Mwaka 2015 ilikuwa UKAWA vs MAGUFULI, mwaka 2025 itakuwa CCM vs Wananchi na kivuli cha Magufuli

Mwaka 2015 ilikuwa UKAWA vs MAGUFULI, mwaka 2025 itakuwa CCM vs Wananchi na kivuli cha Magufuli

Magufuli kimsimamo namfananisha na Rais wa Misri alietokana na Wanyonge Mohamed Mursi

Alipochaguliwa Mafisadi ya Egypt yaliyojazana Jeshini yakiongozwa na Generali Abdilfatah Alsisi yakishirikiana na Mabeberu yalidhan yanaweza kumshawishi alegeze misimamo yake ya kutetea Raia

Yalivyoshindwa kumuangusha yakakusanya majeshi kumtisha alegeze Msimamo akakataa wakamtoa na wakamfunga lakini akiwa Gerezani msimamo wake ukabaki vile vile hadi akauwawa akiwa Kizimbani kwa sumu wakadai eti Matatizo ya Umeme wa Moyo.
Duuh! Kwa hiyo na Magu aliuawa?
 
Mitandaoni Magufuli ni Rais wa hovyo kuwahi kutokea nchi hii.

Kitaani Magufuli ni shujaa watu wanampenda mpaka sifa nyingine wanamuongezea.

Ile suprise waliyoona watu wa mitandaoni wakati wa msiba wa Magufuli tuombe Mungu isije kujirudia kwenye chaguzi against yoyote anaesema tofauti juu ya Magufuli.

Inawezekana Magufuli aliletwa kuanzisha siasa mpya kwenye nchi. Tunayoyaona mtaani yanaeleza lugha fulani ambayo unaweza kuwa mkaidi kuikubali ila wakati siku zote ndio msema kweli.
Kabisa mkuu,umenena sana
 
Amani iwe kwenu,

Mimi kama mwananchi na mwanaCCM nakumbuka ilivyokuwa ngumu kuiuza CCM mwaka 2015 kiasi ambacho hata wafanyakazi wa CCM waliogopa kuvaa sare za chama hata walipokuwa ofisi za Lumumba kwa kuhofia kipigo na fedheha toka kwa wananchi.

Naam, kazi kubwa ilifanyika hadi kutafuta washauri nguli ambao walitushauri tukiwa majukwaani tujinadi kama chama cha Magufuli na sio CCM.

Kuna kila dalili mwaka 2025 na kuendelea ni dhahiri CCM itaenda kwenye uchaguzi dhidi ya wananchi na hapo siku zijazo itabidi kumtafuta Magufuli mwingine kunusuru chama.

Ajizi nyumba ya njaa!


Tunapenda kudakia vitu. Bila tume huru tusije kufikiria mambo yatakuwa kama zamani Chadema haitashiriki bila tume huru huo ndiyo ukweli. Hii ni 30%~40% ya wapiga kura!. Labda hata idadi ya wapiga kura watapeli!
 
Unajua hali ya mtaani ni tofauti kabisa na wanavyozani ccm watu wamewachoka
 
Tusidanganyane, Magufuli angekuwa anakubalika asingeiba uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wote wa 2020. Magufuli aliwekwa na NEC na Police kuwa Rais mwaka 2020.

Acheni kumtukuza Mwendazake ambaye alikuwa mwizi, MWONGO na dikteta aliyetaka kuiharibu Nchi yetu.

CCM wakishindwa mwaka 2025 watashindwa kama chama tu na siyo huyo wenu tuliyemzika Chato
Nani wa kuishinda CCM 2025 wakati hata wapinzani wanashangilia Kinana na wajanja wa bao la mkono kurudi?
 
Magufuli kimsimamo namfananisha na Rais wa Misri alietokana na Wanyonge Mohamed Mursi

Alipochaguliwa Mafisadi ya Egypt yaliyojazana Jeshini yakiongozwa na Generali Abdilfatah Alsisi yakishirikiana na Mabeberu yalidhan yanaweza kumshawishi alegeze misimamo yake ya kutetea Raia

Yalivyoshindwa kumuangusha yakakusanya majeshi kumtisha alegeze Msimamo akakataa wakamtoa na wakamfunga lakini akiwa Gerezani msimamo wake ukabaki vile vile hadi akauwawa akiwa Kizimbani kwa sumu wakadai eti Matatizo ya Umeme wa Moyo.
Aiseh wewe ni wa kuandika hv kweli!!!?we si timu Born town wewe!!!?au?
 
Magufuli alikuwa na misimamo yake tata na haikueleweka na kundi la elites.

