TANZIA Mwana-JamiiForums, Thadei Ole Mushi afariki dunia

TANZIA Mwana-JamiiForums, Thadei Ole Mushi afariki dunia

Anahubiri injili
 

Attachments

  • IMG-20240204-WA0584.jpg
    IMG-20240204-WA0584.jpg
    64.8 KB · Views: 2
Mbona siku hizi watu wanafariki wadogo sana!

Ndani ya miezi miwili hii, nimeshakutana na taarifa za vifo si pungufu ya 10 kwa watu ambao ni 45 kurudi chini...
Kunaweza kukawa na sababu nyingi lakini sababu moja kubwa ni hii ,

Mithali 10:27 SRUV​

Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa .

Kutokana na kupungua au kutoweka hofu ya Mungu , siku hizi dhambi za kila namna zimekuwa ndio mtindo wa maisha. Watu wanadhulumu bila haya , uzinzi na uasherati ndio imekuwa ujanja, unywaji wa pombe na kamali vimekuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya vijana wengi. Hauwezi ukavunja kanuni za Mungu halafu ukategemea utakuwa salama.. Leo unaweza ukajiona mjanja , lakini jua utalipa tu siku moja, kwa kuwa apandacho mtu ndicho atachovuna.
 
Siamini hili, Old Mushi alikuwa Chawa mpaka uteuzi tu, hajawahi kuwa threat Kwa serikali
Kwenye jukwaa hili alipunguza threads. Majukwaa mengine aliongeza posts nyingi. Misimamo yake juu yauwekezaji nchini kama hawakumlisha maneno kwenye mitandao hiyo...yalikuwa yakufikirisha uwanachama wake. Apumzike kwa Amani!
 
MwanaCCM na MwanaJF Thadei Ole Mushi amefariki dunia.

Ole Mushi alikuwa anaugua kwa muda mrefu.

Thadei amefariki duniani asubuhi hii katika hospitali ya moyo JKCI, Muhimbili.

Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi na atupe nguvu na faraja.

Zaidi soma Ole Mushi ni mgonjwa sana.

View attachment 2893963View attachment 2893962
Picha: Ole Mushi enzi za uhai wake
Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele. Ni vijana waliochangia kuchangamsha fikra za Watanzania. Tunamshukuru Mungu kwa nafasi aliyotupa kuwa naye katika mapambano ya fikra. Raha ya milele umpe Ee Bwana. AMINA.
 
MwanaCCM na MwanaJF @Thadei Ole Mushi amefariki dunia.

Comrade, pumzika.


Michango yako chamani na kwenye Jamii, yatadumishwa.

R.I.P Brother.

Sincerely, you will be missed.

Poleni Wafiwa.
Poleni sote JamiiForums,

"Where we dare to talk Openly.
 
Back
Top Bottom