DOKEZO Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Daniel Ole Njoolay, amewafukuza wanafunzi Kidato cha 4 kwa kutotoa Tsh 70,000 ya kambi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama ni makubaliano toeni hizo pesa ili shughuli ziende ,hizi siasa zinawafanya kuwa wajinga .Toeni pesa mambo yaende
Mzazi aina yako ndiyo chanzo cha watawala ku presume kwamba wananchi wote ni mabogus.

Ada ya elfu 20 tu kwa mwaka iliwashinda wazazi wengi hadi kufikia mahali watoto wamefaulu ila wameshindwa kujiunga na sekondari kwa kukosa ada hiyo ndiyo serikali ikafanya tathimini na kuja na wazo la kufuta ada zote ili watoto wote waweze kupata haki ya elimu.

Sasa kama ada ya elfu 20 kwa mwaka mzima imemshinda mzazi vipi kuhusu 70,000 ambayo anailipa ndani ya mwezi ama miezi miwili anaitoa wapi?

Uwe unafikiria pande zote kabla ya kuja na hoja zako mkuu.
 
Alf unakuta waalimu hawaudhurii na washamaliza Topic
 
Sasa mtu kama hawezi kumudu elfu 70 kwanini anazaa?
Wazo la watoto kukaa kambini to me is good ides .

Naona watu wanapinga tu Ila hawajui kuwa kizazi chao kilikuwa well protected with less destruction.

But I Feel sorry kizazi cha Leo mazingira sio friendly Sana mtaani mtoto anapokuwa anajiandaa na mitihani Kama form four anabidi kuandaliwa mazingira mazuri Sana .
 
wanakosa busara
Yani mwanafunzi asisome kisa kambi🤔
Aisee
Inaumiza mno kama mzazi aise.

Yaani mtoto akose haki ya elimu kisa mchango usiokuwa na kichwa wala miguu?

Nawashauri wazazi wenye watoto wao waji organize waende kumweleza ukweli huyo mwalimu kwamba mchango ni hiyari sio lazima kwakuwa hakuna mahali popote kwenye sheria,kanuni wala muongozo wa elimu ulipotaja suala la michango kama ni suala la lazima.
 
Inasikitisha sana mkuu yaani una imagine huyo ni mkuu wa shule alivyo mweupe kichwani namna hiyo vipi hao walimu anaowaongoza watakuwa na hali gani?

Yaani unamuadhibu mtoto kwa kukosa mchango wakati mtoto hana vyanzo vya mapato anamtegemea mzazi.
 
Serikali na siasa zinawadanganya Sana.

Kama mzazi you have to be responsible Elimu ni siasa za kijinga

Mtoto wako akipata zero au akifeli that's ur burden and not government burden

Kwahiyo mnapokuwa mnapinga kila kitu na hata kile kinacholenga kuwasaidia mnakuwa mnakosea .


To me wazo la kuwaweka wanafunzi pamoja kuelekea mtihani wa mwisho ni wazo bora

Ila kuhusu kulipa hiyo 70K hapo tunabidi kuangalia both side kuona je tunafanyaje .


Kwakuwa pesa haina thamani kuzidi Elimu ambayo mtoto akiipata itamsaidia to his or her lifetime.


So tuwe makini hapo

Siasa za Elimu bure zisitufanye kuwa blindness
 
" Mana nina uhakika hakuna mwalimu hapo mwenye A ya fizikia na maths both levels" hizi diss punchlines zilishudiwa enzi za akina Tupak Shakur na Notorious B.I.G wakati huo Hiphop ipo kwenye peak...
 
Then NRNE
 
Watu hawakatai kulipa issue ziwe hizo gharama ziwe formal, sio zile mtu anaamka anasema kesho mje na ada ya fagio la mwalimu mkuu
Si kamati ya Wazazi inashirikishwa na ndio inayochambua hiyo elfu 70 itatumika vipi. Wakiridhika mchango unapitishwa kwa Kauli moja.
 
Hiyo 70K inakuwa included na Chakula if yes lipia haraka mtoto apate kuandaliwa vizuri.
Mtoto wangu hakuna Kambi asome anarud nyumbani Kambi ya kitu gani? Wanatuharibia watoto tu, hata wakisema Bure mtoto wangu Kambi haendi
 
Nakukumbuka nilivyokuwa f4 nilitolewa kwenye kipindi na kuchapwa nikafuate
kuni kuenda home mzaz alimind kwa nn nirudi kisa hicho nisisome kisa hicho

Alikuja kuhamishwa huyo mwl
 
Sk za mwisho kwa nn isiwe mwanzoni sana
Na bado kuna zero
 
Lipa gharama za mtoto wako acha kukwepa majukumu, wanaokudanganya elimu bure wao wanasomesha watoto wao kwa kulipa mamilioni ya pesa, we kutoa tu elfu 70 ili walimu wajaribu kumpa mtoto wako kilicho bora unakuja kupiga mkwara hapa.
 
Ni Bora kwani hamlipwi si mfundishe kawaida vitu ambavyo mnalipwa kwenye mishahara ?, anafaulu mtoto sio kwa hayo maprogram ya kishenzi
Kweli kabisa kamanda... ata walimu wasipofundisha watoto wote wana akili na watafauru tu
 
Kweli kabisa kamanda... ata walimu wasipofundisha watoto wote wana akili na watafauru tu
No wajinu wa walimu kufundisha sababu wanalipwa kama hizo program ni muhimu waiambie serikali izipitie na kuziingeza kwenye mfumo. Sio kutuletea chochote wanachotaKa.

Mimi Toka Shule ya MSINGI mpaka namaliza masters sajawai kufeli na hayoakozi sijawahi hudhuria
 
Hana akili
 
Ada imerudi ki wizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…