Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Mtoto kwanini asikupende???

Kama mtoto hakupendi lazma kuna shida lazma kuna shida.....shule huwa kuna mwalimu mkali anakun'guta lakini ni mshakaji wa watoto. Ukali pekee sio sababu mtoto akuchukie kwa cha ziada
Una point dada! Nimeshaliishi hilo!

Baada ya kuhitumu Chuo Kikuu, nilifanya kwa muda kazi ya ualimu ingawa mimi si Mwalimu kitaaluma!

Japo mimi ni mpole, lakini nilifahamika kwa wanafunzi kama Mwalimu anayeongoza kwa ukali!

Ajabu ni kuwa walinipenda sana na kuniamini mno.

Nilikuwa nikiwachapa mpaka wanafunzi ambao wenzangu walikuwa wakiwaogopa, pale wanapostahili adhabu hiyo. Na wengine nilikuwa nikishawaadhibu, unaweza ukanikuta nimekaa nao tunapiga stori kama marafiki.

Waliniamini sana kiasi kwamba nilipoamua kuacha kazi, uongozi uliniomba nisitangaze kwa kuhofia kuwa kutawasikitisha sana wanafunzi (Ilikuwa ni shule binafsi ya boarding).

Ila kuhusiana na hilo la Mwalimu aliyedaiwa kuwaadhibu watoto isivyo, bado nasita kuamini kama kweli yametendwa na mlalamikiwa au katengenezewa tu skendo!
 
Zinasaidia ama hazisaidii nchi?

Kwa hivyo ili kupata Div one ni sahihi kupiga mtoto kokote mwilini ilomradi apate ufaulu mzuri?
Kumpiga mtoto ni kosa! Ila kumchapa pale anapostahili hiyo adhabu ni sahihi!

Kumpiga tu ovyo hovyo ni makosa Kisheria na ni dhambi mbele za Mungu!

Hupaswi kumwadhibu mtoto ukiwa na hasira!
 
Kumpiga mtoto ni kosa! Ila kumchapa pale anapostahili hiyo adhabu ni sahihi!

Kumpiga tu ovyo hovyo ni makosa Kisheria na ni dhambi mbele za Mungu!

Hupaswi kumwadhibu mtoto ukiwa na hasira!
Ndicho nilichokizungumza

Kuwachapa watoto hovyo bila kuzingatia sheria ama taratibu ama maelekezo ni kuwafanyia ukatili


Seminari zinaumiza watoto
 
Dah natamani kuzaliwa miaka hii nisome shule za serikali niwe sipigwi Wala siguswi yaani ni full kutetewa .

Hapo namkumbuka mwalimu Janeth (mke wa mwendazake ) niliwahi kubeba peni yake ofisini kumbe Kuna ticha aliniona yule mama alinifinya haswa mpaka leo nilikuwa najiapia kama angeng'aa kwenye sura yangu siku yoyote hakika ningemkumbusha kuwa mama Mimi ndiye yule kijana niliyekwiba peni yako alafu ukanifinya vibaya mno .


Jamani mtoto sio fimbo ila walau kipigo Cha kawaida ni muhimu kwa maendeleo ya akili ya mtoto .
Kifinyo kilikusaidia?

Ungali na hasira na Mwl Janeth?
 
Ndicho nilichokizungumza

Kuwachapa watoto hovyo bila kuzingatia sheria ama taratibu ama maelekezo ni kuwafanyia ukatili


Seminari zinaumiza watoto
Sina uzoefu na seminari, lakini uchapaji wa hasira ni makosa. Adhabu kwa mtoto, iwe nyumbani au shuleni halipaswi kutawaliwa na hasira. Hasira ya binadamu huzaa hasara
 
Ukiwasikiliza vizuri hawa watoto kuna mahali utajua mambo hayako sawa. Hawana nidhamu kabisa. Ningekuwa mzazi wao ningewaongeza viboko vingine
Nakubaliana nawe kwa sehemu! Nidhamu ya hao watoto imepinda. Pengine ni kama walishakuwa Sugu kwenye utomvu wa nidhamu.
 
Kabla sijawa mwalimu nilikuwa na mawazo kama Yako.
Na mimi kabla ya kufanya kwa muda kazi ya ualimu nilikuwa siamini katika adhabu ya viboko. Lakini nilipoingua "field" niligundua kuna watoto hawaendi bila viboko.
 
Mwalimu kolo, mtoto wangu kama kakosea kabla ya adhabu nipewe taarifa kwanza
Mfundishe nÿumban,unajua situation aliyokutana nayo? Mfano mwanafunzi kamtukana Mwalimu kwahyo asishughulikiwe Hadi wewe upate taarifa? Atashughulikiwa ipaswavyo
 
Kuna haja gani kumpiga mtoto wa mtu kwakuwa tu amechelewa kufika shule au jana yake hakuja shule? Wewe mwalimu kazi yako ni kufundisha tu hayo mambo mengine hayakuhusu sanasana unaweza kumuita mzazi wake na kumueleza tatizo la mwanawe ili kama kumpiga ampige yeye mwenyewe.
Ningekuwa mwalimu haya matatizo ya kujitakia ningeyaepuka kabisa ningeacha kujitia kiherehere kwa kujifanya nampenda sana mwanafunzi wakati yeye mwenyewe hana mpango na elimu.
Wisely spoken
 
Sasa umpige mtu mpaka avimbe mkono ndio nini?Hii sio adhabu mwalimu ana stress za maisha hasira zake anamalizia kwa watoto.Mwambieni sa100 awaongezee mishahara sio kupiga piga na wengine wameua watoto wa watu wakaishia kukimbia.
 
Mwalimu Kisogi wa shule ya Sekondari Mwilibona awapiga wanafunzi wake 2 na kuvimba mikono na damu kumwagika kisa wamechelewa kufika shule.

Wanafunzi wao wamesema walikuwa wanakwenda kusaini ofisini kwake kwa sababu walikuwa wanakosa shule. Kwahiyo walitakiwa kila siku wasaini saa moja na nusu sasa leo wakiwa wamechelewa baada ya hapo mwalimu huyo akawashushia kipigo kizito wanafunzi hao.

Soma Pia: Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati
Haya wengine wapo mbioni kuja wapo kwenye mchakato wa usahili. Hivi kwani adhabu za mashuleni hazijulikani?Bora hata umpe kazi za mikono au uzalishaji apoteze muda siku nyingine akome kurudia kosa sio kumjeruhi.
 
Tazama clip hapo chini. Serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka kwenye suala hili na kufanya uchunguzi wa kina kabisa ikiwemo na kuwahoji watoto wanaosoma hizi shule maana hivi tunavyoona inaweza ikawa ni tip of the iceberg tu.

Malaria 2 ndiyo mnavyofundisha watoto hivi mpaka mnawatoa damu?

 
Back
Top Bottom