[h=5]NA TIMOTH LEVY
NILIPOELEZA MATUMIZI YA KONDOMU NA MWISHO WAKE KWA LUGHA NYEPESI NI HIVI,
Nia ni kuwatahadarisha vijana na siasa hizi za kutumika bila kufikiria mwisho wake ni nini. Niwakumbushe kwa mara nyingine tena mwanamama mmoja aliyejulikana kwa jina la Anjelina Levarasi a.k.a Anjelina Mrema. Alivuma sana nchini.
Huyu alidaiwa kuzaa na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augsutine Mrema. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijua fika jambo hilo, lakini ni baada tu ya Mrema kujiengua kwao.
Anjelina alitoka na kutangaza hilo hadharani na CCM ikamdaka kuendeleza kampeni chafu hiyo kwa kumtumia ili kumvunjia staha Mrema; wakati huo akiwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Mwanamama huyo alikwenda nyumbani kwa Mrema kudai hili na lile. Alifikia hatua ya kuvua nguo zote na kubaki uchi. CCM wakachekelea.
Hata hivyo, Anjelina alifika mwisho bila kupata cha maana kutoka CCM waliomtumia. Mwishowe alikuja kufa kifo cha kusikitisha akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni bila ya msaada wowote. Waliokuwa wakimtumia hawakumsitiri.
Michael Nyaruba aliyekuwa kiongozi mwandamizi Chama cha Wananchi (CUF), ni mfano mwingine. Hakuwa mali kitu kwa CCM hadi pale alipokosana na viongozi wa CUF. Alihamia CCM ambako alionekana lulu. Akatumiwa kuvuruga CUF. Alijinasibu kujua siri za aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Seif Sharif Hamad, ambaye sasa ni katibu mkuu wa chama hicho na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Siri alizodai kuzijua zikihusisha viongozi wa CUF zikatumika kutengeneza kesi ya uhaini Zanzibar.
Nyaruba alikuwa anakwenda Zanzibar kama mfalme. Akikodishiwa hadi ndege na kuandaliwa mikutano ya hadhara uwanja wa Malindi, kwa ufadhili wa iliyokuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) chini ya Rais aliyepachikwa jina la Komandoo, Dk. Salmin Amour.
Siyo tu alihudumiwa usafiri na matumizi kwa safari za kwenda na kurudi Zanzibar kuandaa ushahidi dhidi ya Maalim Seif ili ashitakiwe mahakamani, bali pia alipewa ulinzi mzito.
Hakufika mbali. Aliishia tu mtu wa kutumwa na kazi yake ilipoonekana haina tena tija, akatekelezwa na CCM. Kwa kuwa angali hai, mwenyewe anaweza kueleza haya vizuri zaidi.
SASA NI WENYE AKILI TU NDIYO WANATAMBUA KUWA CCM NI ILE ILE HAIJABADILIKA NA MALENGO YAKE NI YALE YALE TU.
"DUDU LIUMALO USILIPE KIDOLE HATA KAMA LINATABASAMU"[/h]