Ila kundi la watu wa kawaida walipenda misimamo yake na falsafa zake.

Sasa hapa kuna makundi mawili la hao elites ambalo utalikuta twitter na JF likitema nyongo.

Na lingine la watu wa kawaida awa wanajadili kwenye daladala, vijiweni nk

Awa elites wapo kama laki 8 kati ya watanzania million 60.

Hizi namba kwa mwenye akili hawezi kupuuza awa wanyonge.
Hata laki nanae hawafiki hao
 
Magufuli alijuwa Tanzania Ina illiterates wengi na akawafanya mtaji. Akazima vyombo huru vya habari na akabakia yeye tu ndiye sauti kupitia TBC na channel 10.
Propaganda zake tu za uwongo ndizo zilitawala kwa miaka 5, ndiyo maana wewe sinza pazuri unaona kama watu wanamkubali.

Tutaendelea kuwasomesha Polepole mpaka waelewe kuwa Magufuli was a mediocre leader but a ruthless dictator
Jitoe ufahamu subiri hiyo 2025 ndio utajua hujui.
 
Tokea lini CCM inategemea kura yako, kama ungekuwa na uwezo wa kuamua si ungebadili katiba au hata kuandamana, SAMIA RAIS WA LEO NA KESHO, acha ubwege.
Mtaingia Ikulu lakini mtagawana wabunge na vyama vya upinzani. Subiri uone !
 
Kwani kwa akili yako Maccm yaliwahi shinda uchaguzi wowote tangu 2010?
Wanashinda sana tu. Kwa nini wasishinde iwapo wapinzani wenyewe hawa wa kubadili gia anagani ? Hivi sasa hata kujua wapinzani wanajipanga vipi haileweki halafu wakija kushindwa wanaanza ooh tumeibiwa ! Hovyo kabisa.
 
Adolph Hitler mwenyewe anayelaaniwa kwa kuanzisha vita vya pili vya Dunia anaenziwa kila mwaka huko Germany. Lakini bado haimfanyi kuwa kiongozi mzuri.

Kuhusu kumchafua Magufuli, huo ni uongo. Alijichafua mwenyewe kwa kumiliki kikundi cha WASIOJULIKAMA, kuua wakosoaji, kutugawa watanzania kiitikadi na kikabila.

Muache aendelee kuoza huko ahera
Hata wewe utakufa tu kwani utaishi milele ?
 
Angekuwa amefanya makubwa hivyo asingenajisi uchaguzi wa 2020. Yeye mwenyewe akiwa hai ilibidi anajisi uchaguzi. Kama alikuwa anakubalika hivyo huko mtaani angeheshimu box la kura.
Huo mwaka 2020 nani angeitoa CCM madarakani ?
 
Magufuli is no more, kuongelea mambo ya 2025 sasa hivi sio sahihi, kumbuka siasa hubadilika muda wowote na mpaka kufika mwaka huo mengi yatakuwa yameshatokea kubadili upepo.
Hujui kitu 2025 siyo mbali kwa hali inavyoenda subiri mtanange
 
Mkuu, na usisahau humu JF ni kama tawi dogo la Chadema ambapo kila kitu kihusucho mazuri ya JPM basi watapinga na kutukana

Ila kiuhalisia mtaani huko ni habari nyingne kabisa JPM ni Rais aliyetokea kukubalika sana nchini
Hata likiwa ni Tawi la CHADEMA wataishia kutukana humu na Ikulu hawaingii kamwe
 
Tunapenda kudakia vitu. Bila tume huru tusije kufikiria mambo yatakuwa kama zamani Chadema haitashiriki bila tume huru huo ndiyo ukweli. Hii ni 30%~40% ya wapiga kura!. Labda hata idadi ya wapiga kura watapeli!
Kwani CHADEMA bado ipo ?
 
Umeandika kilichoko mitaani mkuu,

Mimi mwenyewe CCM ila CCM iliyopo sasa bila Kumpata mwenye kuendana na JPM, kura yangu siwapi hao wezi waliopo sasa!
 
Upo sahihi kabisa. Cha ajabu ni kwamba, CCM wameshasahau hayo yote, wanadiriki hata kumdhihaki JPM. CCM ilikosa kabisa kibali machoni pa Watanzania lakini JPM binafsi ndo aliyekiheshimisha tena chama kwa Watanzania.
Rai yangu, CCM wasilewe madaraka wakafikia hatua ya kupuuza kazi za JPM.
Wataangukia pua si muda mrefu sana.
 
Back
Top Bottom