ndio, kwasababu nafafanuliwa na Roho Mtakatifu. ninyi mnasoma seminary hadi vyuo lakini mnasoma kama masomo mengine tu na Roho Mtakatifu hahusiki, hamna Mungu ndio maana hata mapepo mnayaogopa. nikupe mfano huu, ili uamue dini ya kweli ni ipi.
Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alipita akihubiri, akitoa pepo na kuponya wagonjwa. akasema, "mtu aniaminiye mimi kazi nizifanyazo atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi". baada tu ya kupaa na Roho Mtakatifu kuwashukia wanafunzi wake, walianza kuhubiri na walifanya kazi zoote alizozifanya Yesu za kuponya wagonjwa kutoa pepo, kufufua wafu n.k. hadi leo wapo watu wa Mungu wanaotoa pepo, wanafukuza mashetani, wanaponya wagonjwa na kufufua wafu n.k, wananena kwa lugha.
lakini wakatoliki pamoja na kusoma dini sana, hawana nguvu ya Mungu kutoa pepo hata kinyamkera tu, hawajazwi Roho Mtakatifu. ulishawahi kuona padri hata askofu tu ameombea mtu akatoka pepo? hata papa tu uliwahi kusikia ameweka mikono juu ya mgonjwa akapata afya? kuwa mkweli, wapi uliwahi kuona? je? dini halisi ambayo ndiyo Yesu alielekeza ile watu wanaongozwa na Roho Mtakatifu wakanena ka Lugha mpya na kuweka mikono juu ya wagonjwa wapate afya, ni ipi? ya wakatoliki?