Mwakani nitaanza kuishi na wadogo zangu naomba bajeti ya chakula

Mwakani nitaanza kuishi na wadogo zangu naomba bajeti ya chakula

Kumbe wenye familia mnateseka sana... Sie mabachelor buku 4 tuu kwa siku umekula na kushiba
Kama upo single hiyo buku four ni nyingi Sana inaoneka unatumia vibaya Sana pesa Mimi Kama katibu wa UWABATA-wanaume bahili Tanzania
 
We andaa bustani, genge, matunda wawe na shughuli ya kufanya.
Hao watapigwa miti hapohapo ndani ukaletewa mimba vile vile ulee.
Mark my word
 
Kumbe wenye familia mnateseka sana... Sie mabachelor buku 4 tuu kwa siku umekula na kushiba
Ef4 mbona kubwa sana.
Ukiwa na kila kitu elfu 4 inabaki.

Sema wanaume ni wavivu kupika
Mnapenda kununua chakula


Kwa sisi wadada
Mimi nikinunua vitu vyangu vyote zinapita siku situmii hata sh mia.
 
Kila kitu kipo 10,000 ya nini tena?
Unanunua nyama, let say kilo moja unatoa 10000, mimi ni mchaga ukipika ndizi, lazima ununue sio chini ya elfu 4, hapo hujaweka utumbo ambao ni luxury

Sometimes ukila kande, watoto wanapikiwa vyakula vyao.

Asubuhi lazima ununue vitafuniwa - wanangu wanakula kama mchwa tena mwanangu wa kiume anapiga mara saba kwa siku, akishiba anachezea dude.

Watoto wanakula vitu vya ziada, kama maziwa, mayai etc for their health benefits

Kwa wiki kila siku kinapikwa chakula chake, naonaga watu wengi wanakula Wali na ugali tu.
 
Subiri uanze kuishi nao utajiona tu umeanza kulima matembele nyuma ya nyumba bila kushauriwa, unalima mahindi na mambo kama hayo
 
Unanunua nyama, let say kilo moja unatoa 10000, mimi ni mchaga ukipika ndizi, lazima ununue sio chini ya elfu 4, hapo hujaweka utumbo ambao ni luxury

Sometimes ukila kande, watoto wanapikiwa vyakula vyao.

Asubuhi lazima ununue vitafuniwa - wanangu wanakula kama mchwa tena mwanangu wa kiume anapiga mara saba kwa siku, akishiba anachezea dude.

Watoto wanakula vitu vya ziada, kama maziwa, mayai etc for their health benefits

Kwa wiki kila siku kinapikwa chakula chake, naonaga watu wengi wanakula Wali na ugali tu.
Vitafunwa nunua unga , nyama,mayai
Vinatayarishwa nyumbani.
Chapati,maandazi,bajia,sambusa,mkate.
Mayai Trey zima linatoboa wiki
Soseji pakti kadhaa.
Unakuwa unamix hapo.

Kama vitafunwa lazima hela iende sana.
Vitafunwa vinamaliza hela.
 
Mwwkani ni mbali rafiki... Subiri ukibaki mwezi mmoja ndipo tutakushauri
 
Vitafunwa nunua unga , nyama,mayai
Vinatayarishwa nyumbani.
Chapati,maandazi,bajia,sambusa,mkate.
Mayai Trey zima linatoboa wiki
Soseji pakti kadhaa.
Unakuwa unamix hapo.

Kama vitafunwa lazima hela iende sana.
Vitafunwa vinamaliza hela.
Vitafunwa sinunui barabarani sijawah toka nizaliwe

Mke wangu anatengeneza pancakes, cakes, mikate, nk nyumbani.

Gharama zangu ziko hivyo tu najaribu kupangilia ila ziko palepale

Siku ambayo kumepikwq wali, ndio siku pekee ambayo nimepika bila gahrama kubwa. Hapo inanunuliwa nazi na mboga za majani tu.
 
Back
Top Bottom