Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Wa zamani sio siku hizi.
Graduate anavuta sio chini ya laki 8 akiwa na masters anavuta 1.8.
Ukipata Kazi ya ualimu omba vijijini life is simple Hakuna kufatiliana baada ya Kazi piga ujasilimali.
Timiza wajibu wako wasome wasisome shauri yao na wazazi wao ukijifanya unawafatilia fatilia Ili wasome watakuroga.
Anaetaka kusoma mpe ushirikiano.
Wikiendi kuwa bize kwenye mishe zako.
 
Huyo Mwalimu ni sahihi alivyotendwa KILA Kazi Ina taratibu zake ukiacha wengine wanajaza nafasi.
Pia KILA mmoja anayo njia yake ya kutoka afanye ubarmaid kwa malengo Ili aje amiliki bar mbeleni.
 
Watanzania wengi tunapenda sana kukopakopa bila sababu maalum! Sanasana sababu ya ufahari.

Unakopa gari Harrier, mshahara hauzidi tshs 1m, unategemea nini?

Hapo ndiyo wiziwizi mpaka kwenye kahela ka chai!
 
Ni elfu thelathini na nne(34000).Mr.Ban huyu mwalimu ni graduate, ana degree kutoka UDSM.
Atunukiwe medali ya ushujaa wa kuishi kwa Sh. 1133.33 kwa mwezi na kuweza kukidhi mahitaji yake yote
 
huo mshahara mbona ni mkubwa sana kwa wenye masters na degree wasio na ajira wanaopuyanga mitaani.

Angetuliza tuu matako hapohapo.
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Madeni aliyatengeneza kwa kuzingatia kipo chanzo cha kipato ambacho ni mshahara kutokana na kazi yake ya ualimu kama alikosa nidhamu wangefanyeje.....TSC walimpatia adhabu ya kumshusha cheo baada ya maonyo kadhaa pia kwa kuzingatia maadili ya viongozi/watumishi wa Umma....watanzania tusiwe wanaharakati kwa kila jambo tuziache mamlaka zifanye kazi zake..

Sent from my EVA-L19 using JamiiForums mobile app
 
Ina Maana huo mshahara anakatwa zaidi ya moja ya tatu???hata kama adhabu ya makato ya nusu mshahara haiwezi kufika 34000|= kwa mfumo wa moja ya tatu!!
Taasisi za mikopo zipo nyingi na haziko integrated, mkopaji kila eneo huchukua kwa wakati wake. Kuitekeleza sheria ya kuachiwa β…“ ya mshahara inakuwa ngumu.
 
Hii stori ni ya kufikirika na haina hata chembe ya uhalisia. Nahisi ina lengo tu la kuwajaza watu upepo ili watokwe na mapovu!

Naomba niwe tu wa mwisho kuiamini. Maana ina maswali mengi kuliko majibu.
 
Elfu 34 tu, mbona hatari, mimi na net ya 4.6m bado haitoshi.
 
baadae atakapopata kazi nyingine serikalini kurejea kwenye utumishi ndo atajua hajui yaani. mchalato ni mgumu sanaaa. Ila hii ngozi nyeusi tuko na roho mbaya sana tunafikiria zaidi kukwamishana kuliko kusaidiana
Data base ya watumishi wa umma ni moja.
Unapotoroka kazi, kupata kazi labda ughushi kila kitu, jambo ambalo ni gumu.

Ukiona mtumishi anatoroka, elewa katamani ujasiria mali ama kazi za mashirika binafsi.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mwalimu bhanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ halafu 2025 utamkuta anabebana na masanduku ya kura za wizi ili aisaidie ccm ipate ushindi.
 
Ushauri Bora kabisa huu wa mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…