Mwambieni CAG, sisi tumeridhika kwa kuwa tumezoea kuibiwa

Sasa najiuliza ikiwa ripoti ya CAG imeonesha madudu je, ni jinsi gani sasa kama taifa tumeingiaje uchumi wa Kati? Ikiwa tumeibiwa Sana namna hii.

Kuna bandiko linatembea nazani ni kutoka timu Sukuma Gang kujibu tuhuma za Msoga gang.

=====

MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM.

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga.

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye.

Tutakua Taifa la kijinga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga wavivu wasio na lolote walioachiwa Nchi waiongoze wakihangaika na umbea udaku na ushambenga.

Kwa taarifa yenu [emoji847]#SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.

#TutakukumbukaDaimaJPM
Ni Wapumbavu tu ndio Wamezoea KUIBIWA
 
Tunahitaji mafisadi kama Magufuli kwa miaka 30 tu ili nchi yetu iwe kama Ulaya.

Kama huyu jamaa aliiba mabilioni ya pesa na bado akaweza:

-Kununua ndege zaidi ya 9 kwa cash. ( Ni wajinga sana wanunuao ndege kwa cash )
-Kutoa elimu bila malipo kwa miaka takribani 6 (Hata ulaya hawatoi elimu bure)

-Kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati (reli ya kisasa, umeme mkubwa, madaraja makubwa, barabara etc. kwa cash sio kwa mkopo.

-Kijenga vituo vya afya zaidi ya 400 nchi nzima( sio Zahanati jamani, vituo vya afya hata huduma ya operation inapatikana)

-Kulipa watunishi wa serikali kabla ya tarehe za mishahara.

-Kujenga vituo vipya vya mabasi kila mkoa.

Kujenga masoko makubwa kila mkoa.

-Kubwa kuzidi yote...kuingia uchumi wa kati miaka 5 kabla.

Huyu jamaa hatari.
 
Kwa miaka mitano tu.Tunahitaji watu kama hawa.Sio kina Assad wachumia tumbo
 
Huyu msela mtoa mada ni disaster kwa jamii na mbaya zaidi it seems ubongo wa huyu mchizi uko vacation Chato kazikwa nao yule Fisadi..

Alipo hapo hajitambui mnyonge huyu anajaza server za Maxence Melo kwa threads za ki Pumbavu..
 
Mimi ni mtanzania na nina haki ya kutoa mawazo yangu.Nimeridhika na wizi wa Magufuli,kwa kuwa hata kama kaiba,ila nimeona alichofanya,tena kikubwa.Wengine walishibisha matumbo yao,familia zao na kugawa bure mali za Watanzania kwa mabeberu.
Uko sahihi...
 
NAOMBA msimtukane Huyu jamaa mwenye uzi huu ila mpite kimya kimya au kwa sala na kumuombea ajue hivi "KUNA WATOTO WAMESHINDWA KUPATA MKOPO ILI WASOME CHUO KIKUU" ila pesa za matamasha zilikuwepo
Huyu ni wa kumpuuza tu. Akitaka sana aende chato akamfufue mwendazake. Kama hana nauli wazalendo tumchangie akaifanye kazi tukufu ya ufufuaji huko maeneo ya jirani na Burigi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni raha kuwa na Rais fisadi kama Magufuli, ambaye anaiba kwa kuwanufaisha wananchi wake, anaiba anajenga vituo vya afya, anajenga reli, na kufufua reli iliyokufa zaidi ya miaka karibu thelathini, anaiba watoto wanasoma bure, anaiba anajenga barabara na kuweka taa za barabarani karibu miji yote Tanzania, anaiba huku akitulindia madini yetu, anaiba akiongeza mikopo vyuoni, anaiba akiboresha huduma za matibabu sasahivi wote tunatibiwa nchini, hata yeye kafia hospitali za hapa hapa.

