Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Hakika!!
 
Ni mwaka wa mafunzo baada ya kupita katika bonde la mauti na ilibaki kidogo tuu nifike mwisho kama siyo simu ya yule dogo niliempokea kazini akitokea mtwala. Sasa nina mtazamo tofauti kabsa na dunia hii hakuna kitu kisichokua na mwisho kikubwa ni kuwa postive muda wote na ikimpendeza Mungu mwezi wa 12 nitaungana tena na familia japo kwa wiki mbili
 
Huu mwaka umenifanya niamini kila kitu kinawezekana... nimefanya mambo makubwa ambayo kwa umri wangu sikudhani kama naweza kufanya....Mafanikio ya kila mtu yapo mikononi mwake kwakweli, ni suala la kumwomba Mungu na kuamua kufanya
Tugawane hayo mafanikio.

Kwangu naona kama sijafanya makubwa , Malengo hayajatimia kwa 60%. Najipa moyo mda bado upo? NAAMINI MUNGU ANAWEZA KUTOA HATA KAMA YAMEBAKI MASAA KUMALIZA MWAKA.
 
Hakika
 
Wakuu

Najua tuna mambo mengi yanayotusibu kwenye harakati za kila siku kutafuta mkate.

Leo ikiwa ni tarehe 13 December kuna kitu/vitu ulitamani kufanikisha lakini unaona vimeshindikana au hujafikia matarajio tupeane uzoefu.

Naamini tuna mengi ya kujifunza as long as bado tunaendelea kupambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…