Nchi imejaa manabii fake. Wanalikufuru jina la Bwana kwa kulitumia jina lake kuwatapeli wajinga waliokosa maarifa.
Huu ni utimilifu wa lile neno lisemalo, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
Mtu anauziwa mchanga, anauziwa maji, na bado anaamini anayemuuzia ni mtumishi wa Bwana!!
Niambieni ni wapi imeandikwa, Kristo aliwaponya wagonjwa, aliwaponya vilema na kuwafufua wafu kwa malipo ya fedha.
Kuwa mkristo ni kukubali kufuata yale aliyoyatenda Kristo. Kristo alijifanya mtu, akaubeba mwili wa kibinadamu ili atuoneshe namna mwanadamu astahilivyo kutenda.
Ushindi wa CCM sio kushindwa kwa Chadema wala ACT bali ni kumkataa Mungu katika Taifa hili na adhabu yake itawaumiza sana watu kama inavyokuwa kule Israel walipoanza kujisahau na kuona kuwa ushoga ni haki yao na kujitangaza hadharani huku wakiwakejeli wale wanaoupinga . Matokeo yake Mungu amekaa mbali na sasa Magaidi wanaingiwa na roho ya vita na mauaji na kuanza kazi ya kumfurahisha shetani kuliangamiza lile taifa teule. Waisrael wangemsikiliza Yesu na kuzitii amri za Mungu leo wanaishi kwa amani sana na Ndugu zao Waarabu maana waarabu sio adui yao. Adui zao walishaamalizwa siku nyingi sana na Daudi na Suleimani. Wengine waliopou adui unaotengenezwa kutokana na kumkataa Masihi wa Mungu awatawale kiMungu.
CCM nayo ilishasema haimtegemei Mungu kutawala apende asipende watawala na kubaki madarakani.
Sasa Mwamposa kutumia mgongo wa kanisa kuomba kura kwa CCM ni unafiki na uchawa wa kiLucufer kwa sababu CCM walishasema hawahitaji kura kushinda . Sasa huyo waakala wa shetani na CCM anapata wapi mamlaka ya kuomba kura wakati wenye chama walishasema hawahitaji kura za wananchi wala Mapenzi ya Mungu kushinda bali kwao ushindi ni lazima.
Waumini wote halasishaneni maana ushindi wa CCM ni wazi sasa kuwa utakua ni kufuru kubwa sana kwa Mungu aliyetuumba na kutuweka hapa Tanzania na rasilimali zote alizoumba yeye na sio CCM bali ni mapenzi yake Kutuumbia hii nchi.
CCM ikishinda Mungu atadharauliwa sana hapa Tanzania . Hili wakristo na waislam tusikubali kamwe. Tuna vyama viwili vilivyoonyesha angalau kulinda heshima na utu na angalau kutetea Haki na kupinga dhulma ,ambavyo ni CHADEMA na ACT . Tujipange tu wachague kuanzia serikali mitaa ,udiwani ,ubunge na urais ili CCM wakae pembeni watubu na kumheshimu Mungu kuliko mwenyekiti wao na wajue kuwa mwenyekiti wao na serikali yake wanaweza kutoa uhai wa mtu lakini hawawezi kuweka pumzi ya mtu wala kuleta mvua juu ya ardhi. Ndio maana hata wao watakufa kama wengine na watarejea kwenye asili ya viumbe vyote kama wengine hivyo kuwategemea CCM na kukufuru Mungu ni laana tosha kwa Taifa hili.
Kataa CCM, kataa Wahuni ,kataa wauaji na watakaji ,kataa tozo kubwa ,kataa , mfumuko wa bei,kataa matumizi makubwa ya serikali , kataa ufisadi , kataa kuuzwa kwa ardhi yetu ,kataa kumkufuru Mungu na kutukuza CCM ,kataa machawa .
Pigeni Kura nyingi kwa ACT na Chadema kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa . Hivi ni vyama vyenye kumjua Mungu wa Haki.