Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Usihukumu kabla hujahukumiwa, kuna mambo yanatokea walimu wanajua mazingira
Nasubiri taarifa kabla sijahukumu
 
Maswala ya ada achaneni nayo, we piga mtoto wangu apasuke then uone ambavyo naweza nikakuchukulia hatua mwenyewe za kukutia nguvuni.

Huu upumbavu wa kuumiza watoto kwa stress zenu lazma ukomeshwe in a hard way.
Elimu inaanzia nyumbani, mzazi unaposhindwa kufunza wanao nyumbani, mzigo unaangukia kwa walimu. Mlee mwanao katika njia bora, hatachapwa. Kama huwezi kulea, mpeleke shule za mqmilioni, kule wako tayari kukusaidia.
 
Mkoa gani huko ambao wanafunzi bado wanaenda tuition miaka hii!??
Mkuu upo nchi gani? Licha ya serikali kupiga marufuku tuition bado kuna walimu wanawatoza wanafunzi fedha za tuition kwa kisingizio kwamba wazazi wenyewe wameomba.

Pia tuition mbona zinafundishwa maeneo mengi tu hasa ya Dar kama Mwenge, Mchikichini, Mnazi Mmoja na maeneo mengi. Mikoani ndiyo kabisa.
 
Kipigo kizito unakijua wewe mzee ebu acha ukuda.

Halafu mlisema hao watoto wasichapwe matakoni wamepigwa mikononi nyenyenye......

Safi sana mwalimu kisogi
 
Kwahiyo mtoto wa kike sio mwanafunzi hatakiwi kupigwa?
 
Hivi baadhi ya walimu au hata wazazi wanatoa wapi nguvu za kumchapa mtt mpaka akaumia...mfn kuvimba au kupasuka? mie mbona sina nguvu hizo!!!! Nikichapa mtt kdg tu siku ya pili nikiamka mkono unauma
 
Ivi Kuna utofauti gani wakuu Kati ya enzi zile za ukoloni ambapo watu waliadhibiwa kwa fimbo na mijeredi na fimbo zinazotolewa mashuleni na walimu Kama vile watoto mashuleni bado wanauishi ukoloni wa enzi hizo
 
Usihukumu kabla hujahukumiwa, kuna mambo yanatokea walimu wanajua mazingira
Nasubiri taarifa kabla sijahukumu
Hakuna mahali nimehukumu,maoni yangu yametokana na habari ilivyoandikwa kwamba mwalimu amepiga wanafunzi na amewaumiza sasa kama mleta uzi ameandika tofauti na kilichotokea huko hilo siyo langu.
 
Hao QT mkuu....
Reseaters...
Au Elimu ya Watu Wazima... Auu Failures wanaotafuta credits.

Ile tuition ya kucover class topics iko mikoa gani siku hizi .!?. tulisoma zamani . Or else wanaenda kudinyana tu.

Wanafunzi wako makambini siku hizi...
 
Ila wakifeli. Walimu hawafundishi.
Ukipigwa mikononi lazima uvimbe.
Ili kuepusha haya serikali ifute viboko, yatakayojiri jamii itulie tuli.
Vimbo ni ukatili ila kukosa nidhamu na hatimae elimu ni ukatili zaidi.
We are very emotional to a corpral purnshment but very silency to a failed and disorganized of education system.
fu#c@k the corrupt society!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…