Mwambieni CAG, sisi tumeridhika kwa kuwa tumezoea kuibiwa

Mwambieni CAG, sisi tumeridhika kwa kuwa tumezoea kuibiwa

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyo hivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!...
Mkakati wao wa kumchafua JPM tutaupinga kwa gharama yoyote! Umma upo na chuma [emoji109]
 
Mafisadi wanamchafua JPM! Chuma alipanda mbegu na sasa hatutokubali uhuni ....mnataka kuharibu taswira yake overnight? Hao aliowaamini ambao wameingia woga wa ajabu dhamira zitawasuta daima ...sie wengine tutasimamia maono yake ....
 
Kuna kapoint fulani!
Sawa CAG report imetoka
Ni hatua gani itachukuliwa

Ova
Lengo ni kumchafua JPM tu na sababu ni marehemu wanajua hakuna wa kumtetea! Mmesahau walianza kumchafua hadi Nyerere? Same stupid people wanaoungwa mkono na wanasiasa uchwara ...
 
Kaka ume Sikitisha saana na kuni kumbusha mbaaali sana....!

CAG anajifanya hakuwepo watu walipo sema milion.10 HELA YA MBOGA....?

wakabeba hadi kwenye mmaguni...
 
Sasa najiuliza ikiwa ripoti ya CAG imeonesha madudu je, ni jinsi gani sasa kama taifa tumeingiaje uchumi wa Kati? Ikiwa tumeibiwa Sana namna hii.

Kuna bandiko linatembea nazani ni kutoka timu Sukuma Gang kujibu tuhuma za Msoga gang.

=====

MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM.

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga.

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye.

Tutakua Taifa la kijinga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga wavivu wasio na lolote walioachiwa Nchi waiongoze wakihangaika na umbea udaku na ushambenga.

Kwa taarifa yenu [emoji847]#SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.

#TutakukumbukaDaimaJPM
SISI
Wewe na Nani?

#YNWA
 
Zungumzieni hela za awamu ya tatu na nne zilienda wapi,what is 1.5 trillion hata kama kaiba in the face of probably 400 trillions which disappeared during Mkapa and Kiketes' eras,mbona mnakuwa viazi hivyo?After all kaiba kapeleka wapi,mbona hata kwake hamna kitu.Hata nyumba yake ni modest.Mnatumiwa ninyi si bure.
Mbona maneno yamekuwa mengi....au kutaka kujua issue iliishaje ni kitu kibaya!
 
Imeridhika usitisemee, eti maendeleo ya Magufuli unayaona, ok ndege unaziona, zimekupa faida gani ? Wakati toka ununuzi wake ni hasara kwa mwaka billion 60, mwaka jana wanafunzi 7,000 wamekosa madarasa mbali walio kosa mkopo wa elimu ya juu, we pumbavu sana.

Unaona maendeleo ya juu tu Yaani Yale madaraja ya Dar es salaam tu ? Jee hizo barabara alijenga nani?

Yaani wizi ulio fanyika miaka hii 5 hata EPA ipo nyuma, kila kona ni wizi na mmetia nchi kwenye madeni kutoka asilimia 8 to 35 .

Hawa wanao sifa wizi ndio wizi wenyewe, na mpaka sasa takukuru hawajachukua hatua.

Nchi ya ajabu hii au ndio mpaka Rais Aseme?
 
Kufa na wewe umfuate basi. Naona unatamani kwenda kumsalimia na kumwambia kuwa "wenzako wanakutukana".
Mmebaki na maneno ya hovyohovyo tu kamahivi.
Naona unatamani kujinyonga ukisikia miradi kama stigle PM akisema lazima ikamilike kwa wakati, na ndio maana ya zege hailali kama hamjui.
Fanyeni kazi mtakufa njaa nchi inaendelea kwa kupiga kazi sio majungumjungu na wivu wa kipuuzi shawishi jiranizako walipekodi kwa wakati tujengenchi.
 
Acheni kulialia hatakama amekopa kwani shidaikowapi, ilimradi tunaona matokeo ya izohela it's just fine, Ok?.

We lipakodi deni lilipwe na ndio tafsiri ya kujenga nche wewe mwenyewe kwa pesa zako.
Nyie watu nani amewashikia akili?.

