Mwalimu wa Kanisa ahukumiwa miaka 30 kwa kosa la kulawiti

Mwalimu wa Kanisa ahukumiwa miaka 30 kwa kosa la kulawiti

Dar es Salaam.
Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi (22), mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani.

Mushi, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kufundisha watoto kanisani anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, mwaka huu katika Kanisa la Embassy Kingdom.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Ester Mwakalinga baada ya kuwasikiliza mashahidi saba wa upande wa mashitaka, akiwamo mtoto mwenyewe, mama mzazi pamoja na mchungaji wa Kanisa la Embassy Kingdom aliyekiri kumfahamu mama mzazi wa mtoto aliyetendwa.

Mashahidi wengine ni daktari wa Hospitali ya Sinza Palestina aliyempima mtoto huyo pamoja na askari wa Kituo cha Polisi Osterbay. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ester alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa, mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa analotuhumiwa nalo.

“Kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa, ikiwemo ripoti ya daktari (PF3) na ushahidi wa mama na mtoto mwenyewe, mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, hivyo inakutia hatiani kwa kosa la kulawiti,” alisoma Hakimu Ester.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hilda Kato aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kufanya vitendo vya udhalilishaji na kikatili kama hivyo katika jamii.

SOURCE: MWANANCHI
 
Dar es Salaam. Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi (22), mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani....
Dah habari kama hizi sio za kutangaza.

Serikali ipige marufuku kutangaza mambo ya kikatili kama haya lakini hukumu ziendelee.

Kuyapaza sauti haya mambo inakera,omba yasimkute ndugu yako haya mambo utaona inavyouma kutangaza.

Nimesema kutangaza sio kuhukumu,hukumu ziendelee ila isiwe matangazo.
 
Bora kupiga nyeto miaka 30 jela ni mingi
 
Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi, mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani...
Elisha Mushi-mchaga mpumbavu
 
Najaribu kuvaa uhusika kama mzaz wa mtoto nina iman kesi isingefika hapo kortini....!! Mwalimu wa kanisa ni mpuuzi pia nadhani anatumikia shetani badala ya mungu.
 
Ingekuwa ni ustadh wa madrasa tungeona mtiririko mrefu lakini mwalimu wa kanisa kimyaaa.
We jamaa ovyooo KABISA...nani kakuzuia kutiririka?nyie ndio mnaoharibu dini yetu...kwakulalamika vitu visivyo na msingi...HAPA TUNASIKITIKA HII DHAMBI ALOTENDA HUYU SHETWAN,NA KUMUHARIBU MTOTO,WEWE UNALETA ANGEKUWA NANI SIJUI,NANI ETI...
 
Na ndvyo mungu wao anawasisistiza kufanya uo ushenzii...tunawasisitiza kila siku zikimbien dini ngeni amtaki ona sasa maajabu yake, awo mnaozan watakatifu kumbe ndio mashetan namba moja.....fucking colonial religions
 
Watoto zetu wakiwa mtaani shida, mashuleni tatizo adi sehem takatifu ndio majanga kabisa..


WAKIBAKI NYUMBANI MA HOUSE GIRL PIA KIKWAZO..

itabid tutembee nao makazini aiseee
 
Nilitaka kuuliza ni kanisa gani ila nimeamua kuacha tu.
 
Back
Top Bottom