Mwana Siasa Yupi hapa Nchini Mwenye Uwezo wa Kukusanya Na kubeba watu Wengi Kiasi hiki Cha Rais Samia?

Mwana Siasa Yupi hapa Nchini Mwenye Uwezo wa Kukusanya Na kubeba watu Wengi Kiasi hiki Cha Rais Samia?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Huu ni Zaidi ya Upendo ndugu zanguni Watanzania.Haijawahi kutokea hapa Nchini pengine hata ndani ya Bara zima la Afrika kwa Mwanasiasa kupendwa ,kukubalika,kuungwa mkono,kusikilizwa ,kufuatwa ,kubeba na kukusanya watu Wengi kiasi hiki Utafikiri watu wanavutwa kwa sumaku kutoka majumbani Mwao.

Embu niambieni ni Mwanasiasa yupi hapa Nchini kwenye uwezo na ushawishi wa kuwaleta pamoja watu kumsikiliza yeye kwa wingi kiasi hicho? Nani mwenye uwezo huu? Nani mwenye ubavu,nani mwenye nguvu za aina hiyo? Nani anapendwa Nchi hii kumzidi huyu Mama mwenye moyo wa upendo, ukarimu, uzalendo,unyenyekevu na upole?

Nani anaweza kuwafanya watu wengi kiasi hiki wakaacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumsikiliza yeye tu? Zaidi ya Rais Samia ni Nani mwingine anaweza wafanya watu wakimbie mbio kuwahi nafasi viwanjani na kufurika mpaka kukosa nafasi ya kupita sisiminzii ili tu wamsikilize?

Rais Samia kwa hakika siyo mtu wa kawaida ,ni mtu na nusu ,ni nyota kwelikweli,ni nuru popote pawapo na giza.ni tumaini popote pawapo na kukata tamaa. Ni vipi unaweza mzuia Mama huyu kugombea Urais? Ni vipi unaweza mshinda mama huyu kushinda kwa kishindo? Utamzuia kupitia nini? Kwa njia ipi? Kwa sera zipi? Kwa kigezo kipi unaweza mzuia Mama huyu Chaguo la Mungu kurejea ikulu kwa awamu ya pili hapo Mwakani? Ni vipi unaweza kata jina la huyu Mama kwenye Urais ndani ya CCM? Nani atakuelewa? Nani atakukubalia na kunyamaza? Huoni itasababisha machafuko na vurugu Nchini?

Hivi bado hamjatambua ya kuwa huyu Mama ni Chaguo la Mungu Mwenyewe? Hamjatambua bado kuwa kainuliwa na mkono wa Mungu na hata sasa anaongoza Nchi kwa kibali cha Mungu Mwenyewe? Mnataka mpewe ishara gani mpate kuamini?muoneshwe nini na kitu gani na picha zipi mpate kuamini enyi watanzania?
Screenshot_20240928-224331_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Wengine hapo wamekuja kushangaa tu land cruiser.
Yaani bendera fuata upepo.
Hawana moja wala mbili.
Kulia twende kushoto twende.
Ccm wasibadili mganga wao
 
Wengine hapo wamekuja kushangaa tu land cruiser.
Yaani bendera fuata upepo.
Hawana moja wala mbili.
Kulia twende kushoto twende.
Ccm wasibadili mganga wao
Nenda na wewe ukaitishe mkutano mahali popote pale hapa Nchini hata sokoni tu uone kama utapata watu hata hamsini tu wa kuja kukusikiliza.
 
Kwangu mimi hata angechukiwa na kutokukuasanya mtu hata mmoja ila mambo yakaenda vema na kitaa maisha yakapungua ugumu...

Nikitaka watu wa kukusanya watu nitawatafuta wasanii au kwenda kwenye game ya mpira...
 
Kwangu mimi hata angechukiwa na kutokukuasanya mtu hata mmoja ila mambo yakaenda vema na kitaa maisha yakapungua ugumu...

Nikitaka watu wa kukusanya watu nitawatafuta wasanii au kwenda kwenye game ya mpira...
Watanzania wanampenda ,kumkubali na kumuunga mkono Rais Samia kwa hiyari ya mioyo yao
 
Nguvu ya buku Tano Tano.
Mimi naijua hiyo. Tukiwa boarding Lindi high school akija PM, Rais au vice president tulipewa offer ya kuhudhuria mkutano huku tukiambiwa tuvae nguo za nyumbani. Cha ajabu shule tulikuwa haturuhusiwi kuwa na home garment lakini siku akitimba mkuu unaambiwa vaa za nyumbani azima hata kwa jirani . Mnaujaza uwanja.
Kwa kweli mtoa mada huna akili.
Ni tahira.
Mtu yeyote anayefanya kazi ya kumsifia binadamu mwenzake huyo ni tahira.
 
Back
Top Bottom