Hawa uliowataja ni mawakala wa wazungu wenyewe wenye kuchukia wanapoona tunataka kufaidika na bandari kwa asilimia mia moja.
Wengi wa hawa wanasheria ni watu wanaolipwa baada ya kuongea mbele ya waandishi wa habari hivyo ni silaha muhimu ya siri ya wenye pesa katika vita dhidi ya mipango ya serikali.
Rais Samia unaweza kumuona mpole lakini yupo kimkakatia sana kuliko hawa wanasiasa wapiga kelele wanavyomchukulia.
Hawa wapiga kelele wanawafanyia jambo baya sana wadau halisi wa bandari ambao wanaunga mkono mia kwa mia uwekezaji huu.
Kuna hizi ICD yaani container depot ni sehemu ya kuhifadhi mizigo zilizobuniwa katika awamu ya nne na ya tatu, ambazo kwa kiasi kikubwa ni mali za mawaziri na mabosi wengine wa serikalini, hawa watapinga uwekezaji wa DPW.
Akija huyu mwekezaji kutakuwa hakuna sababu ya mzigo kuhifadhiwa kwenye yard ya mtu eti ukisubiri kwenda kupakiwa melini, hizi foleni zilizotengenezwa ndizo zinazowapa ulaji wafanyabiashara wachache wa mijini, ni upumbavu mtupu unaoendelea pale TPA.
Mitambo ya kisasa itapakua na kupakia mzigo wa melini kwa haraka zaidi na ufanisi utakaokuwepo utawafanya wafanyabiashara wafikirie masuala mengine kwenye huo muda wanaotumia kufikiria kutoa au kuingiza makontena bandarini.
Kundi la wanaopinga uwekezaji linawatumia hawa wanasiasa wenye kuheshimiwa mbele ya umma kwa ajili ya kujenga hofu na picha hasi juu ya kinachotaka kufanyika lakini mwisho wao umeshakaribia.