Mwalimu Nyerere na Dkt. Magufuli ndio wanaonekana marais bora, ila ndio marais wabovu kuliko wote

Nisome shule za kata ... Kikubwa Ubongo wangu ni mkubwa .


Nyinyi mlozoea Maisha ya ujanja ujanja ,uhuniuhuni, mnajiita watoto wa Mjini , very poor kichwani

Ndio mlioumizwa sana sana na utawala wa JPM.



Mimi Binafsi nafurahi kuona Kuna ALAMA ALOZIACHA JPM ,ambazo watoto wangu wanakua, nitakua nawaambia , alitokea Rais MCHAPAKAZI .



Ungekua unajituma, Miaka mitano ya JPM,, usingeiona michungu ikiwa unazungumza nje ya mwelekeo wa kisiasa.
 
Ni vigezo vipi umetumia kupima productivity? Isije ikawa alichotumwa JK na jamhuri na alichotumwa JPM na jamhuri vina muunganiko ila matokeo ya muunganiko umeanza kuyaona kwa JPM. Kwann unaamini JK hakuwa productive?
 
Utajiri umefanywa kuwa sifa mbaya na halafu umasikini umefanywa Kama ndio utakatifu vile..taifa la watu wenye hizi fikra maendeleo tutayasikia kwa hao mabeberu
 
Unapochanganya Pumba, Mawe kwenye Kamchele na bado ukaita huo ni mchele unaweza ukasababisha ulichonacho chote kionekane ni pumba wakati ungetenganisha ungebakiwa angalau na mchele kidogo...

Hapo umweka concepts mbalimbali ambazo theoretically they are incorrect...

Unavyosema matajiri je utajiri huo ni self made (kama kina bhakresa au wabunifu kama kina Gates, Jobs,) au ni utajiri wa kama kina Abramavich na wengine wanaopiga deals na kujigawia commanding heights of the country economy (natural resources) na kuzifanya ni za kwao binafsi kwa manufaa yao na hivyo kuwanyonya wengine ?; Au ni utajiri kama kina Edison waliopata vingi kutokana na their business acumen wakati kina Tesla waliongundua hayo mengi na kuwatajirisha wengine hawakupata kama wao kutokana na their inferior business skills ?

Kama babu yangu alikuwa chifu je ni sawa ule mto unaopita kwenye ule mlima niseme ni wangu na kila atakaye kunywa maji lazima anilipe ? Nadhani hio ni tofauti kama nikija na formula ya kutengeneza maji ambayo kila atakaye anaweza kunywa kwa gharama ninayotaka mimi.

Kufupisha maneno marefu modes of production changes with time...., na ile so called socialism was never socialism bali capitalists (wachache / wanyonyaji) living in socialist clothes; kwasababu ya production was inefficient wachache walijinufaisha kwa jasho la wengi....., Pili hata hivi sasa hakuna a pure capitalistic au socialistic country labda kwenye vitabu (zote ni mixed economies), China is doing fine industrial wise na its a country with market socialism...

Tatu even capitalism as we know it hivi sasa itaendelea na kuja kubadilika kutokana na mahitaji, teknolojia na scarcity ya resources...., (its a time bomb wakati wewe una kila kitu alafu umezungukwa na watu wasio na chochote) huwezi ukawa unamiliki ziwa alafu kuna watu hawa hata chemichemi ya kunywa maji alafu ukadhani watakuangalia tu sababu kuna ka-mkataba kanakosema bibi yako alinunua lile ziwa....
 
