walienda mbali mpaka wakafikia kumutukana Rais matusi mabaya kabisa.

Hawa wameonekana dhahiri kutumiwa na Serikali kuharibu mjadala kwa sababu za wazi zifuatazo:
1. Huwezi ukamtukana Rais halafu tena watu wakazingatia unachokiongea badala yake kila mtu ataamka na kumlinda huku akipuuza unachosema.

2. Kuwabagua wazanzibar na kuonesha kuwa hawana haki ya kusimamia mambo ya nchi wawapo viongozi. Hapa Mbowe, Mwabukusi na Lissu wameonesha dhahiri kuwa wamekula mlungula wa kutosha ili wajifanye wanawashambulia wazanzibar kisha watu wasimame kuwatetea na agenda ya msingi isahaulike.

Hawa jamaa wameharibu kila kitu na watajibu siku ya kiama kwa kukubali kutumiwa ili kuwasahaulisha watu agenda muhimu na nyeti.
Wewe kakulipa nani
 
Wewe Intarahamwe wa DPWORLD unataka mjadala gani Zaid kwenye mkataba wa kimangungo Kama huu Karne ya 21, TATIZO MNATUMIKA KAMA TOILET PAPER KWENYE MASUALA YA MSINGI, Watetezi wa rasilimali wanaitwaje waharibu mjadala, foolish.
 
Ukikosa hoja unakuja na huu upuuzi wa bandari kupewa waarabu. Stupid and childish argument.

DPW wana miliki bandari mbili za UK na huko pia wanataka kuwamilikisha waarabu bandari zao?.

Huu ndio ujinga wanaotumia kama chambo cha kuziteka akili za watu wengi huko mitaani. DPW wamewekeza kwenye bandari zaidi ya 30 duniani na huko kote wanazo akili za kibaguzi na kipuuzi kama hizi za mpendwa Anita?.
Kwa mkataba kama huu??
 
Kichwa chako kina matatizo
Wewe unaona ni Sawa kabisa MTU WA bara kutoruhusiwa kuwa kiongozi Zenj Wala kumiliki ardhi zenji lakini MTU WA zenji bara anakuwa na sifa Hizo hyo Kwako ni Sawa kabisa?
Aboud Jumbe rais wa awamu ya pili Zanzibar kuna taarifa zinakinzana, wapo wanaosema alizaliwa Mpitimbi - Ruvuma, na taarifa rasmi za kiserikali zinasema alizaliwa Zanzibar.

Mwinyi Seneior Raisi wa awamu ya Tatu Zanzibar amezaliwa Mkuranga hakuna anaepinga hili.

Mwinyi Junior ameanzia siasa kwao akiwa mbunge wa Mkuranga, sasa ni Raisi wa Zanzibar.

Mbali mawaziri kuanzia Mapuri (kutoka Tabora), Mwakanjuki (Kutoka Mbeya), na wengineo. Almost kila awamu Zanzibar ina at least waziri mmoja kutoka Tanganyika.

Hata sasa wapo viongozi wa chama na serikali kwenye serikali ya Mwinyi wanaotoka Tanganyika, mfano Zena Ahmed Said, Suzan Kunambi, Joseph John Kilangi, Charles Hillary, bila kumsahau First lady.

Kwenye chama ndio watupu, almost kila mkoa wapo.
 
Sio kubagua ubaguzi upo kwa wazanzibari kamili hata katiba yao ipo hivyo wana Urania Pacha so hawana uchungu kwa Watanganyika na kibaya maisha yao yote wanasema Watanganyika wanawanyima haki zao.. and Chao ni chao na chetu ni Chao pia.. what is this?
 
Heshima kwenu Wakuu,

Majamaa tajwa hapo juu yawezekana kuwa wamelipwa rushwa kubwa sana na mamlaka za juu ili waharibu mjadala wa kitaifa juu ya uwekezaji wa DP WORLD katika bandari ya Dar es Salaam.

Hili limetokana na ukweli kwamba mara tu mjadala ulipoanza watu hawa walikimbilia kushambulia watu na kukandia asili zao badala ya kujadili hoja iliyopo mezani.

