Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Uko sahihi sana Mkuu...
 
Huyo ndo mama samia anayeabudiwa na akina Lucas mwashambwa ChoiceVariable na chawa wenzao.

Hivyo ndivyo anavyotatua matatizo yake. Amri na imla
 
Kwa hiyo kama Waziri anajipa mamlaka ya kufanya atakavyo. Tuna rais wa nini sasa?

Nikiwaambia tuna rais dhaifu mno wala sikosei. Maelezo yako yamethibitisha yenyewe
 
yeye si hodari sana, si mwamba sana, tunachoomba asijinyonge tu kwa stress, lakini Lazima ashike adabu na anyooke vizur, huu ni mwanzo tu, atapata tabu sana kwenye mafao
Mafao ya wapi sasa?

Kama hataki uteuzi wa bibi yenu huyo na kama hataki kurudi kazini huko Temeke kuendelea kula vumbi la chaki maana yake hata hayo mafao chukueni, yupo tayari na amejiandaa kwa hilo..

Unafikiri yeye ni kama wewe ambaye ili mkono uende kinywani na watoto waende chooni ni mpaka ulambe miguu ya maboss wako hapo Lumumba..?

CWT ni taasisi huru isiyofungamana moja kwa moja na serikali. Kama ameamua kufanya kazi na CWT, let him go na hao ndio watamlipa mafao yake..!
 
Kwani hizo pesa za bwerere pale CWT ambazo serikali inataka Kwenda kuzichota ni za nani hasa?Maganga au serikali?maana nimeshtuka sana kwamba kumbe CWT kuna pesa za bwerere, kumbe basi ndio maana hata akina Janeth Maganga wamegomea teuzi kwa maana watakua wameondolewa kwenye mzinga wa asali ya bwerere,maana CWT ni sehemu Salama sana ya kujichotea fedha za walimu za bwerere.WALIMU KWELI FEDHA ZENU ZINATAFUNWA NA WAJANJA WACHACHE.VP HABARI YA KUAMKA KWA WALIMU,Sijui tuwaachie walimu wenyewe.
 
Huyo Janeth anataka Ofisi ya menejimenti ya utumishi wa umma imsikilize yy kama ilivyofanya toka barua ya kwanza ila yeye hayupo tayari kuisikiliza ofisi kuu ya Utumishi.
 
umeazimwa mara ya kwanza umekubaliwa, umeazimwa mara ya pili umekubaliwa, mara ya tatu umekataliwa ndio imekua nongwa?
Kwanini wakati huu alipokataa UCHAWA ndipo anyimwe ruhusa wakati miaka ya nyuma alikuwa anaongezewa muda bila kikwazo? Huoni kwamba kuna walakini hapo?
 

nanaliu, si usemezane kwa polepole, fujo la nini sasa unileta huku

kwaihiyo huyo mujamaa yako, asingalikua Mwalimu, angelikua na sifa ya kua katibu mkuu wa CWT right?

ngoja nitumie na lugha hii labda utanielewa,

Msingi wa kua katibu mkuu wa CWT si ni Lazima uwe mwalimu?

na uhuru wa CWT uko upande gani au nayo ni kama chadema na ACT?
 
kweli humu Duniani kuna watu na viatu,
akiomba yeye ni sharti apewe tu eti ndio haki na hana shukran wala heshima kwa mamlaka, akiombwa yeye sasa, mabega juu hataki tena kwa mikogo kama yote,
akinyimwa sasa ilo shavu linavyofura kama chatu kameza sungura 🤓

sasa mtu kama huyu aliejaa uchoyo, tamaa na kiburi, aisee acha niishie hapo....
Huyo Janeth anataka Ofisi ya menejimenti ya utumishi wa umma imsikilize yy kama ilivyofanya toka barua ya kwanza ila yeye hayupo tayari kuisikiliza ofisi kuu ya Utumishi.
 
Tumeambiwa aliomba kibali Utumishi,sasa mm na ww tujiulize Hv kibali huwa hakiishi ,mm naamini kibali kinaisha kulingana na muda uliopewa.JANETH hakuajiriwa CWT,waliomuajiri ndio walimpa kibali pale alipoomba kutumikia CWT,Kumbuka mwajiri mkuu ni serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na CWT sio mwajiri na kuigomea serikali iliyokupa kibali kwenda huko uliko ni kosa lingine,kama kibali kimeisha muda wake basi turudi tulipotokea ndio busara kuliko kuwa na kiburi kisicho na maana.Angeenda kutumikia CWT bila kibali kutoka Ofisi ya Utumishi kwa muda wote ambao amekuwa huko,ningewashangaa sana Utumishi kumtaka arudi kule alikokuwa ilhali hawakumuandikia kibali.Ni vema tukazingatia taratibu za Utumishi na tusi sikilize bush loyals ambao mwisho wa siku hawana cha kutusaidia.
 
Mkuu huo mfuko wa sementi unaupoteza wewe mwenyewe kwa sababu ya kutojua haki zako. Hebu fanya hima umwandikie barua mwajiri wako ujitoe CWT. Hiki ni chama cha hiyari, mtu halazimishwi kujiunga au kuungwa kwa nguvu. CWT wanakata pesa zako isivyo halali na ukikomaa mahakamani watazitapika hela zote walizokukata tangu ulipoajiriwa. Hawa watu ni wahuni tu hawana lolote. Hebu soma document hii upate mwangaza kuhusu haki na wajibu wako wa kujiunga au kutojiunga na chama chochote. Pitia document hii ujielimishe.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…