Daah! huyu fisadi Magufuli ni kiboko. Siyo wale mafisadi wa EPA, mafisadi wa Richmond, waligawana wao wenyewe fedha na kuita hela ya mboga huku watanzania wengi wakiugulia maumivu. Hata hawakukumbuka kununua hizo ndege za mkopo, ambazo Assad, anadai huyu fisadi Magufuli ati ni kichaa hana akili kwa kununua ndege kwa cash.

Naomba kuuliza hivi ukinunua kwa mkopo ndo wapata faida? Au hutolipa hilo deni? Make najua deni utalilipa tu tena kwa faida. Ok fisadi Magufuli lala salama wewe kweli ni shujaa wa mafisadi unae iba ili kufaidisha Taifa lako. Tunasubiri kuona hawa waliokuwa wasafi wasio mafisadi, wapi wanatupeleka, je wataweza kufanya tuliyoyaona kwa ufisadi wako lakini leo, tunayafurahia. Yetu macho.
 
Tunahitaji mafisadi kama Magufuli kwa miaka 30 tu ili nchi yetu iwe kama Ulaya.

Kama huyu jamaa aliiba mabilioni ya pesa na bado akaweza:

-Kununua ndege zaidi ya 9 kwa cash. ( Ni wajinga sana wanunuao ndege kwa cash )
-Kutoa elimu bila malipo kwa miaka takribani 6 (Hata ulaya hawatoi elimu bure)

-Kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati (reli ya kisasa, umeme mkubwa, madaraja makubwa, barabara etc. kwa cash sio kwa mkopo.

-Kijenga vituo vya afya zaidi ya 400 nchi nzima( sio Zahanati jamani, vituo vya afya hata huduma ya operation inapatikana)

-Kulipa watunishi wa serikali kabla ya tarehe za mishahara.

-Kujenga vituo vipya vya mabasi kila mkoa.

Kujenga masoko makubwa kila mkoa.

-Kubwa kuzidi yote...kuingia uchumi wa kati miaka 5 kabla.

Huyu jamaa hatari.
sema ww ndio unahitaji. MWIZI NI MWIZI TU. HAIJALISHI ANAIBA KANDAMBILI AU BILLION BANK.

hii nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria sio matakwa ya kikundi fulani.
 
Tunahitaji mafisadi kama Magufuli kwa miaka 30 tu ili nchi yetu iwe kama Ulaya.

Kama huyu jamaa aliiba mabilioni ya pesa na bado akaweza:

-Kununua ndege zaidi ya 9 kwa cash. ( Ni wajinga sana wanunuao ndege kwa cash )
-Kutoa elimu bila malipo kwa miaka takribani 6 (Hata ulaya hawatoi elimu bure)

-Kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati (reli ya kisasa, umeme mkubwa, madaraja makubwa, barabara etc. kwa cash sio kwa mkopo.

-Kijenga vituo vya afya zaidi ya 400 nchi nzima( sio Zahanati jamani, vituo vya afya hata huduma ya operation inapatikana)

-Kulipa watunishi wa serikali kabla ya tarehe za mishahara.

-Kujenga vituo vipya vya mabasi kila mkoa.

Kujenga masoko makubwa kila mkoa.

-Kubwa kuzidi yote...kuingia uchumi wa kati miaka 5 kabla.

Huyu jamaa hatari.
bado madini mmereranni kuwekewa ukutaa na tunaapigwaa Tanzania tajiri sana
 
NAOMBA msimtukane Huyu jamaa mwenye uzi huu ila mpite kimya kimya au kwa sala na kumuombea ajue hivi "KUNA WATOTO WAMESHINDWA KUPATA MKOPO ILI WASOME CHUO KIKUU" ila pesa za matamasha zilikuwepo
Kwanini awape waliosoma serikali 100% hafafu wengine hatupe 70 kwani sisi sio watanzania?
 
SUKUMA GANG.. Hamkati tamaa, endeleeni kupambana
Hivi anayewadanganya kwamba ni swala la Usukuma against Msoga ni nani,hili ni swala la evil against good.Kueni wazalendo kidogo.
 
Sasa najiuliza ikiwa ripoti ya CAG imeonesha madudu je, ni jinsi gani sasa kama taifa tumeingiaje uchumi wa Kati? Ikiwa tumeibiwa Sana namna hii.