Saalam! Carlos
Kutanguliza neno mpumbavu halitofanya nisikujibu ulichoandika
Kila binadamu ana makosa na hujifunza kulingana na makosa hivyo hata JPM alikuwa na mapungufu yake kosa kubwa ninaloona alilitenda ni kusimama na hao vijana ulosema wanapenda mteremko
Vijana wengi walikabidhiwa nyadhifa mbalimbali wakati huo wakiwa hawana uwezo wakuongoza
Walitumia nguvu na mabavu na ilifika hatua ilionekana kufanya ubabe ni kumfurahisha JPM sababu vijana hao hawakuwajibishwa wakati uwo na wengine walitoka hadharani na kujigamba
Hatujui lengo hasa lilikuwa ninini ila ata walio onyesha kumtii siyo sababu walimweshimu bali walifanya kwa kumwogopa nadhani sasa unaona wanavyo furukuta
Kama JPM alikuwa mtu sahihi basi hakufanya kazi na watu sahihi
Ila bado taifa hili tunasubiri mtu sahihi [emoji27][emoji27]
 

Frankly speaking nahisi ndugu yangu umeajiriwa na kipindi cha Magufuli kilikukuta umeajiriwa, japo mishahara ilipandishwa kwa nadra Ila policy zake zilifanya bidhaa zisipande na kuwafanya walioajiriwa kuwa less affected

Ungekuwa umejiajiri au unatafuta pesa zako mwenyewe town au umeajiriwa private sector hususani zinazodeal na biashara,

ungejua stress na depression watu walizopitia na jinsi covid ilivyowachanganya watu, sidhani kama ungeyasema hayo

Magufuli alifanya mazuri yake lakini kauli ya kusema ambao walioathirika katika kipindi chake ni wavivu au waliotegemea pesa za deal. Umewakosea watu wengi sana
 
Heading yako haiendani na ulicho andika.

Huwezi mfananisha magu na Nyerere kwa mfanano wa aina yeyote ni kama mbingu na aridhi...

Labda kam unamtindio wa ubongo..
 
Ungekua unajituma, Miaka mitano ya JPM,, usingeiona michungu ikiwa unazungumza nje ya mwelekeo wa kisiasa.

Mkuu hiko kizazi cha fesibuku hakiwezi kukuelewa,,, Watu wanaopenda hela halafu hawataki kufanya kazi JPM alikuwa ni mwiba mchungu sana kwao...

JPM ukiacha siasa zake,,, alipenda sana Kazi.
 
Mkuu hiko kizazi cha fesibuku hakiwezi kukuelewa,,, Watu wanaopenda hela halafu hawataki kufanya kazi JPM alikuwa ni mwiba mchungu sana kwao...

JPM ukiacha siasa zake,,, alipenda sana Kazi.
JPM labda kwa nyie wanyonge, ila kwa watu wenye akili na wasiotegemea serikali ni utopolo
 
Nyerere, Mkapa na Magufuli ni Marais bora na wazalendo kuwahi kutokea.

Hawakuwa wabinafsi, na waliamini hii ni nchi ya Watanzania wote, siyo wao na familia zao pekee.

Hawa wengine waliobaki wanaamini hii ni nchi yao na familia zao pekee.
 
JPM akahakikisha Ofisi Y Z M K L, zinatangaza Ajira hadharan, Vijana wanapata Ajira Kwa uwazi kabisa.... Kwa kikwete yalikuwepo hayo ???
Ajira zipi hizo mkuu??

Utawala wa Jpm haukua mzuri hata kidogo.

Huenda ni kweli aliwaminya matajiri lakini aliwapa nguvu kubwa viongozi aliowateua, aliwapa mamlaka hata ya kuamua kesi ilhali wao sio mahakama.

Sio busara kwa sisi watz kuwatusi watu wazima tena hadharani, lakini kwenye utawala wake wastaafu walisemwa vibaya na viongozi wenye umri sawa na wajukuu zao.

Ilikua akikuoenda raisi basi ndo tiketi ya kunyanyasa wenzio.
Matajiri walisumbuliwa mno na watawala, na bahati mbaya sio wote walikua na pesa za mchongo ila waliteswa, kupigwa, kuuwawa na wengine kupokonywa mali zao.
 
Jpm hakua raisi safi.

Huyo mnaemuita mnyonge ni yule aliezisaka akazikosa, lakini eti ndo anyenyekewe kisa tu kashindwa kupata pesa. Na aliezipata anaonekana ni mpigaji na anamnyonya huyo aliekosa.

Sijui akili za wapi hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…