Mwamposa, Lusekelo na Mitume wengine: Tenda ya kuyaondoa mapepo yanayorusha mawe Arusha!

Mwamposa, Lusekelo na Mitume wengine: Tenda ya kuyaondoa mapepo yanayorusha mawe Arusha!

Ningekuwa wewe, ningeomba muujiza utokee niende kwasababu hata magari yapo chini yako.

Wafia dini mnajifanya(ga) mna imani sana lakini inapofika mahali pa kujitolea, hamna pesa.
Pesa imeingiaje hapa? Kwamba niache shughuli zangu niende huko?
 
Mapepo kijiji fulani huko Arusha yamechachamaa.
Yameanza kurusha mawe kama vijana wa kipalestina dhidi ya Waisraeli.

Kwa vile mapepo hayo hayaonekani, wananchi wameamua kuvaa ndoo kichwani ili kujihami na hayo maw.

Hapa ndo tuwaone kina Mwamposa, Lusekelo na Manabii wengine.
Tenda hiyo kuyaondoa mapepo!
Nadhani tenda hii apewe Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha sababu kwanza alikuwa mfanyabiashara Arusha pili mahubiri yake kila siku ni vita na wachawi, majini na mapepo.
 
Mapepo kijiji fulani huko Arusha yamechachamaa.
Yameanza kurusha mawe kama vijana wa kipalestina dhidi ya Waisraeli.

Kwa vile mapepo hayo hayaonekani, wananchi wameamua kuvaa ndoo kichwani ili kujihami na hayo maw.

Hapa ndo tuwaone kina Mwamposa, Lusekelo na Manabii wengine.
Tenda hiyo kuyaondoa mapepo!
kuna mitume bongo ndugu ?
 
Mbona ameshawahi kwenda nabii no 7 kutoka Arusha mjini, akaomba na kukemea kwa jina la Yesu, kilichotokea ni gari yake ikakung'utwa jiwe kwanza na baadaye mawe yaliendelea kurushwa licha ya ukemeaji kwa jina la Yesu, hali ilipozidi kuendelea ikabidi ahaidi kwamba baada ya siku 21 hali hiyo itakoma.🤣🤣, hadi anaondoka katika eneo hilo mawe yaliendelea kurushwa tu.
 
Mbona ameshawahi kwenda nabii no 7 kutoka Arusha mjini, akaomba na kukemea kwa jina la Yesu, kilichotokea ni gari ikakung'utwa jiwe kwanza na baadaye mawe yaliendelea kurushwa licha ya ukemeaji kwa jina la Yesu, hali ilipozidi kuendelea ikabidi ahaidi kwamba baada ya siku 21 hali hiyo itakoma.🤣🤣, hadi anaondoka katika eneo hilo mawe yaliendelea kurushwa tu.
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
Imenikumbusha incident fulani na intruders wakati niko mgodi fulani, kuna watu wanapenda kujifanya wanaweza kutuliza mizuka hata ya wavuta bangi, siku hiyo tungekufa uzuri tulivaa hard hats aisee!
Jamaa anajifanya kuhutubia ndugu zangu sijui nini, lilifurumushwa jiwe, wenzake nao wakaamshwa kuokota mawe, tulikimbiza gari kwa reverse, mpaka tulipoona vumbi limeharibu uoni wa intruder ndiyo tukageuka na kusonga!

Aisee, wangetuua wale. Tulipokuja kuangalia gari lilivyopondwa Ka lilipinduka!!
Mungu alitulinda, nilimaliza mkataba sikutaka kazi tena!
 
Back
Top Bottom