Kuna bandiko linatembea nazani ni kutoka timu Sukuma Gang kujibu tuhuma za Msoga gang.

=====

MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM.

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga.

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye.

Tutakua Taifa la kijinga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga wavivu wasio na lolote walioachiwa Nchi waiongoze wakihangaika na umbea udaku na ushambenga.

Kwa taarifa yenu [emoji847]#SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.

#TutakukumbukaDaimaJPM
Mkuu you are misinterpreting and misrepresenting this issue.Issue hii sio rahisi kama unavyo jaribu kuonyesha.Hakuna Sukuma gang na wala hakuna Msoga gang.Wewe unachojaribu kufanya nikuleta chuki kati ya familia ya Marehemu Magufuli na Kikwete.This is wrong and utter nonsense,and uncalled for.Hii ni vita ya evil against good,it has nothing to do with Magufuli and Kikwete.Please understand this.
 
Natamani niweke like miakenda.

Well said bro.. Nakuunga mkono kwa % 100 jambo la maana hapa nikwamba sisi watanzania sio wajinga tuna macho na tunaona.

Kuna watu hawana aibu hata chembe kweli njaa mbaya sana, yani wanajaribu kumchafua mtu aliepambana kuonyesha kwamba tunaweza kufanya mambo makubwa sisi kama nchi.
Tena kwa mifanohai na kwamudamfupisana.

Mungu amlaze pema JPM.
Huko kupambana kisirisiri bila kufuata utaratibu ndio kunakoleta mashaka. Kama umeridhia ni wewe binafsi ila mimi kama miongoni mwa mlipa kodi sijaridhia. Hayo mambo yanayoonekana kwa macho yanamsaidia nini mlalahoi anayeishi kijiji cha kiwale huko malinyi ambapo yeye hiyo barabara za juu, barabara nane nane, treni ya mwendokasi na midege isiyoleta faida haimpatii lolote wakati wa pesa kwake umekuwa mgumu halafu anaambiwa achangie ela kwaajili ya miradi ya shule na zahanati akishindwa kufanya hivyo anawekwa ndani.
 
Huko kupambana kisirisiri bila kufuata utaratibu ndio kunakoleta mashaka. Kama umeridhia ni wewe binafsi ila mimi kama miongoni mwa mlipa kodi sijaridhia. Hayo mambo yanayoonekana kwa macho yanamsaidia nini mlalahoi anayeishi kijiji cha kiwale huko malinyi ambapo yeye hiyo barabara za juu, barabara nane nane, treni ya mwendokasi na midege isiyoleta faida haimpatii lolote wakati wa pesa kwake umekuwa mgumu halafu anaambiwa achangie ela kwaajili ya miradi ya shule na zahanati akishindwa kufanya hivyo anawekwa ndani

Yani unaongea kama umekurupushwa usingizini, wewe unataka kilakitu kinacho fanywa na serikali kimridhishe kilamtu??.

Watu kamawewe ndio jualikiwaka mnataka mvua, mvuaikinyesha mnatakajua

Kama unaona reli, barabara, na flyover hazisaidii kitu basi check your self.

Unajua tunaokoa kiasigani cha pesa kwakurahisisha usafiri katika majiji makubwa kama Dar es salaam??.
Unajua chanzo kikuu chamapato nikodi inayotokana na wafanya biashara ambao wengi wana connection na jiji la Dr.?

Ukokijijini kwako unakotaka papewekipaumbele mnachangi kiasigani kwenye pato la taifa.
Subiri turahisishe usafiri mijini ambopo ndio chanzo kikubwa cha mapato ambayo yana tumika kujenga zahanati unazoziona uko kijijinikwako pamoja na umeme unaouona kwenye nyumba za tembehukokwenu.
Pia ukiona watoto wenu wanasoma bure ujue pesa inatoka huku serikali inapo wekeza pesa kwa kurahisisha movement kwa walipakodi.
 
Back
Top Bottom