GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Una point dada! Nimeshaliishi hilo!Mtoto kwanini asikupende???
Kama mtoto hakupendi lazma kuna shida lazma kuna shida.....shule huwa kuna mwalimu mkali anakun'guta lakini ni mshakaji wa watoto. Ukali pekee sio sababu mtoto akuchukie kwa cha ziada
Baada ya kuhitumu Chuo Kikuu, nilifanya kwa muda kazi ya ualimu ingawa mimi si Mwalimu kitaaluma!
Japo mimi ni mpole, lakini nilifahamika kwa wanafunzi kama Mwalimu anayeongoza kwa ukali!
Ajabu ni kuwa walinipenda sana na kuniamini mno.
Nilikuwa nikiwachapa mpaka wanafunzi ambao wenzangu walikuwa wakiwaogopa, pale wanapostahili adhabu hiyo. Na wengine nilikuwa nikishawaadhibu, unaweza ukanikuta nimekaa nao tunapiga stori kama marafiki.
Waliniamini sana kiasi kwamba nilipoamua kuacha kazi, uongozi uliniomba nisitangaze kwa kuhofia kuwa kutawasikitisha sana wanafunzi (Ilikuwa ni shule binafsi ya boarding).
Ila kuhusiana na hilo la Mwalimu aliyedaiwa kuwaadhibu watoto isivyo, bado nasita kuamini kama kweli yametendwa na mlalamikiwa au katengenezewa tu skendo!