Wengine kama Nshalla walienda mbali mpaka wakafikia kumutukana Rais matusi mabaya kabisa.

Hawa wameonekana dhahiri kutumiwa na Serikali kuharibu mjadala kwa sababu za wazi zifuatazo:
1. Huwezi ukamtukana Rais halafu tena watu wakazingatia unachokiongea badala yake kila mtu ataamka na kumlinda huku akipuuza unachosema.

2. Kuwabagua wazanzibar na kuonesha kuwa hawana haki ya kusimamia mambo ya nchi wawapo viongozi. Hapa Mbowe, Mwabukusi na Lissu wameonesha dhahiri kuwa wamekula mlungula wa kutosha ili wajifanye wanawashambulia wazanzibar kisha watu wasimame kuwatetea na agenda ya msingi isahaulike.

Hawa jamaa wameharibu kila kitu na watajibu siku ya kiama kwa kukubali kutumiwa ili kuwasahaulisha watu agenda muhimu na nyeti.
Kasema jana wanafadhiliwa na kikundi kinajiita SAUTI YA WA TANZANIA ni jukumu la usalama wa Taifa kuwajuwa kina nani hawa na wanataka nini? Bandari wanatumia kama kisababu tu ila wana agenda kubwa zaidi ya hii. Kama umewasikia wameanza ku post hatutaki kupewa hadhi maalumu tunataka uraia pacha na jana Dr Slaa kaongelea hili kulipa bill. Haya mambo zaidi ya bandarim kuna watu wanatafuta balaa nchi hii.
 
Kwani nani amekataa hao DP World wataleta ufanisi,na kuingiza hizo hela....kinachopingwa hapa ni aina ya hayo makubaliano.....mnajitoa ufahamu tu,eti kama angekuja mhindi acha kulamba matako watu wa nje,,,,,kwa nini hufikirii kama sisi wamatumbi tuna uwezo huo wa kuendesha bandari zetu?????........huna ushahidi akina lissu wanatumika nyamaza!
Mmatumbi ni mwizi tu pale bandarini, kila kukicha anachora michoro ya kudokoa kisicho cha kwake.

Mmatumbi hana nidhamu ya kazi na hachelewi kuleta kujuana na ukabila kazini.

Ushahidi ni aina ya ubishi wanaouleta katika mijadala yao na aina ya upotoshaji wanaoutumia katika kujenga hoja zao.
 
Ulishaona mkataba usiooonyesha ukomo?
Mkataba unaosema eti hâta iweje mkataba hautavumjika,mkataba hauonyeshi tutapataje faida,mkataba unaosema eti bandari zote Ktk maziwa yote na hâta dry port eti vyote vitakuwa chini ya waarabu,et ukitaka kuendeleza bandari yoyote umtaarifu yéyé mwarabu kwanza Kuna mkataba duniani uliouona unafanana hvyo? Acha utahira wewe mla urojo WA MAKUNDUCHI
Ukomo upo kwenye hii mikataba ya utendaji itakayosainiwa baada ya kuwa azimio limeshapitishwa bungeni.

Zinavunjika ndoa zilizodumu kwa miaka zaidi ya hamsini sembuse mikataba ya kibiashara!.

Kwanini ufikirie masuala hasi badala ya kutazama unakwenda kupata nini kwenye huo mkataba?.
 
Mmatumbi ni mwizi tu pale bandarini, kila kukicha anachora michoro ya kudokoa kisicho cha kwake.

Mmatumbi hana nidhamu ya kazi na hachelewi kuleta kujuana na ukabila kazini.

Ushahidi ni aina ya ubishi wanaouleta katika mijadala yao na aina ya upotoshaji wanaoutumia katika kujenga hoja zao.
Upotoshaji upi wamefanya, weka ushahidi…

Mmatumbi ni wote ambao hawana nidhamu ya kazi na ni wezi?? Hii ndio enough reason au justification waarabu wapewe bandari yetu milele??? Hujitambui , wewe ndio unatumika
 
Taratiibu unahama kutoka kwenye mada na kuanza kutoa mapovu.
 
Ni sawa, lakini hoja inabidi zijibiwe...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom