Kivipi wanamtandao walihusika na umafia? Watajwe tu ili ukweli ujulikane ni nani wanahusika kupanga mauaji, sio kukwepesha ukweli wakati hata mbulula wa chini ya mtu anaweza ku sense aliyepanga jaribio la kumua TAL ni nani. Muachage propaganda
..mtoa mada ama ni mjinga kupindukia, au anadhani sisi ni wajinga.
..tuchukulie mfano wa ndege zetu kushikiliwa kutokana na serikali kutokulipa madeni au kuvunja mkataba.
..Je, mabeberu tulioingia nao mikataba wanahitaji msaada, au nyaraka zozote, toka serikalini ili watushitaki?
..Kwanza si serikali iliitangazia dunia kwamba imenunua ndege tena CASH? Sasa huko si kujichongea wenyewe kwa wote wanaoidai serikali?
..Pili makampuni yaliyotupeleka mahakamani ni yale tuliyoingia nayo mikataba. Na walitushtaki kwa madai kwamba tumevunja mikataba.
..Je, kampuni tuliyoingia nayo mkataba si tayari inao mkataba tuliosaini nao? Na kutupeleka mahakamani si suala la wao kutumia nyaraka ambazo tayari wanazo tangu wakati wanasainishana na serikali?
..Mabeberu hawahitaji msaada wowote ule toka Tanzania ili kuweza kuiburuza serikali yetu katika mahakama za usuluhishi zilizoko katika nchi zao. Kwanza hata wanasheria wanaofungua kesi hizo wako katika nchi hizohizo.
..Ni ujinga kuamini kwamba mabeberu waliwahitaji wanamtandao, au Mtanzania yeyote, ili kuwezeshwa kufungua kesi dhidi ya Tanzania.