Swala la kumuunga mkono Rais wetu Mh, Samia Suluhu hiyo inaeleweka na wote tunaungana kwa hilo.
 
Imeridhika usitisemee, eti maendeleo ya Magufuli unayaona, ok ndege unaziona, zimekupa faida gani ? Wakati toka ununuzi wake ni hasara kwa mwaka billion 60, mwaka jana wanafunzi 7,000 wamekosa madarasa mbali walio kosa mkopo wa elimu ya juu, we pumbavu sana.

Unaona maendeleo ya juu tu Yaani Yale madaraja ya Dar es salaam tu ? Jee hizo barabara alijenga nani?

Yaani wizi ulio fanyika miaka hii 5 hata EPA ipo nyuma, kila kona ni wizi na mmetia nchi kwenye madeni kutoka asilimia 8 to 35 .

Hawa wanao sifa wizi ndio wizi wenyewe, na mpaka sasa takukuru hawajachukua hatua.

Nchi ya ajabu hii au ndio mpaka Rais Aseme?
Hizi ni story za vijiweni mkuu zenye nia ovu ya kumpaka Magu matope.Lakini mwenye macho haambiwi tazama.Ingekuwa busar na hekima mngetuambia miaka 30 ya Mwinyi,Mkapa na Kikwete hela yetu ilikwenda wapi,maana kwa Magufuli tuliona wazi aliyokuwa anafanya.
 
Mimi ni mtanzania na nina haki ya kutoa mawazo yangu.Nimeridhika na wizi wa Magufuli,kwa kuwa hata kama kaiba,ila nimeona alichofanya,tena kikubwa.Wengine walishibisha matumbo yao,familia zao na kugawa bure mali za Watanzania kwa mabeberu.

Mawazo yako au umecopy na Kupaste..watu wawili mnafanana maandiko.. Majinga kabisa nyie Masukuma.
 
Mawazo yako au umecopy na Kupaste..watu wawili mnafanana maandiko.. Majinga kabisa nyie Masukuma.
Wala mimi sio Msukuma.Na wala ku-copy na ku-paste sio issue,issue ni message.Na swala la usukuma linatoka wapi?Kama kila jambo jema ni la Kisukuma,basi nakubali kuwa Msukuma.
 
Wala mimi sio Msukuma.Na wala ku-copy na ku-paste sio issue,issue ni message.Na swala la usukuma linatoka wapi?Kama kila jambo jema ni la Kisukuma,basi nakubali kuwa Msukuma.
Toa mawazo yako na kile unachokiamini.. Kucopy na Kupaste ni kuonesha udhaifu wako wa kufikiri
 
Toa mawazo yako na kile unachokiamini.. Kucopy na Kupaste ni kuonesha udhaifu wako wa kufikiri
Kwani wewe elimu uliyo nayo ni original,si copied and pasted,acha mtizamo finyu wewe. Na una uhakika gani kwamba nime-copy.Lete na wewe bandiko lako,angalau hata copied and pasted.

Nirudie ku-copy na ku-paste sio issue,issue ni message.Hii sio journal paper,nia ni ku-inform,acha uzuzu.
 
Pumbavu wewe.

Sema umeridhika wewe na mume wako,sisi wenye akili hatuwezi ridhika na upuuzi kama huo.
[emoji23][emoji23][emoji23]kinacho furahisha ni kwamba wakija wenye kusapport wanasema wenye akili wanajua Nini kafanya mwendazake mkija na nyinyi mnasema nyinyi wenye akili hamwezi kukubaliana na aliyofanya [emoji23][emoji23][emoji23]dunia tamu hii Perception ina nguvu Sana
 
Lakini kazi ya mabeberu si unaijua,na hiyo si ndio kazi yao,na wewe ni kifaa chao.Boss wako Lissu si naye unajua ni mtetezi wa mashoga,sasa unaweza kuwa mtetezi na wewe bila kujua hivyo fani.
Boss wangu mama Samia mbwa wewe
 
Kazi ya CAG si kutafuta mazuri yaliyofanywa na serikali,
Ona huyu naye sijui katoka wapi. Kazi yake ni kutoa opinion so yote mabaya na mazuri anatakiwa kuyasema
 
Back
Top Bottom