econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Mimi ni shahidi wa kuwa huyu Shangazi anajitahidi sana sana kwenye kazi zake, labda tu kuna watu wanampiga vita kwa mambo yao. Huyu Shangazi hanijui, simjui, ila mwaka jana alitusaidia sana mimi na familia yangu. Mama yangu alikuwa anashida ya figo, tukamtafuta, alihakikisha tunapata msaada wa kipekee sana. Na wala hatujui, maskini ya Mungu.
Huduma ya afya Tanzania ni pana sana kusema umbebeshe lawama Waziri. Hii Wizara inahitaji efforts za watu wengi hasa Rais mwenyewe. Huku panahitaji budget kubwa sana, ila na sisi nchi ni maskini, na bado vipaumbele vya serikali havieleweki (kwa muda mrefu hatujaweka afya kama kipaumbele). Yeye kama waziri mwenye dhamana, kazi anaifanya sana tu.
Sawa Ummy tumekusikia. Usitumie nguvu nyingi kujisafisha fanya kazi kwa ubora.